Shule yetu iyunga ya ufund ipo katika mkoa wa mbeya
magharibi mwa jiji la mbeya,elimu ya iyunga ya kisasa
ya kitanzania kuiendeleza ni daima x2
Nilikua nachukia kuimba huu wimbo wa shule kila juma tatu na maswala ya kukaguana assembly asubuh na kina mwambene,ndudi, mshana na mng'ong'o aka dude. Ikifika usiku ni kuishia lumbila kwenye muvi huko huko na kukutana na watoto.Asubuhi ikifika wenye ela zetu tunakimbilia kiyunzo kwenye maziwa mazitoo ombea uko usikutane na kina ndudi ni msala.
Ikifika disco ni toto za loleza apo kila mtu atajitahid kuoga japo na lile barid lilikua ni noma sasa ukute mtu ana pafyum itagongewa na washkaj mkiingia wote mnanukia pafyum ya aina moja had madem wanagundua.
Kwenye soka sasa ndo usiseme ni vurugu,shule kama meta,kalobe tukikutana nazo ni vita tu.Yale maisha yalikua ni vurugu vurug tu hadi raha yan