Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Bado udikteta upo Tanzania.
 
Uandamane au usiandamane maazimio yao watapitisha tu!! Bongo unafiki umejaa sana yaani mtu anaratibu maandamano halafu anakula nyoya.Anawaachia msala muhangaike na mbu wa central.
Mi ndo maana kila siku nasema Bungeni kitu kikipita hakuna maajabu yatakiondoa, zilikuwepo harakati za Tozo ila sasa hazipo tena, ikaja ushoga, sasa ni bandari yataisha
 
Vipi mbona una gadhabu sana? Au mmechezea kichapo
 
Hahaha hahahaha hahahaha nyie watu mna roho mbaya Sana, mwenzenu tangu asubuhi hata chai hajagonga mnahimizana apewe maua wakati hata maji hamjampelekea.
 
Mkuu mbona POVU kama huyo kiumbe wa kwenye AVATAR yako.................
😌😌🙂🙂☺️☺️😊😊
 
Hapo wangepaswa wasimame wazee/wababa na wamama kwanza maana ndo mizizi ya unafiki na woga ilipoanzia ndipo vijana wafuate nje na hapo vijana wataishia kuumizwa tuu na kuonekana kama wahuni fulani.
 
Demokrasia inayoimbwa hata nchini ipo tu kwenye majukwaa ya siasa lakini kimsingi hatuna demokrasia......

Maandamano ni haki ya kikatiba ya wananchi kuelezea hisia juu ya mambo yanavyokwenda nchini mwao.....leo hii haki hiyo inaharamishwa na watawala kwa kuwa tu wanaoandamana wanakuja na hoja zinazo wakaraisha...........

Tumeshuhudia maandamano mengi ya kusifia na kupamba.....lakini leo hii hao hao walioruhusu maandamano ya kusifu na kuabudu ndio wanaopinga ya kukosoa............hii inaendeshwa kwa utashi wa watu wachache wanaojiona wao ndio wana hatimiliki na nchi hii badala ya katiba mama..............
 
Hao watu wameonesha njia,,

Nilifikiri tutajitoa wote kwenda kuonesha njia na kumfanya saa100 alale na viatu kumbe walaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…