Nyamesocho
JF-Expert Member
- May 5, 2023
- 487
- 1,287
Wapigania Uhuru wa nchi yetu walianza harakati za kupigania Uhuru wa nchi yetu mara tu baada ya uvamizi wa kikoloni barani AfrikaHi Great thinkers.
Nafikiri kuna jambo haliko sawa hasa tunaposema tulipigania uhuru. Tulipigana na nani.?
Mi navojua ule ulikuwa ni mchakato wa kupata uhuru wa Tanganyika, Na hakuna mtu aliyegoma kutupatia uhuru eti hadi tuanze kupigania.
Ni bora isemwe tu kwamba walioongoza harakati za kupata uhuru wa Tanganyika na siyo kupigana .
Labda kama ni sielewo kiwahili vizuri kati ya harakati/Kupigana.
Baadhi ya wapigania Uhuru kabla ya vita ya pili ya dunia ni kama Kijenkitile Ngwale,Mkwawa,Mtemi Isike,Abushiri na wengineo
Baada ya vita ya pili ya dunia wapigania Uhuru wengine walijitokeza akina Nyerere ambaye alihamasisha watanganyika kuungana na kudai uhuru wa kweli ili waafrika tujitawale moja kwa moja na kujitegemea
Nyerere alipigania uhuru wa Tanganyika kwa kuwaunganisha watanganyika kuwa kitu kimoja na kupinga janja janja za wakoloni kutaka kukabidhi Uhuru kwa vibaraka wao akina Zuberi Mtemvu
Kupigania siyo lazima uchukue mtutu,hata kwa kelele au hamasa ni kupigania Uhuru pia na shukuru vita ya kwanza ya dunia ikawepo sidhani kama mjerumani angekabidhi Uhuru kwa amani