Walioruhusu picha hii itumike hawakuwa wajinga

Walioruhusu picha hii itumike hawakuwa wajinga

Kasome hapa
Mathayo 26:
48 Yuda aliyekuwa amkabidhi Yesu kwao, alipanga kufanya kitu cha kuwajulisha yupi kati ya wafuasi alikuwa Yesu. Alisema, “Mtu nitakayembusu ndiye mtakayemkamata.” 49 Hivyo Yuda alikwenda kwa Yesu na kumwambia, “Salamu, Mwalimu!” Kisha akambusu.

Kama Yesu angekuwa maarufu na anayejulikana Yuda asingewaambia hao maaskari maneno hayo.

Kama Yesu angekuwa mashuhuri na maarufu wala asingewapa Wanafunzi wake Misheni ya kumtangaza yeye na habari zake.

Vinginevyo haujui maana ya MTU maarufu na mashuhuri
Fact tupu,
Watu wapunguze mahaba
Yesu hakua maarufu bhana
Hata hukumu yake ilkua ya kawaida Kama wahalifu wengine wasumbufu wa serikali ya kiyahudi[emoji4]
 
KiswahiliEdit. NominoEdit. maarufu. ni kujulikana hasa katika sanaa au kisiasa; umaarufu pia kuwa unajulikana kitaifa na hata kimataifa.

Huyo Yesu hata Askari wenyewe walikuwa hawamjui.
Rejea Yuda akiwaambia hao maaskari.

MTU maarufu au mashuhuri Kwa mfano kama Mwamposa, Askari au Watu wa kawaida wa Hapa Dar es karibu wote wanamjua.

Yesu alikuwa mgeni katika jiji la Jerusalem
Sahii KABISA mkuu,
Umenikosha unavojibu kwa facts[emoji4]
Watu waache kulazimisha mambo[emoji106]
 
Ndio maana tukapishana,

Maarufu na mashuhuri ni MTU anayefahamika/julikana iwe kitaifa au kimataifa.

Sasa Yesu bado hakuwa katika hiyo stage katika Wakati wake.

Umaarufu wa Yesu umeanza Baada ya Dola la Rumi kuichukua dini ya Ukristo kama dini ya kirumi, kisha kuisambaza Kwa UPANGA,
Kisha wakaja Wazungu.
Vinginevyo huyo Yesu wala usingemjua hata Wewe Kwa sababu kimsingi Hana maajabu bila ya Promo
Ha ha ha ....
umepiga Kwny mshono
Walokole hawatakagi KABISA [emoji4]
 
Kwa maarifa na taarifa wanazomiliki Kanisa katoliki pale Vatican city Kwa mantiki ya maelezo yako basi hata picha au taswira ya Mtume Muhamad(Saw) Kwa wenzetu ndugu zetu sana Waislamu,wakatoliki wanayo.
sasa kama padri wa katoliki ndo mtu wa kwanza kumuandikia mtume aya za qurani hilo linashindikana vipi?
 
I hope y'all are doing just fine, It has been long time since I was here[JF Inteligence]
View attachment 2545863
Kuna mtu alileta mada humu akiuliza kwamba picha inayotumiwa na wakristo hasa wakatoliki ya mtu mmoja mzungu kua “ndie” yesu, je hiyo picha ni ya Yesu kweli? Akaongeza kwa kusema kwamba wakati yesu akiwepo kulikua hakuna teknolojia ya Photography wala Motion Picture…So wao waliitoa wapi picha hiyo na wana ushashidi upi kwamba yule ndio Yesu mwenyewe??

I’m glad you asked coz I would like to use this moment to Splendid Explain these stuffs to you!

Toka dunia kuumbwa, dunia imeshuhudia kuzaliwa kwa watu wawili wenye akili zaidi.watu hao walikua wenye uwezo wa kujifunza mambo wao wenyewe yaani Autodidacts na walikua wana uelewa na uwezo wa kufanya mambo meengi kwa wakati mmoja yaani Polymaths…watu hao si wengine bali ni Imhotep kutoka Misri ya zamani (Ancient Egypt) na Leonardo Da’Vinci kutoka Sicily Rome.

Imhotep alikuwepo duniani Zaidi ya miaka 5000 kabla ya kuzaliwa kwa Da’Vinci, Da’Vinci kazaliwa miaka 600 iliyopita yaani 1400s.Imhotep alikua kuhani mkuu wa mungu mkuu wa wamisri aitwaye mungu jua Ra, mbali na hayo jamaa alikua mbobevu katika hesabu,fizikia na biology hivyo alijikita sana katika usanifu wa majengo na tiba mbalimbali. Ukiziona Pyramids zilizopo misri wala usidanganyike kua alien ndio wamejenga bali ni huyu Inhotep ndio alizisanifu.

Wagiriki walimuabudu huyu mtu kama mungu wao wa tiba kutokana na mchango wake mkubwa katika tafiti zake zi kitabibu.

Kwa waliosoma mada zangu kadhaa zilizopita nilielezea jinsi utawala wa Ugiriki ulivyotokea na kuanguka na matokeo yaliyotokea baada ya ugiriki kuanguka. Kwa ambao hawajasoma nitaelezea kwa ufupi sana nini kilitokea.
Miaka ya nyuma ugiriki ya zamani ilikua imeundwa na miji ipatayo 100 na kila mji na ulikua na utawala wake japo walikua wakiungana na kusaidiana pindi uvamizi unapotokea, enzi hizo superpower wa dunia alikua Persia yaani Iran ya sasa. Iran ilikua inajitanua kwa kuvamia maeneo na kuyachukua hapo ndio alipoikaribia Ugiriki akitaka aanze kuchukua mji baaada ya mji, hapo ndio unakutana kisa cha mfalme Leonidas wa jiji la Sparta.

Vumbi ilitimka kweli kwa wapenzi wa muvi waliotazama muvi ya 300 na 300 Rise of Empire wanaelewa.
Baada ya vamizi kadhaa zilizokua zinafanywa na nchi kubwakubwa wagiriki wakaamua kuungana na kutengeneza nchi moja ya Greece. Mikaka ikaenda akatokea alexander the great akaikuza sana Greek, akaanzisha mji wake ulioitwa Alexandria katika nchi ya Misri. Kipindi hicho misri ilikua ndio hazina na kitovu cha Elimu dunia nzima.
View attachment 2545869
[Mwigizaji Gerald Butler aliyeigiza kama mfalam Leonidas wa sparta kutoka muvi ya ]

Wanafalsafa wengi na walienda hapo kusomea, hata mwandishi wa injili Luka alisomea hapo. Miaka ikaenda baada ya Ugiriki kuanguka Superpower aliyeibuka akawa Rome, Rome ilienda kuchukua kila kitu kilichokua misri wakakihamishia kwao. Maarifa yote yaliyokua Misri kwenye Maktaba ya kwanza kuanzishwa duniani yalihamishiwa Rumi.

Wakati nchi ya Israel ikitawaliwa na Rumi anazaliwa Yesu anafanya kilichomleta duniani kisha anafariki miaka 33 baadae, wafuasi wa Yesu wanaongenzeka na kupata ushawishi mkubwa katika serikali na maeneo mengi duniani.

Kwa wanaopenda Conspiracy, inasemaekana baada ya utawala wa Rumi duniani kuanza kuanguka watu wenye kufikiria mbali (futurist) wakiongozwa na mfalme Nero walikabidhi madaraka kwa wafuasi wa Yesu Kristo wa kipindi hicho ili Rumi iendelee kutawala dunia kupitia mlango wa nyuma (indirectly) ndipo ukristo ukatambuliko rasmi duniani kama Roman Catholic na wakapafanya Rumi kama ndio makao makuu ya Ukristo badala ya Yesrusalemu. (Sina uhakika kama nadharia hii ina ukweli ndani yake ila ina make sense sana maana wote twafahamu nguvu na ushawishi iliyonayo RC katika mataifa mbalimbali)

Miaka kadhaa tawala ya Rumi inaanguka, Ukatoliki ukawa umeenea maeneo mengi na ushawishi mkubwa ulimwenguni anazaliwa Leonardo Da’Vinci 1452, kutokana na uwezo mkubwa katika mambo mbalimbali kila alichokifanya kiliweza kua Perfecto. Davinci aliweza kuifanya tasnia ya uchoraji kua kubwa na yenye thamani sana kutokana na kazi zake bora na zenye kufikirisha za uchoraji.

Ni moja kat ya wachoraji wakubwa kuwahi ktokea hapa duniani kuna vitu kachora hakuna mwingine anayeweza kuchora labda urumie Powerful software…kama utanibishia jaribu kuchora duara na pembe nne vikiwa pamoja kama alivyochora mchoro wake wa Vitruvian man… Jamaa alikua anaweza kujichora yeye mwenyewe sura yake…Baadae anazaliwa Michelangelo ambae na kwa kiasi Fulani alijitahidi sana katika uchoroja unaweza kujionea michoro yake ya Sistine Chapel iliyopo hapo Vatican, lakini pia nae alibobea katika uchonganji (sculptures)
View attachment 2545902
[Sistine Chapel]
Inahusiana vipi na Picha ya Yesu…?

Kama nilivyoeleza huko juu Baada ya Ugiriki na Misri kuanguka na Rumi kuibuka kama Superpower alibeba maarifa yote yaliyokua Rumi na Ugiriki na kuyahamishia Roma, hivyo baada ya rumi kuanguka kanisa katoliki likabaki limeshikilia maarifa kutoka pande zote za dunia hasa misri,ugiriki na Israel. Leo hii hakuna taarifa au maarifa ambayo hayapo Vatican…Vatican inamiliki moja kati ya eneo lenye kulindwa Zaidi duniani ambalo hua haiingii huko mtu bila ruhusu maalumu…Hata Pope inabidi apate kibali kutoka kwa kiongozi wa Jesuists ndio anaweza kwenda huko.

Hivyo basi sidhani kwamba kanisa katopliki wanaweza kua wameshindwa kupata piacha ya yesu wakati wameweza kumiliki taaroifa za kutoka kila pande ya dunia. Kama Plato,Socrate, nk picha zao zipo na waliishi miaka mingikabla ya yesu haiwezekani yeye picha yake isiweze kupatikana.

Nimesema kipindi hicho taaluma ya uchoraji na uchongaji ilitumika Zaidi katika kuweka kumbukumbu za watu mbalimbali ndio maana leo ukiitaka picha ya Plato unaipata, kuna watu wamejaliwa uwezo mkubwa wa uchoraji unaweza kumuelezea kwamba Fulani sura yake ipo hivi na hivi na akaichora kama ilivyo. Njia hii hutumiwa sana na mashirika ya usalama hususan FBI na polisi. Tena sasa hivi kuna msaada wa softwares yaani ukimuelezea mtu anakutulea mchoro kama picha halisi…hivyo basi natumaini hata picha ya yesu watu wa zamani walitumia njia hiyo kuhifadhi taswira ya Kristo.

Ndio maana utakuta picha hiyo inayotumika sura yake ipo mahali pote sio tofauti. Hata miaka ya 1970s wakati wanaandaa filamu ya yesu walijaribu watu Zaidi ya waigizaji 200 ambao watafanana na Sura hiyohiyo ni Brian Deacon pekee ndio alifanikiwa kufit kwenye role hiyo kutokana na sura yake kufanana na sura inayotumika kuwasilisha taswira ya Kristo.
Ndio maana wasiojua wanapoona hiyo taswira ya yesu hua wanasema kwamba ni sura ya mwigizaji Brian Deacon…Si kweli, kwa maarifa waliyonayo RC hawawezi ruhusu hilo.

So kwa kuhitimisha ni kwamba Wakatoliki kukubali kuruhusu picha hiyo ya Yesu kutumika sio wajinga hata kidogo kwamba hawafahamu taswira halisi ya Kristo.
leso/kitambaa alichomfutia yesu usoni wakati yupo msalabani kilibaki na taswira ya yesu,na kitambaa hicho kipo vatican.
 
KiswahiliEdit. NominoEdit. maarufu. ni kujulikana hasa katika sanaa au kisiasa; umaarufu pia kuwa unajulikana kitaifa na hata kimataifa.

Huyo Yesu hata Askari wenyewe walikuwa hawamjui.
Rejea Yuda akiwaambia hao maaskari.

MTU maarufu au mashuhuri Kwa mfano kama Mwamposa, Askari au Watu wa kawaida wa Hapa Dar es karibu wote wanamjua.

Yesu alikuwa mgeni katika jiji la Jerusalem
Binafsi nalisikia jina la mwamposa kwa Sura simjui. Je mwamposa sio maarufu?

Kwa zamani ili umfahamu mtu njia pekee ni kumuona kwa kutumia macho yako.
Mtu mwenye uwezo wa kukusanya watu zaidi ya 10k ( wanaume 5k walikula mkate na samaki) kwa pamoja sio maarufu huyo?
Haijalishi alikuwa maarufu kwa watu wa aina gani ( masikini kwa wingi) ila alikuwa maarufu.
 
Hakuwa maarufu Kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Zingatia huyo Yesu Route yake ilianzia wapi na kuishi wapi.
Zingatia pia hakuwa mwenyeji wa Jerusalem, ndio alikuwa amefika, hakuwa na muda mrefu wa kufahamika.
 
Mtu asiye maarufu Ngazi za kitaifa habari zake zinafikaje kwa wakuu wa Nchi?
Herode alimjua Yesu ( au alisikia habari za yesu) kabla ya Yesu kupelekwa kwake?
Mtu ambaye habari zake zimefika mpaka Chemba za watawala unasemaje sio maarufu?
 
Nashindwa kuelewa mnapo sema Yesu hakuwa maarufu. Vitu vipo very clear, inahitaji very simple logic kulink the dot na kupata a clear picture ya umaarufu wake.

Advancement of Technology
Lazima muelewe kwamba tunaongelea miaka 2000 A.D iliyopita ambapo maendeleo ya teknolojia yalikuwa madogo lakini bado still haikuzuia umaarufu wake. Leo hii katika karne ya 21th century tunaona mapinduzi makubwa ya sayansi na teknolojia, dunia ipo kiganjani. Jambo linasambaa duniani kote with in a minute or with in a single digit, maajabu ya World Wide Web inavyofanya kazi yake.

1. Kwa mantiki iyo kwa nini Mwamposa asijulikane mpaka uso wake?
2. Kwa mantiki iyo kwa nini Kuhani Mussa asijulikane mpaka na kanisa lake?

Huku vitu kama radio now days unaweza ukatune online listening or offline listening kwa nini asijulikane mpaka na vocal sound yake?

Leo hii tukimfufua mtu aliyeishi miaka 2000 A.D iliyopita akakukuta unawasiliana na simu, wewe upo Mwanza muda huo huo unawasiliana na mtu yupo Mbeya immediately wewe ungeitwa mchawi namba moja. Lakini this day's ni jambo la kawaida mtu yupo Bongo anawasiliana na mtu yupo Nevada - Marekani through telecommunications hakuna anayeshangaa wala kushtuka.
That is power of Technology my dear.

Imagination is more powerful than knowledge.
Imagine, miracles za Yesu zingefanyika katika karne hii, unafikiri neno famous lingeweza kumfit kwa maana angekuwa "more than famous" that's it!

Let's move our attention katika Injili Takatifu.
Marko 3:7-12
Umati Wa Watu Wamfuata Yesu

"7 Yesu pamoja na wanafunzi wake waliondoka mahali hapo wakaenda ziwani wakifuatwa na umati mkubwa wa watu kutoka Galilaya na Yudea. 8 Na watu kutoka Yerusalemu, Idumaya, na eneo lote la ng’ambo ya Yordani, sehemu za Tiro na Sidoni, waliposikia mambo aliyokuwa akitenda, wakamwendea. 9 Akawaomba wanafunzi wake wamwandalie mashua ili asisongwe na kubanwa sana na watu. 10 Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wote wenye maradhi walikuwa wakisukumana wapate kumgusa. 11 Na kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kulia kwa sauti kuu, “Wewe ni Mwana wa Mungu.”12 Lakini aliwaamuru wasimtambulishe kwa watu."

Ukisoma Injili Takatifu unaona kabisa umati mkubwa wa watu ulimfwata kutoka miji mikubwa ya Galilaya, Yudea, Yerusalemu, Idumaya, pamoja na Yordani.
Hauwezi kusema Yesu hakuwa maarufu?

Pia ukisoma Marko 3: 9 anawaomba wanafunzi wake wamwandalie mashua hili asisongwe na kubanwa sana na watu. Hii inakuonyesha jinsi gani umati ulivyokuwa mkubwa mpaka anatafuta alternative space kwa ajili ya kuzungumza nao na kuwa ponya matatizo yao.

Lakini ukisoma Marko 3:12 Yesu aliwapa maagizo wanafunzi wake wasimtambulishe kwa mtu yeyote. Hii inakuonyesha hakuja dunia kusaka Fame, kuwa Celebrity au A Top Richest man in the world. Alisimamia katika mission yake ya "kuokomboa ulimwengu" na hakutaka show-off za Dunia hii, tofauti na wafalme au watu mashuhuri wa zama hizo walilewa sifa za fame, starehe na show-off za kila namna.

Umaarufu wa mtu sio lazima mpaka uwe, ama kuwepo na picha zake.
Mtu akisema Buddha - unajua alikuwa spiritual teacher wa South Asia na founder wa Buddhism.
Mtu akisema Lao Tzu - unajua alikuwa Chinese philosopher na founding figure wa Taoism in China.
Mtu akisema Griselda Blanco Restrepo - unajua Cocaine God mother wa Colombia.

Watu wazamani walisifika kwa matendo yao kuliko muonekano wao. Now days watu wanatumia sana muonekano wao kuliko matendo yao kuwa fame & celebrity.

I'm done
🙌

Robert Heriel DeepPond Da'Vinci
 
Picha za Yesu zinamuonesha yupo smart kama watawala wa enzi hizo ilihali alidharaulika sana hadi wakasema ''ni huyu mtoto wa seremala'' ina maana alikuwa common man tu. Sasa kwanini wachore picha anafanana na tabaka la watawala?, au ni ili kuleta picha ya ufalme wa Mungu? Basa kama ndio hivyo picha haina uhalisia.

kuna watawala hata viongozi wa kanisa katoliki (mapapa na makadinali) picha zao za mionekano halisi hazipo sasa inakuwaje iwepo ya mwananchi wa kawaida tu au ya Yesu wanayemuhubiri. Hii haijakaa sawa sababu wao tunategemea wangekuwepo picha zao kamili kabisa.

Anyway bado sijashawishika kabisa juu ya hii picha. Kuna movie moja ya Yesu inamuonesha akiwa tofauti sana na huyu, yupo angalau kama raia wa kawaida.

Kuna habari kuwa picha za Mtume Mohammed hazipo kabisa na za kubuni hawa ndugu zetu hawazitaki, kitu ambacho ni kizuri.

Picha ya Yesu ni kama zilivyo picha za wakina Moses, Abraham, Yusufu, Joshua n.k ni picha zakubuni tu.
Sasa Ni Wapi Palipoandikwa Hizo Ni Picha Halisi?!!
 
Nashindwa kuelewa mnapo sema Yesu hakuwa maarufu. Vitu vipo very clear, inahitaji very simple logic kulink the dot na kupata a clear picture ya umaarufu wake.

Advancement of Technology
Lazima muelewe kwamba tunaongelea miaka 2000 A.D iliyopita ambapo maendeleo ya teknolojia yalikuwa madogo lakini bado still haikuzuia umaarufu wake. Leo hii katika karne ya 21th century tunaona mapinduzi makubwa ya sayansi na teknolojia, dunia ipo kiganjani. Jambo linasambaa duniani kote with in a minute or with in a single digit, maajabu ya World Wide Web inavyofanya kazi yake.

1. Kwa mantiki iyo kwa nini Mwamposa asijulikane mpaka uso wake?
2. Kwa mantiki iyo kwa nini Kuhani Mussa asijulikane mpaka na kanisa lake?

Huku vitu kama radio now days unaweza ukatune online listening or offline listening kwa nini asijulikane mpaka na vocal sound yake?

Leo hii tukimfufua mtu aliyeishi miaka 2000 A.D iliyopita akakukuta unawasiliana na simu, wewe upo Mwanza muda huo huo unawasiliana na mtu yupo Mbeya immediately wewe ungeitwa mchawi namba moja. Lakini this day's ni jambo la kawaida mtu yupo Bongo anawasiliana na mtu yupo Nevada - Marekani through telecommunications hakuna anayeshangaa wala kushtuka.
That is power of Technology my dear.

Imagination is more powerful than knowledge.
Imagine, miracles za Yesu zingefanyika katika karne hii, unafikiri neno famous lingeweza kumfit kwa maana angekuwa "more than famous" that's it!

Let's move our attention katika Injili Takatifu.
Marko 3:7-12
Umati Wa Watu Wamfuata Yesu

7 Yesu pamoja na wanafunzi wake waliondoka mahali hapo wakaenda ziwani wakifuatwa na umati mkubwa wa watu kutoka Galilaya na Yudea. 8 Na watu kutoka Yerusalemu, Idumaya, na eneo lote la ng’ambo ya Yordani, sehemu za Tiro na Sidoni, waliposikia mambo aliyokuwa akitenda, wakamwendea. 9 Akawaomba wanafunzi wake wamwandalie mashua ili asisongwe na kubanwa sana na watu. 10 Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wote wenye maradhi walikuwa wakisukumana wapate kumgusa. 11 Na kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kulia kwa sauti kuu, “Wewe ni Mwana wa Mungu.”12 Lakini aliwaamuru wasimtambulishe kwa watu.

Ukisoma Injili Takatifu unaona kabisa umati mkubwa wa watu ulimfwata kutoka miji mikubwa ya Galilaya, Yudea, Yerusalemu, Idumaya, pamoja na Yordani.
Hauwezi kusema Yesu hakuwa maarufu?

Pia ukisoma Marko 3: 9 anawaomba wanafunzi wake wamwandalie mashua hili asisongwe na kubanwa sana watu. Hii inakuonyesha jinsi gani umati ulivyokuwa mkubwa mpaka anatafuta alternative space kwa ajili ya kuzungumza nao na kuwa ponya matatizo yao.

Lakini ukisoma Marko 3:12 Yesu aliwapa maagizo wanafunzi wake wasimtambulishe kwa mtu yeyote. Hii inakuonyesha hakuja dunia kusaka Fame, kuwa Celebrity au A Top Richest man in the world. Alisimamia katika mission yake ya "kuokomboa ulimwengu" na hakutaka show-off za Dunia hii, tofauti na wafalme au watu mashuhuri wa zama hizo walilewa sifa za fame, starehe na show-off za kila namna.

Umaarufu wa mtu sio lazima mpaka uwe, ama kuwepo na picha zake.
Mtu akisema Buddha - unajua alikuwa spiritual teacher wa South Asia na founder wa Buddhism.
Mtu akisema Lao Tzu - unajua alikuwa Chinese philosopher na founding figure wa Taoism in China.
Mtu akisema Griselda Blanco Restrepo - unajua Cocaine God mother wa Colombia.

Watu wazamani walisifika kwa matendo yao kuliko muonekano wao. Now days watu wanatumia sana muonekano wao kuliko matendo yao kuwa fame & celebrity.

I'm done
🙌

Robert Heriel DeepPond Da'Vinci

Nafikiri haujui maana ya neno maarufu au mashuhuri.

Yaani hata Yohana Mbatizaji Kwa Kipindi kile alikuwa anamzidi Yesu Kwa umaarufu tena Kwa mbali Mno.

Yesu amedumu kwenye kazi Kwa miaka 6 tuu,
Ndio alikuwa anaanza Kupata umaarufu, ni kama vile kina Costa Tich huyu mwanamuziki aliyekufa juzi jukwaani.
 
I'm done🙌
 
Back
Top Bottom