Kweli historia ya nchi yetu inayofundishwa mashuleni imechujwa chujwa lakini hata hivyo tunahitaji historia ambayo ni ya kweli bila chembe za bias kuwa jamii moja dio Ilikuwa zaidi kuliko nyingine katika harakati za kudai uhuru ili hali wanannchi wote irrespective of religious affiliation walishiriki!
Nitakupa mfano mmoja dhahili unaooneshwa na Mohamed Said nao ni pale anaposema babu yake aliongoza migomo mitatu ya wafanyakazi wa shirika la Reli [TRAU]; lakini wote tunajua kuwa wakati huo kufanikiwa kwa migomo ya wafanyakazi halikuwa jukumu la mtu mmoja [ Mohamed anataka tuamini hivyo] bali ushirikiano wa wengi!! Na sio ushirikiano wa chama cha wafanyakazi wa reli peke yao bali pia ushirikiano na vyama vingine vya wafanyakaza kwa mfano wale waliokuwa wanafanya kazi mikongeni wakiongozwa na wakina Mkello!!!
Tunahitaji historia ya kweli isiyokuwa na bias ya aina yeyote ya kupendelea sehemu ya jamii!!
Ndinani,
Nadhani umeninukuu au umeuelewa mfano wa babu yangu ''out of context.''
Nimetoa huo kama mfano wa kukufahamisha kuwa historia hii ninayoieleza hapa mimi ni mwenyeji nazungumza kitu ninachokijua.
Sikuwa na maana kuwa migomo yote hiyo kaiongoza peke yake.
Bahati mbaya sana kwako kuwa umeelewa vinginevyo.
Tuje kwa hili la ''jamii moja.''
Ikiwa huamini mimi sina tatizo na hilo lakini historia ya uhuru wa Tanganyika ndivyo ilivyo na ushahidi uko tena mwingi tu.
Angalia historia ya Abdul Sykes.
Baba yake ni muasisi wa African Association mwaka wa 1929 na kaacha mswada ambao leo ni sura katika kitabu alichohariri John Iliffe.
Hili nimelieleza mara nyingi hapana haja ya kulirudia.
Sasa tuje kwa babu yangu Salum Abdallah.
Yeye hakuwa muasisi wa African Association kuwa alikuwapo katika ule mkutano wa uasisi lakini alikuwa moja wa wanachama wa mwanzo kabisa.
Babu yangu na Kleist Sykes walikuwa majirani nyumba zao zikitazamana hapo Mtaa wa Kipata na wote wakifanya kazi Tanganyika Railways katika miaka ya 1920s.
Hii ndiyo sababu kubwa unaniona historia hii naijua vizuri.
Babu yangu alihamia Tabora mwaka wa 1947 baada ya Loco Shed idara ambayo alikuwa akifanya kazi kuhamishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Tabora.
Akiwa Tabora ndiko alipoongoza hiyo migomo niliyoitaja.
Mwaka wa 1953 TAA Tabora ilimtuma Germano Pacha TAA HQ na maelekezo aliyopewa ni kuwa afike nyumbani kwa Abdul Sykes na amweleze mipango ya TAA Tabora kutaka kuunda chama cha siasa.
Hiki ni kisa kirefu hapa nafupisha laikini nimekieleza katika kitabu cha Abdul Sykes kwa ukamilifu wake.
Jibu ambalo Abdul alimpa Germano Pacha ni kuwa Tabora wawe na subra mipango inafanyika TAA HQ na ikikamilika watafahamishwa.
Huu ndiyo ukawa mwanzo wa mikutano ya siri Town School, Tabora kila Jumapili na aliyekuwa akiwafungulia darasa kukutana hapo alikuwa Abubakar Mwilima ambae alikuwa mwalimu hapo na agenda yao ilikuwa moja tu nayo ni kupata taarifa kutoka TAA HQ New Street kuhusu chama cha siasa kudai uhuru wa Tanganyika.
Haya ndiyo maisha ya babu yangu yalivyofungamana na TANU.
Ulipokuja mwaliko wa mkutano wa TAA wa mwaka wa 1954 wa kuunda TANU Germano Pacha kama Katibu wa TAA Western Province akahudhuria mkutano ule.
Mchango mkubwa wa kumwezesha Pacha kusafiri kuja Dar es Salaam alitoa babu yangu na ilikuwa shs. 20.00.
Hii ndiyo historia ya wazee wangu sidhani kama kuna mtu ana haki ya kunikataza kuihifadhi historia hii kwa kuwa tu ni historia ya uhuru wa Tanganyika.