Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hapa umeingia sehemu usiyotakiwa. hebu jaribu kuingia. HAPA nadhani hapa panakuhusu sana
Hv afande ntibwela yupo jamani maana yale matusi yake yalitusababishia majanga assembly tulicharazwa sitokaa ni sahau....siku hiyo asubui Masawe yuko mbele anahutubia ntibwela akawa anazingukia mistari ya wanafunzi na yale matusi yake kosa kijana mgeni akacheka bwanabwana akabwatuka afande wanakucheka huku walikuja ma MP tulichangamkiwa sitokaa nisahau.
Skaponda (shozniga) niliskia amefariki.
Hivi afande njenje (Bakuza) naye yuko wapi
Dah kumbe!
Basi mwenzio nilidanganywa na NECTA kuwa nimefaulu hata cheti walikipamba kwa flying colours.
Mkuu Mtamile mbona unabishana na huyo jamaa bana hii thread ni kwa ajili ya wana Jitegemee na kama tulifail darasa la saba au form four haimuhusu ili mradi tunazungumzia Jitegemee tuliyosoma
Na yeye huyo jamaa aanzishe uzi wa Tabora boys na Mzumbe kwa wana special school wazungumzie yao
Hakuna mtu aliyemkaribisha hapa kuja kusoma masuala ya wana Jitegemee wakati hayamhusu na hayapendi au azungumze na watu walio "fail" akakae na waliofaulu wenzake wa tabora boys na mzumbe bana
Hahahaha namkumbuka sana Kwame.We Paw unamkumbuka Kwame eti sasa ni mwalimu kule dodoma nkacheka sana yule jamaa alikua mtu wa matukio sana najua utakua lazma unamjua au ndo wewe Paw
Hahahaha namkumbuka sana Kwame.
Nilimuacha darasa moja nyuma. Jamaa alikuwa maarufu sana kwa matukio. Ila hata mie nilipoambiwa ni Mwalimu nilistuka sana aisee.
Enzi zile Jitegemee ilikuwa shule kamili kila idara kuanzia taaluma hadi vipaji. Siku hizi imebaki historia tu
kuna ambao walishiriki halaiki ya kuadhimisha miaka 45 ya uhuru. Tulichanganywa Jite, Chang'ombe na Kibasila, tukawa tunaletewa sausage na kuku wa Jana, wanaume tukaweka mgomo, hakuna kufanya tizi, Mkisi kaja anatubembeleza watu tumedinda, kesho tukaanza kusign posho buku 5. Ha ha! Pigwa sana na jua, sura inakua na rangi saba.. Komwe limebabuka kwa kwata..! Mpo walengwa?
Nimesoma muda huu kwenye FB kwamba yule mwalimu mtaalam wa adhabu tatanishi (Mr. Ndeha) alishafariki dunia.
Mwenye kumfahamu huyu mwalimu, unamkumbukaje?
Hali ni mbaya sana wakuu. Hebu kama alumni tunaojivunia shule yetu iliyotufikisha tulipo tuisaidie kurejesha heshima na performance yake.
Nafikiri kwanza tuanze na reunion, hapo tukutane na tuunde executive committee kwaajili ya kufacilitate na kuja na ideas on how we can help Jitegemee.
Kuna watu wa muhimu sana katika nchi hii waliotoka hapo, ila ni kama hawaioni vile, na kama wanaiona basi hawajui waanzie wapi, Mh. Massawe, Kiswaga, Mkisi....shule inazidi kuzama na kunasa kwenye tope la kuwa kitovu cha matokeo mabaya.