You are far behind the theme. Kinachoongelewa kiko long rooted. Leo hii nikianza kukuleta tangu mwanzo wa hizi chanjo, wapi kulikuwa violated, grounds za underlying worries, physical evidences, na intent ya ku hide serious immediate adverse reactions, background ya covid-19 pandemic, move ya kuibatiza endemic etc, kwe wewe uliyekariri clinic trials na uka assume kwamba kila kitu kinafanyika namna uliyokariri, itakuwa vigumu.
Nenda kasome uelewe, uje na relevant points. Usinishushe huko ni chini sana na mbali na mahala nilipo mimi.
Una evidence leta kama unajua unachofanya na una uhakika.
Tuko kwenye mjadala wa wazi hapa. Hakiki chanzo chako cha taarifa na wataalamu wako kabla haujazimwaga hapa.
Kwa hiyo, wewe ndo una vifaa vya kuhakiki dawa kuliko FDA zilizoko kila nchi dunia nzima au hata hujui utaratibu wa kuingiza dawa kila nchi unajitegemea na FDA ya nchi husika? Wao waliozipokea hizo chanjo toka kwenye hizo kampuni ni hamnazo, ila wewe ndo una siri ya dunia.
1: Sijui kama unajua Paracetamol uliyokunywa mwaka jana ilipitia mnyororo gani kukufikia kwenye mdomo wako, lakini unashupaza shingo ya chanjo.
A: SARS ilipowapiga Wachina 2002 -2004 mbona hamkusema ni hujuma?
B: SARS ilipopiga Middle East 2012 mbona hamkusema hujuma?
Mnajua watu walifanyia kazi kiasi gani hayo yaliyotokea wakati huo?
Unajua simu unayotumia kuandika huu utopolo inaweza kutumika kama siraha ya maangamizi kwako?
Theory ipi ya uchumi inakwambia ua soko la bidhaa zako ili ufanikiwe?
Wewe ni threat kiasi gani kwa mzungu mpaka ahangaike na wewe kiasi hicho wakati mawazo yako mwenyewe haujitoshelezi/not innovative hata kwa graceful environment uliyonayo?
Kama huwezi kuamini taratibu na vyombo tulivyojiwekea na misingi yake basi jifahamu unakuwa Paranoid. Utaanza kukikimbia kivuli chako.
Dawa zote zilizoko madukani, hakuna hata moja ametengeneza binamu yako, kaka yako, dada yako, ukiumwa unaenda wapi?
Ni nani amesimamia hizo dawa mpaka ziko dukani hapo?
Umeshindwa kutenga hata kisamvu na Cyanide unakula, lakini unaona una ufahamu wa hali ya juu kuhusu mfumo wa ugunduzi, kuendeleza na kusupply dawa individually kuliko institution zilizopewa mamlaka kisheria.
Nenda katembelee crinical trial hata moja jifunze nini kinafanyika ili wakati unarudia kusoma haya mambo yako ujione unavyozunguka porini.
2: Mnakomaa na conspiracy theories na taarifa za anti-vaccine groups na kuona ndo uelewa wa hali ya juu. Hawa watu wapo tangu 1956 kazi yao ni kuwazoazoa watu kama wewe. Kuna mataifa yalishaonja joto ya jiwe kwa kujitoa kwenye mpango wa chanjo hata hizo ulizochoma za under five na walikiona cha moto wakarejea.
Waulizie Nigeria 2003, kule Kano, Zamfara na Kaduna walipata nini na tatizo lilikuwa nini? Na nchi nyingine zilizolishwa hayo unayoyakumbatia mifano ipo mingi ya anti-vaccine campaign groups.
Usishadadie kila unachoona kimeandikwa kwenye mtandao ukaona ndo uhalisia.