Ndinani,
Historia ya Lucy Lameck nimeipokea kutoka kwa Mzee Yusuf Olotu.
Hebu soma historia ya TANU Moshi hapo chini:
''Wakati sehemu nyingine zikihamasika na harakati za kudai uhuru Moshi ilikuwa katika usingizi. Uongozi wa TANU Arusha, chini ya Japhet Kirilo ulikuja Moshi pamoja na Rajab Chamshama na Robert Otieno kuja kuchunguza kwa nini TANU ilikuwa inachelewa kusajiliwa Moshi.
Viongozi hawa waliitisha mkutano wa uchaguzi Welfare Centre ambao ulihudhuriwa na watu takriban 25, mmoja wao akiwa Yussuf Ngozi.
Mkutano ule ulimchagua Mzee Yussuf Ngozi kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa tawi la TANU Moshi mjini.
Taratibu Kimalando akawekwa pembeni.
Katika halmashauri ya kwanza ya tawi lile alikuwapo msichana mdogo wa miaka 24, Lucy Lameck ambae baadaye alikuja kuwa waziri katika serikali ya wananchi.''
Lucy alikuwa mwanachama Moshi na si Dar es Salaam na TANU Moshi ilikuwa imechelewa sana kuanzishwa.