Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Vijana waandamana jijini Dar es Salaam Tanzania kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na Dubai Ports World pamoja na muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa.

Vijana walioandamana jijini Dar es Salaam kupinga mkataba wa Bandari wamekamatwa eneo la Mnazi Moja.


========

WALIOANDAMANA WAISHIA MIKONONI MWA POLISI

Taarifa za awali zinaeleza kuwa vijana waliokuwa wameandamana kupinga Mkataba wa Bandari eneo la Mnazi Mmoja kuelekea Ikulu ya Magogoni Dar es salaam wamekamatwa na Jeshi la PolisiTaarifa zaidi zitawajia endelea kutufatilia.


MRATIBU WA MAANDAMANO AINGIA MITINI

Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo, a mratibu wa maandamano hayo, Deus Sokkatika hali ya kutofahamika, hajatokea kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mwananchi Digital ilipomtafuta kwa simu zake zote za kiganjani, hakupatikana na katika majina ya waliokamatwa na polisi pia jina lake halikuwepo.

Juni 15 mwaka huu Deus Soka ambaye aligombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo Juni 17 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua akielezwa ni marufuku kufanyika maandamano yoyote.

Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.


Mwananchi
Bado udikteta upo Tanzania.
 
Uandamane au usiandamane maazimio yao watapitisha tu!! Bongo unafiki umejaa sana yaani mtu anaratibu maandamano halafu anakula nyoya.Anawaachia msala muhangaike na mbu wa central.
Mi ndo maana kila siku nasema Bungeni kitu kikipita hakuna maajabu yatakiondoa, zilikuwepo harakati za Tozo ila sasa hazipo tena, ikaja ushoga, sasa ni bandari yataisha
 
Watz ni watu wa ajabu sana yaani kwa jinsi mitandao ya kijamii ilivyo kuwa imechachama kupinga mkataba wa bandari ungeweza kusema kuwa wenda ndo mwisho wa utawala wa Sa100 , lakini leo hii mmeambiwa muandamane ili kuonesha hizo hisia zenu kama mitandaoni. cha kushangaza wote mmeingia mitini.

Kuanzia sasa kama unajijua hukutokea kwenye maandamano leo acha kushinda humu unatujazia page za jf kuukosoa mkataba huo kwa sababu utakuwa unatupigia kelele.

Watu wote mlio kuwa mna mwaga povu humu juu ya huu mkataba alafu mkashindwa kutokea kwenye maandamano ni mbwa waoga na wanafiki wakubwa.
Vipi mbona una gadhabu sana? Au mmechezea kichapo
 
Hii ndio Taarifa mpya ya sasa kutokea Mnazi Mmoja , Dar es Salaam .

Miongoni mwa Maelfu ya Waandamanaji wa kupinga Mauzo ya Bandari kuna Dada mmoja ambaye ametajwa kuwa shujaa wa Taifa hasa baada ya kujitokeza mstari wa Mbele bila kujali vitisho vya Polisi .

Mpeni Maua yake .

View attachment 2662236
Hahaha hahahaha hahahaha nyie watu mna roho mbaya Sana, mwenzenu tangu asubuhi hata chai hajagonga mnahimizana apewe maua wakati hata maji hamjampelekea.
 
Watz ni watu wa ajabu sana yaani kwa jinsi mitandao ya kijamii ilivyo kuwa imechachama kupinga mkataba wa bandari ungeweza kusema kuwa wenda ndo mwisho wa utawala wa Sa100 , lakini leo hii mmeambiwa muandamane ili kuonesha hizo hisia zenu kama mitandaoni. cha kushangaza wote mmeingia mitini.

Kuanzia sasa kama unajijua hukutokea kwenye maandamano leo acha kushinda humu unatujazia page za jf kuukosoa mkataba huo kwa sababu utakuwa unatupigia kelele.

Watu wote mlio kuwa mna mwaga povu humu juu ya huu mkataba alafu mkashindwa kutokea kwenye maandamano ni mbwa waoga na wanafiki wakubwa.
Mkuu mbona POVU kama huyo kiumbe wa kwenye AVATAR yako.................
😌😌🙂🙂☺️☺️😊😊
 
Hapo wangepaswa wasimame wazee/wababa na wamama kwanza maana ndo mizizi ya unafiki na woga ilipoanzia ndipo vijana wafuate nje na hapo vijana wataishia kuumizwa tuu na kuonekana kama wahuni fulani.
 
Demokrasia inayoimbwa hata nchini ipo tu kwenye majukwaa ya siasa lakini kimsingi hatuna demokrasia......

Maandamano ni haki ya kikatiba ya wananchi kuelezea hisia juu ya mambo yanavyokwenda nchini mwao.....leo hii haki hiyo inaharamishwa na watawala kwa kuwa tu wanaoandamana wanakuja na hoja zinazo wakaraisha...........

Tumeshuhudia maandamano mengi ya kusifia na kupamba.....lakini leo hii hao hao walioruhusu maandamano ya kusifu na kuabudu ndio wanaopinga ya kukosoa............hii inaendeshwa kwa utashi wa watu wachache wanaojiona wao ndio wana hatimiliki na nchi hii badala ya katiba mama..............
 
Hao watu wameonesha njia,,

Nilifikiri tutajitoa wote kwenda kuonesha njia na kumfanya saa100 alale na viatu kumbe walaa
 
Back
Top Bottom