Ulikuwa mshindi halali kura za maoni, lakini Watawala wajuu wakakukata jina lako na kumuweka mtu wanayemtaka.
Kisha mliokatwa mkaambiwa muwapigie kampeni hawa mahasimu wenu, kwa ahadi kwamba mmeshafanyiwa vetting mtateuliwa kwenye nafasi zingine.
Kataeni ujinga huo, yani aliyekukata usigombee, baadaye aje akuteue?
Inakuingieni akilini kweli, kwanini asinge mteua huyo aliyempenda na kumpa nafasi yako uliyopewa na wananchi?
Wanasema mlitoa rushwa, sasa kama hilo ni doa tayari huo uteuzi mtaupataje?
Fanyeni maamuzi sasa, nendeni vyama vingine mkagombee kama mnaamini mlishinda na mtashinda nafasi za kuchaguliwa.
Kumbukeni hizi za kuteuliwa ni kama mwanamke anyechumbiwa, hana uhakika wa kuolewa mpaka siku ya kufunga ndoa.
Na ndio maana huona wanawake hulia siku ya ndoa, hawaamini wamefikia hatua hiyo.
Jitoeni CCM nendeni Chadema au ACT, mkathibitishe hamjatoa rushwa, na mlionewa ili wananchi wachague, huko CCM hata mkibaki mneshatuhumiwa kwa rushwa, sasa mtateuliwa vipi?
Muda ndio huu msichelewe kwa ahadi hewa mtajuta.