Walioteuliwa Kwenye Kamati ya Hamasa ya Taifa Stars hawa hapa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii nchi ukiwa mwepesi wa Kucheka unaweza kupasuka Mbavu , Yaani Wahuni ndio wanaoteuliwa eti kwenye kuhamasisha timu ya Taifa .

Kwenye kikosi hicho yumo Mwijaku aliyeshindwa kutimiza ahadi yake ya kutembea uchi ikiwa timu yake ingefungwa.
---
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro ameteua Kamati Maalum kwa ajili ya hamasa kwa Timu za Taifa zilizofuzu mashindano mbalimbali ya Kimataifa ambayo inaundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu pamoja na Wajumbe 15.

Kamati hii itakuwa na jukumu la kuhamasisha Mashabiki na Wapenzi wa michezo ndani na nje ya Nchi kujitokeza kuzishangilia na kuziunga mkono Timu za Taifa pamoja na kuratibu hafla maalum ya harambee ya kuzichangia Timu za Taifa inayotarajiwa kufanyika January 10, 2024 Jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa atamuwakilisha Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya harambee hiyo.

Wajumbe wa Kamati walioteuliwa ni Theobald Sabi (Mwenyekiti), Patric Kahemela (Makamu Mwenyekiti) na Neema Msitha (Katibu) huku Wajumbe walioteuliwa wakiwa ni Beatrice Singano, Michael Nchimbi, Jemedari Said, Nick Reynolds (Bongo Zozo), Hamis Ali, Christina Mosha (Seven) , Mhandisi Hersi Said, Salum Abdallah (Try Again), Paulo Makanza – Mjumbe,

Wajumbe wengine ni Mohamed Soloka, Hassan Mohamed Raza, Lucas Mhavile (Joti), Oscar Oscar (Mzee wa Kaliua), Prisca Kishamba, Burton Mwemba (Mwijaku) na Clayton Revocatus Chipondo (Baba Levo).


Theobald Sabi, Mkurugenzi Mtendaji NBC


Patrick Kahemela, Afisa Mtendaji Mkuu Azam Media


Neema Msitha, Katibu Mtendaji BMT

Beatrice Singano, Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Tanzania

Jemedari Said, Mtangazaji wa EFM Radio



Nick Reynolds (Bongo Zozo), Mhamasishaji wa Taifa Stars

Christina Mosha (Seven), Mkuu wa Masoko Sony Music


Hersi Said, Rais wa Yanga SC

Salum Abdallah (Try Again), Mwenyekiti wa Bodi Simba SC

Mohamed Soloka, CEO K4SSecurity

Clayton Revocatus Chipondo (Baba Levo), Msanii na Mtangazaji wa Wasafi Media

Burton Mwemba (Mwijaku), Msanii na Mangazaji Clouds Media


Prisca Kishamba, Mtangazaji wa Michezo Clouds FM

Lucas Lazaro Mhuvile (Joti), Mchekeshaji

Oscar Oscar (Mzee wa Kaliua), Mtangazaji wa Wasafi FM
 
Kuna Watu Wawili hapa ni Wanaume Jina tu ila siyo Wanaume Kamili Wamejumuishwa hivyo naiona kabisa tayari Nuksi imeingia na Taifa Stars inaenda Kufanya vibaya mno.
 
Hamasa wanayohitaji wachezaji ni pesa tuu, na hamasa wanayo hitaji mashabiki ni matokeo mazuri tuu, kama timu itaendelea kufanya vibaya hata wakimuweka nani kwenye huo upuuzi wao mashabiki wataendelea kua wachache uwanjani, labda kama ni Chaka la kupiga hela watu wanatengeneza
 
Hivi nani katuroga? Tangu lini mafanikio ya mpira yakategemea wingi wa mashabiki?

Ingelikuwa hivi kusingelikiwa na haja ya sports academy wala kutafuta makocha wazuri.

Nchi imejaa upumbavu hii. Usikute wanaliowa hawa kwa ushubwada huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…