Uchaguzi 2020 Walioshinda kura za maoni na kukatwa, msikubali ujinga huu

Nani hakutoa rushwa?! Rushwa zilizidiana kwa kila mgombea, wapo waliotia elfu kumi, wapo waliotoa laki, na wapo waliotoa laki tano.

Chama kina wenyewe, haikujali ulitoa hukutoa.

Sasa maajabu ya CCM inasema itawapangia kazi nyingine watoa rushwa,nchii hii Ni ya ajabu sijapata kuona
 
Ulikuwa mshindi halali kura za maoni, lakini Watawala wajuu wakakukata jina lako na kumuweka mtu wanayemtaka.

Kisha mliokatwa mkaambiwa muwapigie kampeni hawa mahasimu wenu, kwa ahadi kwamba mmeshafanyiwa vetting mtateuliwa kwenye nafasi zingine.

Kataeni ujinga huo, yani aliyekukata usigombee, baadaye aje akuteue?

Inakuingieni akilini kweli, kwanini asinge mteua huyo aliyempenda na kumpa nafasi yako uliyopewa na wananchi?

Wanasema mlitoa rushwa, sasa kama hilo ni doa tayari huo uteuzi mtaupataje?

Fanyeni maamuzi sasa, nendeni vyama vingine mkagombee kama mnaamini mlishinda na mtashinda nafasi za kuchaguliwa.

Kumbukeni hizi za kuteuliwa ni kama mwanamke anyechumbiwa, hana uhakika wa kuolewa mpaka siku ya kufunga ndoa.

Na ndio maana huona wanawake hulia siku ya ndoa, hawaamini wamefikia hatua hiyo.

Jitoeni CCM nendeni Chadema au ACT, au cha chochote mkathibitishe hamjatoa rushwa, na mlionewa ili wananchi wachague, huko CCM hata mkibaki mneshatuhumiwa kwa rushwa, sasa mtateuliwa vipi?

Muda ndio huu msichelewe kwa ahadi hewa mtajuta.
Huu ni UCHOCHEZI wa wazi kabisa! Mbona wale waliokatwa kutoka CHADEMA, ACT, CUF au vyama vingine HUJAWAPA UJUMBE HUU? Huu, nasema tena ni UCHOCHEZI wenye nia ya kuleta misigano ndani ya jamii kwa ujumla na ndani ya CCM kwa upekee. Au nikuulize, huko kwenye vyama vingine hakukuwa na waliokatwa yaani kila nafasi ilikuwa na mgombea mmoja mmoja? Hakukuwa na ushindani huko? Hebu tueleze nia na lengo a ujumbe huu?
 
Mimi Nina ushauri tofauti na WAKO, wasihame wabaki huko huko ccm ila wahujumu mikakati ya ccm
 
Unamaanisha Dada wa Segerea aliyekwata kapewa John Mrema au nabii Shila kule Kilombero ambapo CHADEMA walicheza sarakasi au?!
 
Huu ni UCHOCHEZI wa wazi kabisa! Mbona wale waliokatwa kutoka CHADEMA, ACT, CUF au vyama vingine HUJAWAPA UJUMBE HUU? Huu, nasema tena ni UCHOCHEZI wenye nia ya kuleta misigano ndani ya jamii kwa ujumla na ndani ya CCM kwa upekee. Au nikuulize, huko kwenye vyama vingine hakukuwa na waliokatwa yaani kila nafasi ilikuwa na mgombea mmoja mmoja? Hakukuwa na ushindani huko? Hebu tueleze nia na lengo a ujumbe huu?
Hahaha kumbuka huko vyama vingine mshindi ndiye aliyesimamishwa kugombea.

Hakukuwa na haja ya kura za maoni kama hamkuwa mnahitaji maoni ya wananchi.

Pia kama wenye chama hawakuhitaji wakakukata, unasubiria uteuzi hewa, aliyekukata hawezi kukuteua ni ujinga kukuamini.

Hakuna uchochezi ni ushauri wa bure kwa hao wanaodanganywa kama watoto wadogo.
 
Tunaendelea kuwakataa wote ambao wametevliwa juu, zengwe lá hujuma lazima tulifanye kwenye uchaguzi
Nalog off
 
Unamaanisha Dada wa Segerea aliyekwata kapewa John Mrema au nabii Shila kule Kilombero ambapo CHADEMA walicheza sarakasi au?!
Hakuna aliyekatwa segerea, yule mama ni mgombea Kyerwa.

Na kumbuka hakuambiwa ampigiw kampeni John Mrema, na akuahidiwa vyeo.

Hii ni kwa wale walioporwa ushindi waliodanganywa watapewa vyeo vingine na kuambiwa wawapigie kampeni mahasimu wao.
 
Yaani haujafaa panapohitaji kujua kusoma na kuandika tu kisha ukafae wapi??😂😂
Hahaha ajabu hiyo, halafu nao wanangoja kuteuliwa. Eti unasikia Polepole kasema.

Huyo aliyepewa chako ndiye alipaswa kuteuliwa, wewe pambana kwenye uchaguzi ushinde wananchi wampate waliyempenda.
 
Ulikuwa mshindi halali kura za maoni, lakini Watawala wajuu wakakukata jina lako na kumuweka mtu wanayemtaka.

Kisha mliokatwa mkaambiwa muwapigie kampeni hawa mahasimu wenu, kwa ahadi kwamba mmeshafanyiwa vetting mtateuliwa kwenye nafasi zingine...
Kumbe kura za wazi ilikuwa kiini macho au gilba? Walikuwa na watu wao mifukoni. Ni hiri yao kubaki CCM au kutimkia vyama vingine. Ila ahadi waliopewa ni danganya toto.
 
Hahaha watimke tu, kubaki huko ccm ni ujinga.

Mtu mzima unaahidiwaje kupewa cheo, unaporwa ushindi halali?!
 
Back
Top Bottom