Walioruhusu picha hii itumike hawakuwa wajinga

Yesu hakuwa na nywele ndefu kwa mujibu wa maandiko ilikuwa haifai kwa waebrania wa kiume kuwa na nywele ndefu.
1 WAKORINTHO 11

3 Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.

4 Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.

5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.

6 Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.

7 Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.

8 Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.

9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.

10 Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.

11 Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana.

12 Maana kama mwanamke alitoka katika mwanamume, vile vile mwanamume naye huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu. Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu.

13 Je! Inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunikwa kichwa?

14 Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?

15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi.

16 Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.
 
Wasabato mnaupinga utatu mtakatifu, mnapinga fumbo la imani. Kristo alikufa,Akafufuka na atarudi tena. Nyie ndio wapinga kristo
Hao ndio wafuasi sahihi wa Yesu, maana huo ndio ukweli.
 
Wasabato mnaupinga utatu mtakatifu, mnapinga fumbo la imani. Kristo alikufa,Akafufuka na atarudi tena. Nyie ndio wapinga kristo
Wakuu mi huwa sielewi hebu nifafanulieni kidogo hapa.........

Hivi YESU akirudi mara ya pili ndo siku ya kiama au?
 
Sipo kubishana nawe.

Mungu akikuhurumia atasema nawe utapolala, akili na mwili vitakapotulia.
 
Wasabato mnaupinga utatu mtakatifu, mnapinga fumbo la imani. Kristo alikufa,Akafufuka na atarudi tena. Nyie ndio wapinga kristo
Hakuna kitu inaitwa TRINITY.

Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Amen
 
Wasabato mnaupinga utatu mtakatifu, mnapinga fumbo la imani. Kristo alikufa,Akafufuka na atarudi tena. Nyie ndio wapinga kristo
Mpinga Kristo ni yule anaesapoti ushoga,hana andiko lolote kiimani linalosapoti ushoga
 
Trinity ipo kibiblia ndugu
Najua imeandikwa wapo watatu washuhudiao duniani MAJI, DAMU na ROHO,

Na wapo washuhudiao Mbinguni,

BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.

Tumia akili, mbegu ya Mwanaume ikiingia kutunga mimba Ina DAMU, MAJI na ROHO itokayo Kwa Mungu ndo inakamilisha MTU.

BABA,NENO na ROHO MTAKATIFU huwezi kuwatofautisha kama ambayo huwezi tenganisha DAMU na MAJI na ROHO ktk mwili wa mwanadamu akaendelea kuishi.

Utatu ni Freemasonry, pembe 3 za shetani, au Bikari ni Miungu.

Stukeni mmeaminishwa msichokijua.

Mungu ni title kama ukisema URAIS na ni title au Jina la office kimfumo.

Bt Jina la mwenye office lilifichwa Hadi lilipokuja kufunuliwa.

YESU ndilo JINA la Mungu.

Shetani analijua Hilo, Huwa YESU akipita hapo angani, shetani hutoka mbio zaidi ya mshale.
 
Rais akirudi nyumbani kwake kwa watoto wake wanamtambua kama raisi au baba.
Mnachanganya mambo Mungu sio watatu Mungu ni mmoja nafsi tatu ni kani ya utendaji.

Chukua uelewa huu John ni Mwalimu ,ni mkulima na ni mfanyabiashara hii hakumaanishi John wapo watatu bali ni yule yule mmoja mwenye uwezo wa kujigawa KWA Kazi hizi tatu
 
Kuna tofauti gani kati ya Roho mtakatifu na Kristo/Mungu mwana??
Swali zuri.

Hakuna tofauti kati ya Mungu BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.

Yesu aliingia tumboni mwa bikra Kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU.

Hapo hapo, Yesu anapaa na kusema nitamtuma Roho wangu, ROHO MTAKATIFU na atawafundisha yote, atanishihudia mm.

Wengi wamefunuliwa walipoenda MBINGUNI, ukifika Mbinguni Leo hii, hutomuona kwamba Yesu ni huyu, Baba ni huyu na Roho MTAKATIFU ni huyu,

Ukibahatika kwenda Mbinguni ktk ROHO, utamwona YESU ndiye amekaa ktk KITI Cha ENZI na ndiye anayeabudiwa Mbinguni.

Siri hiyo ni kubwa, shetani amewapofusha WANADAMU wasilijue Hilo, bt shetani anamjua Yesu ni nani.

Amen
 
Tupo pamoja.

Mungu ni MMOJA,

Akija duniani Kuokoa Anaitwa mwana.

Akitaka kuingia ndani ya watu wote ULIMWENGUNI Kwa wakati mmoja Anaitwa Roho wa YESU au ROHO MTAKATIFU.

Akitaka kukalia KITI kufanya HUKUMU anakaa kitini na kuitwa Baba.

Sura ya Mungu ilifichwa na Jina lake lilifichwa miaka na miaka Hadi pate Malaika aliposema aitwe YESU.

Sura ya YESU ndiyo sura ya Mungu inayotazamika ktk KITI Cha enzi Hadi sasa bt Kwa Utukufu mwingi'' sana.

Yesu ndilo JINA la Mungu.

Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.

Amen
 
YESU Kwa ajili ya watu wote waaminio ktk uwepo wa Mungu, ndomana hata ktk kitabu Cha Islam pamoja na kuwa kimefitinishwa na bible kinamtambua YESU ndiye AJAYE kuuhukumu Ulimwengu.

Kaa ktk uislamu wako ila Mwamini YESU,

Ndiye njia pekee ya kukuunganisha na Mungu na kusamehewa DHAMBI.

Hakuna njia nyinfine yeyote,

Yesu Si mtume, Yesu ni Mungu.

Amen
 
Oya huyo jamaa kwa Avatar yako anaitwa Nani??? Naona demu wa msela wangu huwa ana mpost kinoma
 
Ndugu yangu are you serious unappsema Yesu hakuwa maarufu kipindi chake umesoma hata kitabu kimoja cha injili. Wafalme wa kipindi chake walikuwa wanahangaika jinsi jina la Yesu lilivyokuwa linavuma kuliko hata Yao unasema hakuwa maarufu??

Try to be serious hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…