Waliomfitini Dr Mwele kwa Magufuli, wanajisikiaje?

Hebu acha uongo Dr Mwele hakufitiniwa na mtu yeyote yule alijifitini yeye mwenyewe! Jiulize ile Zika ilikwenda wapi?
Na ile ya COVID-19 iliishia wapi?! Ikiwa mlidanganywa hata kwenye ugonjwa wa wazi kama COVID-19, seuze Zika?!
 
Kama sikosei alitangaza matokeo ya utafiti na wala sio janga la ugonjwa.
Ulichoandika no utoto

Utafiti kutangaza ndio kutangaza janga kwenyewe mfano Leo mtafiti aibuke na kusema kwenye utafiti wake kagundua kuna wagonjwa laki moja was Ebola unafikiri hajatangaza kuwa Tanzania kuna Ebola?

Kwebye utafiti wake kusema katika utafiti wangu nimegundua kuna wagonjwa was Zika usichoelewa hapo nini?
 
Rejea interview ya mtoto wa dada yake JPM yule alokuwa akiwania Ubunge wa Kawe na Gwajima
 
Nyundo babu kubwa na imetua kichwani mwake. Ni majaaliwa kama atasimama
 
Msifanye watu humu wajinga si kila tafiti zikifanyika basi unakurupuka kutangaza hasa tafiti za magonjwa makubwa...usifananesha utafiti wamagonjwa makubwa na utafiti wa vikoba!


Haya ndo mawazo ya kuficha data ili watu wasipaniki huku wanateketea.


Utafiti wowote unapofanyika lazima uhusishe mamlaka zinazosimamia tafiti husika. Katika utafiti ule hakuna mamlaka iliyosema haikuhusishwa.

Zika ipo Uganda tangu 1956, na ukumbuke moja ya kazi ambayo imempa cheti Dr. Mwele ni Tropical neglected diseases. Hivyo, suala ka kwanza lilikuwa ni kutambua uwepo kwanza. Baadaye utaangalia ukubwa wa tatizo na nini kifanyike ili kuzuia au kupunguza tatizo.

Kimsingi na mantiki hakuna janga lililotangazwa pale, isipokuwa kama hutaki kuelewa. Zika athari zake unaishi nazo na inakupa kinga ya kudumu. Utafiti uliofanyika ulikuwa wa kuangalia chanzo kwa muda uliopita na si kwamba siku aliyotamka ndo tatizo lilipotokea/ulikuwa mkusanyiko wa tafiti ndani ya mwaka kama jarida.

Tofautisha tatizo la ugonjwa kama ebola ambao dalili na athari zake ni za papo kwa hapo. Leo hii hata hao watoto bado wapo na madhira yako palepale. Huwezi kwenda Kongo leo ukatofautisha mtu aliyepata ebola akapona na ambaye hajapata kabisa.

Kasome tafiti juu ya binadamu na magonjwa ni kiasi gani cha watu hupenda kuambiwa ukweli juu ya kinachowasibu hata kama ni kikubwa kwa kiasi gani dhidi ya wale ambao wanasema nifiche tatizo langu nisijue na uone matokeo ya kuficha dhidi ya kusema ukweli.

Siku gani dunia itasimama ili useme ukweli? Mnapenda tafiti za matumizi ya kondomu kuongezeka.

NB: Utafiti hupingwa kwa tafiti na si kwa mwanasiasa huku anapigwa kiyoyozi ofisini.
 
Zika ipo mpaka kesho acha uongo

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Btw, tuliambiwa humu kuwa Magufuli alikufa mapema kwa sababu ya madhambi yake; sasa huyu binti amekufa kwa sababu ya madhambi ya nani?
Conclusion za makamanda wakati mwingine ni za kijinga sana!
Wako wengi waliokufa natural death kama Dr Mwele lakini Magufuli alikufa kwa sababu ya madhambi yake, hili hakuna ubishi
 
Asante Lukonge kwa kuweka taarifa sahihi.

Huyu Leak ni mmoja tu kati ya mamilioni ya Watanzania ambao walikuwa "brainwashed" na uwongo wa Magufuli. Na kwa UJINGA wa watu hawa Magufuli aliwatumia kama mtaji wa kujenga falsafa zake za kidikteta.

Mtu pekee alipaswa kumpinga Dr Mwele ni mtafiti mwingine wa magonjwa ya binadamu lakini siyo Ummy Mwalimu Wala Magufuli
 
Kile chuma mkuu, miaka 100 mbele wajukuu zetu kuja kupata raisi wa hivi, then mafisadi yamejipanga kila engo kuhakikisha hawafanyi tena kosa mtoto wa mlala hoi kuingia kwenye system.

Tukae mkao majina yale yale uliyokuwa unayasikia toka miaka ya 1980 yataendelea hadi vitukuu na vitukuu
 
Tshs 1.5 trilliini aliyo ulizia CAG ilienda wapi?
Vizazi na vizazi vitaendelea kujiuliza hili swali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…