Uchaguzi 2020 Walioshinda kura za maoni na kukatwa, msikubali ujinga huu

Uchaguzi 2020 Walioshinda kura za maoni na kukatwa, msikubali ujinga huu

WAJUMBE tupo pamoja sana. Ninyi ndiyo mnaowajua fika WATIA NIA na mnaishi nao mtaani. Siyo NEC. Kutoheshimu uamuzi wenu ni kosa kubwa sana na dharau iliyokithiri. Sasa mna kura moja ya turufu. Ni kutowapigia kura ya NDIYO Oktoba 28.
Hilo titalifanya, sasa tunawataka wale walioshinda kura za maoni wasisubirie hisani, waingie kwenye uchaguzi kwa kuamini watachaguliwa na waliowapa ushindi jimboni.

Huko ccm hawatakiwi, sasa waende nje ya ccm wapiga kura ni walewale wananchi.
 
Ulikuwa mshindi halali kura za maoni, lakini Watawala wajuu wakakukata jina lako na kumuweka mtu wanayemtaka.

Kisha mliokatwa mkaambiwa muwapigie kampeni hawa mahasimu wenu, kwa ahadi kwamba mmeshafanyiwa vetting mtateuliwa kwenye nafasi zingine...
Tumieni akili zenu. Akili za kuambiwa ongeza na zako
 
Hahaha kama alishinda "kula" huyo anaweza kuwa alikuwa anashindania vitu tofauti na mjadala huu.

Tunaongelea walio porwa ushindi kura za maoni.
🤸🤸🤸🤸Shushu limeenda shule ..hapa mada ni Kura...sio kula🤣🤣🤣🤣 Viva Lissu
 
Ha haa! Wacha tuendelee kucheza mdumange wa CCM... Watu tulisha shona suti za kijani sasa tutaenda nazo wapi.. Ngoja tuendelee ku socialize huku huku CCM tukisubiri miezi 62 ipite!
Suti za kijani unaweza kuwapa TOT ukabadiri maisha kwa kuvaa kombati.
 
Tumieni akili zenu. Akili za kuambiwa ongeza na zako
Hahaha wamedumazwa akili zao kwa chanjo ya ujinga.

Tunawasaidia antidote watoke huko, waone kwa macho yao, na wafikirie kwa akili zao.

Kuendelea kubaki ccm ni kudhihirisha kwamba wamefungiwa kwenye box.

Yani uneshinda, halafu ukatwe, kisha aliyekukata akuahidi kukuteua halafu nawe unasubiria.

Aliyekukata anasema hufai kuwa mbunge,jiulize utafaa wapi?!

Akili ni nywele, ntaelewa kama una kipara.
 
Fanyeni maamuzi sasa, nendeni vyama vingine mkagombee kama mnaamini mlishinda na mtashinda nafasi za kuchaguliwa.
Halafu wakiunga mkono juhudi mtasema wamenunuliwa
Kwani upinzani hakuna watu mpaka mtegemee makapi ya ccm?
 
Sio wote waliokatwa walikuwa wabunge kabla.

Uongozi ni hiyari kwa wanaoongozwa, sio matakwa ya watawala kutuchagulia wampendaye.
Ni kweli sio wote ila saivi ubunge umekuwa lulu zaidi ya tanzanite
 
Kama walishinda huku chama tawala na wakakatwa watashindwa kukatwa wakishinda wakiwa upinzani
 
Waende tu upinzani. kwani kunajipya gani?

utaratibu wa kuunga mkono juhudi baada ya uchaguzi siunajulikana.
 
Ni kweli sio wote ila saivi ubunge umekuwa lulu zaidi ya tanzanite
Ndiyo kazi uhitaji kuandamana kulipwa mshahara, ndiyo kazi ukistaafu hufuatilii pesa ya kiinua mgongo.

Yani hakuna kutapeliwa na serikali, sijui vikokotoo wala sijui faili halijafika hazina, mara ohoo mwajiri hajaleta makato ya kila mwezi.

Na insurance ya matibabu ni insurance ya ukweli siyo hizi NHIF na nduguze.

Kila mwenye akili ana uhitaji ubunge tu.

Sasa iweje wananchi wakuchague halafu wao wakukate, halafu udanganywe utateuliwa nawe ukubali?!
 
Halafu wakiunga mkono juhudi mtasema wamenunuliwa
Kwani upinzani hakuna watu mpaka mtegemee makapi ya ccm?
Hahaha tunataka wananchi wapewe chaguo lao sio chama, kama kungekuwa na mgombea huru kuna haja gani ukajinyeenyee kwa kina Bashiru, Magufuli na Polepole?!
 
Hahaha tunataka wananchi wapewe chaguo lao sio chama, kama kungekuwa na mgombea huru kuna hsja gani ukajinyeenyee kwa kina Bashiru, Magufuli na Polepole?!
Kwani Ni lazima wawe wabunge?
Hamuwezi kwenda ikulu kwa kutegemea makapi ya ccm
 
Usiwavunje moyo chama cha mapinduzi na serikali yake kuna nafasi nyingi ya uongozi

Mna nini kichwani jamani?? Kama amekatwa kwa kuhonga - ana kosa la kushtakiwa. Hamtaki hata kumshitaki na mnataka astahili kuwa kiongozi - kitu mlichomnyima!

Au akiwa mtu wa rushwa ni mbaya kwa CCM lakini mzuri kwa umma??
 
Kwani Ni lazima wawe wabunge?
Hamuwezi kwenda ikulu kwa kutegemea makapi ya ccm
Hahaha hoja sio kwenda ikulu, wabunge mwisho wao ni bungeni Dodoma.

Kila mtu anafahamu ccm yote makapi, na hii sio hoja hapa.

Hoja ni ushauri kwa walioonewa kwa kuporwa ushindi waliopewa na wananchi na wanaahidiwa wangoje kuteuliwa.

Nimewashauri waondoke huko, kama kweli wanapendwa na wananchi hata wakigombea ubunge kwa ticketi ya TADEA au TPP wanaweza kushinda, hoja ni ku prove mapenzi waliyonayo wananchi kwa kuongozi wamtakaye.
 
Back
Top Bottom