Waliomsindikiza Mwalimu Nyerere safari ya kwanza UNO 1955

Waliomsindikiza Mwalimu Nyerere safari ya kwanza UNO 1955

Na vipi kama wasomaji ni 2% tena wa misikitini tu?

Wakati huo 98% wana historia tayari iliyotangulia na wakaikubali na kuiweka ubongoni na mioyoni?

Historia ya nchi yetu pia imeandikwa na wakoloni waliotawala nchi hii; hivyo nao waliiandika kutokana na biases zao, ingawa waliindika muda mrefu sana hiyo haiwapi uhalali kuwa historia waliyoiandika ndio sahihi!! Hivyo kuna kila sababu pale inapotia shaka kuwa chunvi imeongezywa hatuna budi kudadisi na kutafuta ukweli.

Hivyo hivyo kwa kwa sheikh Mohamed Said , kitabu kuwa Kiko sokoni kwa miaka ishirini na moja hakituondolei uhalali wa sisi kuhoji kama yale yaliyoandikwa yalikuwa na ukakasi fulani!! Watu wana haki ya kutaka ufafanuzi pale ambapo panaonekana kuna kitu ambacho hakieleweki vizuri ili kurekebisha mambo.
 
Na vipi kama wasomaji ni 2% tena wa misikitini tu?

Wakati huo 98% wana historia tayari iliyotangulia na wakaikubali na kuiweka ubongoni na mioyoni?
Azarel,
Kipi kinakufanya wewe useme kuwa kitabu cha Abdul Sykes kinasomwa misikitini tu?

Hiki kitabu kilichapwa mwaka wa 1998 London na kikfanyiwa book review na wataalamu wa African History kama John Iliffe, James Brennan na Jonathon Glassman na kuchapwa katika Cambridge Journal of African History.

Naamini unafahamu maana ya kitabu kungizwa katika Cambridge Journal of African History.

Kitabu hiki kinasomeshwa na vyuo vikuu Ulaya na Marekani nashangaa wewe kusema kuwa kinasomwa misikitini.

Nakala ya Kiswahili ilichapwa Nairobi mwaka wa 2002.
Sina tatizo na historia ''iliyotangulia.''

Sina tatizo kwani ndiyo historia waliyoiandika na kwa hakika ndiyo historia inayotambulika.
Kitabu cha Abdul Sykes sasa kina miaka 21 na kimebadili historia ''iliyotangulia.''

Ushahidi ni huu kwa karibu miaka 10 tuko hapa JF tunakijadili kitabu hiki.
 
Attachments

  • JAMES BRENNAN IOWA.JPG
    JAMES BRENNAN IOWA.JPG
    12.9 KB · Views: 2
  • PROF. JAMES GIBLIN UNIVERSITY OF IOWA.jpg
    PROF. JAMES GIBLIN UNIVERSITY OF IOWA.jpg
    16.2 KB · Views: 3
Historia ya nchi yetu pia imeandikwa na wakoloni waliotawala nchi hii; hivyo nao waliiandika kutokana na biases zao, ingawa waliindika muda mrefu sana hiyo haiwapi uhalali kuwa historia waliyoiandika ndio sahihi!! Hivyo kuna kila sababu pale inapotia shaka kuwa chunvi imeongezywa hatuna budi kudadisi na kutafuta ukweli.

Hivyo hivyo kwa kwa sheikh Mohamed Said , kitabu kuwa Kiko sokoni kwa miaka ishirini na moja hakituondolei uhalali wa sisi kuhoji kama yale yaliyoandikwa yalikuwa na ukakasi fulani!! Watu wana haki ya kutaka ufafanuzi pale ambapo panaonekana kuna kitu ambacho hakieleweki vizuri ili kurekebisha mambo.
Ndinani,
Kwa hakika nakuonea huruma sana.

Nakuonea huruma kwa sababu kama wewe ungekuwa unataka kuhoji ungeanza kuhoji kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni ukauliza wamewezaje kuandikia historia ya TANU bila kusoma Nyaraka za Sykes.

Kama tujuavyo hiyo African Association imeundwa na wao mwaka wa 1929.

''Ukakasi,'' ungeanza kuchubua koo lako hapo si kwangu mimi niandikae historia ambayo imekubalika kwingi na nadhani nishakueleza kuwa ndiyo ikawa sababu ya Kleist Sykes kutiwa katika mradi wa Harvard na Oxford University Press New York, (2011) Dictionary of African Biography (DAB) na mwandishi nikiwa mimi.

Nakuhurimia sana ndugu yangu kama unadhani unaweza kusimama na mimi kwa kuandika mistari mitatu JF.

Kunijibu mimi unahitaji uandike kitabu kizima.

Wako waliochomwa na kitabu cha Abdul Sykes na wameshinikiza iandikwe historia nyingine badala ya ile ya Chuo Cha CCM Kivukoni.

Je unafahamu sababu ya kutakiwa kitabu kingine cha historia ya TANU?
 
Hapa umemfurahisha Sanaa mzee Mohammed Said na wenzie kina FF

Nenda akakununulie gahawa

Hahahaha.........!!!!
Azarel,
Ndugu yangu mimi nakusihi kitu kidogo sana.
Ikiwa unataka kutaja jina langu basi litaje kwenye jambo la adabu na staha.

Mimi siko hapa kwa mzaha na kejeli.
Naamini umenielewa na utaniwekea staha kama nikuwekeayo wewe.
 
Hawezi kumtaja Mkristo, na hata akimtaja...atamtaja yuko na jazba tayari na kaghafilika moyoni.

Wallah,
Azarel,
Katika picha hiyo kuna wanawake wawili hadi leo sijaweza kupata majina yao.
Ungesoma ''caption,'' ya hiyo picha usingeandika hayo.
 
Eti mzee mmoja wa bagamoyo akiitwa Sheikh ramia ndo alikua anamsomea mwalimu dua na maulid

Alafu eti mwalimu suruali yake ya kwanza alishonewaga na mzee mmoja hapo magomeni,
Kabla ya hapo alikua ananipigia vipensi vya ukweli eti!!
Ila mi sijakubali moja kwa moja mpaka nifanye uchunguzi
 
Nakuhurimia sana ndugu yangu kama unadhani unaweza kusimama na mimi kwa kuandika mistari mitatu JF.

Kunijibu mimi unahitaji uandike kitabu kizima

Usinionee huruma kwani mimi sio wa kuhurumiwa na mtu kama wewe. Mohamed unaweza kuandika kitabu kikajaa upuuzi na mwingine akaandika paragraph moja ikawa imeja busara na substance kwahiyo ujue kwamba quantity does not always mean acceptance!! Ujifunze kuwa mvumilivu na kukubali pale hoja zako zinapohojiwa.
 
Ni Uongo mtupu

Wao wenyewe walikuwa wanavaa kanzu wakitoka kwenda masjid na wakibaki nyumbani wanavaa vikoi.

Sawa iweje wamshonee Mwl. Suruali?
Eti mzee mmoja wa bagamoyo akiitwa Sheikh ramia ndo alikua anamsomea mwalimu dua na maulid

Alafu eti mwalimu suruali yake ya kwanza alishonewaga na mzee mmoja hapo magomeni,
Kabla ya hapo alikua ananipigia vipensi vya ukweli eti!!
Ila mi sijakubali moja kwa moja mpaka nifanye uchunguzi
 
Usinionee huruma kwani mimi sio wa kuhurumiwa na mtu kama wewe. Mohamed unaweza kuandika kitabu kikajaa upuuzi na mwingine akaandika paragraph moja ikawa imeja busara na substance kwahiyo ujue kwamba quantity does not always mean acceptance!! Ujifunze kuwa mvumilivu na kukubali pale hoja zako zinapohojiwa.
Ndinani,
Sijapatapo kuandika upuuzi katika maisha yangu na ndiyo maana unaona mkiona jina langu mnahudhuria kwa wingi kusikiliza nimesema nini.

Wala sijaandika upuuzi hata mstari mmoja wa maneno matatu.

Hii ndiyo sababu nimepata marafiki wengi katika ulimwengu huu wa fikra.
Utashangaa ni ''thesis'' na vitabu vingapi jina langu liko kwenye tabaruk.

Angalia magazeti mangapi hapa nyumbani yanachapa makala zangu na mengine kwa kuniomba makala wanapotaka kufanya toleo maalum mathalan Nyerere Day.

Wala sina tatizo na uvumilivu ndiyo maana unaona siku zote hapa anaetukanwa na kukejeliwa ni mimi.

Sina cha kujifunza hapa kutoka kwenu.
Nitakufahamisha.

Mimi nimesomeshwa ilm ya mnakasha (majadiliano) na marehemu Sheikh Haruna Fakir.
Akiniambia, ''Sikiza Mohamed mjadala la kwanza muhimu ni adab.''

Pili akinifunza akisema ''Ulijue somo lako vyema na tatu weka ubongo wako wazi kujifunza kwa unaejadiliananae kwani mtu haingii kwenye mjadala kushinda bali kuongeza elimu kwa kusikiliza kile asichokijua.''

Hapa sijakutana na mtu wa kunifunza lolote kwa hakika.

Siku zote nawaona wanakuja katika mjadala kwa kuwa wamechomwa kile walichodhani ndiyo kumbe siyo na akili zao zinakataa kuamini kile wanachosikia na ndiyo ukweli wenyewe.
 
Ni Uongo mtupu

Wao wenyewe walikuwa wanavaa kanzu wakitoka kwenda masjid na wakibaki nyumbani wanavaa vikoi.

Sawa iweje wamshonee Mwl. Suruali?
Azareli,
Hao wenye kuandika vitu kama hivyo ni watu wajinga wala wasikusumbue.

Ila nakutahadharishe ufikiri kabla ya kutamka.
Kanzu na kikoi kwetu sisi ni vazi la asili wala si kielelezo cha udhalili.

Mimi nina kanzu kadhaa pamoja na vikoi.
Picha hiyo niko Kenyatta University Nairobi angalia nimevaa kanzu.
 
Attachments

  • MOHAMED SAID KENYATTA  UNIVERSITY.jpg
    MOHAMED SAID KENYATTA UNIVERSITY.jpg
    20.2 KB · Views: 2
Mimi nimesomeshwa ilm ya mnakasha (majadiliano) na marehemu Sheikh Haruna Fakir.
Akiniambia, ''Sikiza Mohamed mjadala la kwanza muhimu ni adab.''

Pili akinifunza akisema ''Ulijue somo lako vyema na tatu weka ubongo wako wazi kujifunza kwa unaejadiliananae kwani mtu haingii kwenye mjadala kushinda bali kuongeza elimu kwa kusikiliza kile asichokijua

Mwalimu wako alikuhusia mambo matatu ya hekima na busara sana; endelea kumuenzi kwa kuyazingatia katika maisha yako!!
 
Azareli,
Hao wenye kuandika vitu kama hivyo ni watu wajinga wala wasikusumbue.

Ila nakutahadharishe ufikiri kabla ya kutamka.
Kanzu na kikoi kwetu sisi ni vazi la asili wala si kielelezo cha udhalili.

Mimi nina kanzu kadhaa pamoja na vikoi.
Sio mavazi yenu ya asili, Nguo za asili za Mtu mweusi ni magome ya miti.

Kanzu na vikoi ni mavazi ambayo Waafrika walicopy kutoka kwa Waarabu.
 
Mohamed Said shukrani kwa darasa na elimu.

Lakini kuna mambo mawili nimeyaona, kwanza kuna mchangiaji mmoja Ndinani amerejea mara kwa mara kwamba huyo mwanamke ni Lucy, lakini umeendelea kupinga ilihali yeye anaeleza kwanini anasema ni Lucy na wewe unatoa fafanuzi ambazo huenda zikawa ni za kweli lakini hazijibu ikiwa huyo ni Lucy au sie.

Jambo la pili Kiranga ametolea mfano kuonyesha umuhimu wa kufanya peer review (kutafuta ukweli wa jambo kwa zaidi ya chanzo kimoja tena vyenye kukubalika na kusadikika kuwa na mamlaka kuhusu uwezo wao) hii inamaanisha jambo lolote ili kuondoa sintofaham ya maoni, taarifa au jambo kuchukua upande mmoja wa habari.
Matokeo yake umeeleza mambo mengi sana kukuhusu wewe binafsi, sio jambo baya kitu ambacho hata Kiranga angeweza kujimwambafy akatuonjesha yeye ni nani lakini ameamua kujikita kwenye hoja iliyopo mezani.

Kwa ufupi nnachokusema ni kwamba, unaweza kuwa na uelewa au taarifa nyingi sana lakini kuweza kujiridhisha kutoka vyanzo kadhaa vyenye vigezo ni muhimu sana. Pia haimaanishi unachokijua wewe ndio kipo sahihi na wengine hawaelewi au taarifa zao si za kweli.

Mwisho kabisa kujaribu kwenda kwenye hoja moja kwa moja bila kuweka mambo mengi kama hakuna ulazima.

Endelea kutupa shule kadri upatapo nafasi mkuu. Shukran

Umeeleweka vema
 
Sio mavazi yenu ya asili, Nguo za asili za Mtu mweusi ni magome ya miti.

Kanzu na vikoi ni mavazi ambayo Waafrika walicopy kutoka kwa Waarabu.
Azarel,
Hakika usemayo lakini hivi sasa ni mavazi yetu ya asili.
 
Mwalimu wako alikuhusia mambo matatu ya hekima na busara sana; endelea kumuenzi kwa kuyazingatia katika maisha yako!!
Ndinani,
Maalim Haruna...
Huyo mtu mwingine kaka.

''Mohamed unataka kujibu matusi?

La la la...hujibu matusi na unapotukanwa unakaa kimya.
Jua huyo ushamshinda hana hoja sasa yeye anaona hoja yake ni matusi na kejeli.

Katisha mjadala hadi hasira zake zipoe ndipo akiwa atapenda endelea na mjadala.''

Maalim Haruna huyo.
 
Mimi naona kuna kurunzi kali liliwamulika na kujua malengo ya baadhi ya wapigania uhuru baada ya kupata uhuru, Jambo lililopelekea Mwalimu kutumia busara kufutilia mbali ushiriki wao jambo lililoleta umoja wa kitaifa mpaka sasa
 
Nemo...
Umoja wa kitaifa...
Neno zito sana umesema.

Umoja wa kitaifa utachukua miaka mingi sana kupatikana.
Unaandika kwa hamaki na katika historia ambayo huijui.

Mimi historia hiyo yote baada ya uhuru nimetafiti na kuandika.
Naijua vizuri sana.

Iko paper chukua muda uisome usifanye haraka ya kutaka kurejea hapa kujadiliana isome kwa utulivu utayaelewa matatizo yanayokabili nchi yetu:
 
Huyu mzee amejaa hila, na maandishi yake mimi nayaona kama ya hovyo tu kwakuwa yamejiegemeza ktk kubagua watu kidini kwa kujifunika na blanketi la kujifanya anaijua sana historia ya nchii!!
Hayo maneno hapo ni uthibitisho tosha!

Nimeona vitabu vyake vinauzwa misikitini kariakoo, nikacheka kimoyomoyo!

NAONA MZEE BABA UNAUMIA SANA UNAPOONA MZEE SAIDI ANATUPATIA UKWELI AMBAO KWA UJANJA WA MCONGA NA ROMAN WALIIFICHA. ''THE TRUTH WILL SET YOU FREE''
USIHOFU WAJUKUU ZAKO NAO WATAKUJA KUANDIKA JINSI PENGO ALIVYO ISAIDIA CCM BUT IN MEAN TIME MZEE SAID YUPO SAHII TENA ANATUWEKEA DOCUMENT KAMA PICH AS EVIDENCE UNLIKE WEWE NA AKINA FOXY MNABWABWAJA WITHOUT REFERENCES
 
Back
Top Bottom