Waliopigania uhuru wa Tanganyika Walipigana na nani?

Wapigania Uhuru wa nchi yetu walianza harakati za kupigania Uhuru wa nchi yetu mara tu baada ya uvamizi wa kikoloni barani Afrika

Baadhi ya wapigania Uhuru kabla ya vita ya pili ya dunia ni kama Kijenkitile Ngwale,Mkwawa,Mtemi Isike,Abushiri na wengineo

Baada ya vita ya pili ya dunia wapigania Uhuru wengine walijitokeza akina Nyerere ambaye alihamasisha watanganyika kuungana na kudai uhuru wa kweli ili waafrika tujitawale moja kwa moja na kujitegemea

Nyerere alipigania uhuru wa Tanganyika kwa kuwaunganisha watanganyika kuwa kitu kimoja na kupinga janja janja za wakoloni kutaka kukabidhi Uhuru kwa vibaraka wao akina Zuberi Mtemvu

Kupigania siyo lazima uchukue mtutu,hata kwa kelele au hamasa ni kupigania Uhuru pia na shukuru vita ya kwanza ya dunia ikawepo sidhani kama mjerumani angekabidhi Uhuru kwa amani
 
nakuona unavyopambana kuelewa.....

Jana yanga walipigana kiume sana aisee....
 

Jeshi letu limebakia kwenda Zanzibar kutishia raia kipindi Cha uchaguzi mkuu basi. Hawana la maana.
 
Kuna kitu kinaitwa maana kutokana na muktadha (contextual meaning) Kuna watu wanapigania uhai wodini, Kuna watu wanapigania ndoa zao Kuna watu wanapigania mapenzi na wengine Wana pigania familia zao na wewe upo hapa unapigania ujinga
 
Kuna kitu kinaitwa maana kutokana na muktadha (contextual meaning) Kuna watu wanapigania uhai wodini, Kuna watu wanapigania ndoa zao Kuna watu wanapigania mapenzi na wengine Wana pigania familia zao na wewe upo hapa unapigania ujinga

Vijana wa siku hizi usipoteze muda wako kuwaelezea jambo.

Huko shuleni walisoma Vita Baridi na hapakuwa na mapigano ya silaha. Wao wanachojua kupigana lazima ngumi, silaha na damu zihusike
 
Imagine miaka 60 sasa tuna taifa la majoga ....hakuna elimu wala kujitambua...hatuwezi kusimamia haki yetu kama Taifa....sembuse miaka hiyo.....walijitahidi sana wale wazee sasa tuna key boardworriors
Kabisa mkuu, alafu kuna jamaa anawadharau hapa.
 
Mi mwenyewe hii kitu hua siielewi ni bora hata zanzibar walitegea mwarabu amefunga ana swaum kali akakianzisha wakafanya mapinduzi sasa sisi hamna hata mzungu mmoja alipigwa hata ngumi moja ya pua atleast tuone damu eti tunajisifu tulipigania uhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…