Waliouza madafu kwenye futari ya Ikulu wahojiwa, mmoja ni mwanafunzi wa Chuo cha NIT. Ni wauza madafu kweli?

Waliouza madafu kwenye futari ya Ikulu wahojiwa, mmoja ni mwanafunzi wa Chuo cha NIT. Ni wauza madafu kweli?

Embu kujeni wasikieni ilikuwaje kuwaje hadi kuingia Ikulu.

Wengi wanasema ni Usalama.

===

Clouds wameongea na Samweli Vomboteka, mmoja wa kijana aliyeonekana kwenye hafla hiyo wakiwa na matenga ya madafu. Samweli amesema kijiwe chao ni kipo maeneo ya AtoZ supermarket karibu na Ocean Road, na madafu wanayatoa Kigamboni.

Walilipwa pesa kiasi gani?
Hakutaja kiasi cha pesa walichouza kwa dafu moja, ila Rais Samia aliwapa milioni kadhaa bila kutaja ni milioni ngapi hasa.

Walipataje mualiko?
Mh Magoti ndio aliwapitia akawaambia waandae mzigo na kuwaambia pa kupeleka na muda ulipofika walipeleka

Je, wana historia ya kufanya kazi serikalini?
Anasema hawajawahi kuajiriwa serikalini imekuwa bahati tu wakapata nafasi hiyo, akieleza yeye Logistic NIT mwaka wa 2 wakati mwenzake hasomi na kuuza madafu ndiyo shughuli yao kuu.

Mtaani wanasemaje?
Wanapewa hongera kwa kupata bahati kufika Ikulu na kupata nafasi kama hiyo kiujumla, baadhi wakitamani wangekuwa wanauza madafu na kuangukiwa na bahati kama hiyo.

clouds imefubaa dah...
 
Yaani nimecheka Hadi machozi.

Sasa wewe Jichanganye useme hujawahi muona huko Chuo akisomea Logistics 😆😆😆😆😁😁🔥🔥🤪🤪🤪🤣

=====


Producer wa LeoTena prapraf.paparaz amezungumza na Samweli kwa njia ya simu ,mmoja kati ya vijana wauza madafu walio alikwa iftar Ikulu siku ya Jumanne.
 
Back
Top Bottom