Waliozusha vifo vya Mbowe, Mrema, Maria Sarungi na leo mzee Sarungi wanajulikana

Waliozusha vifo vya Mbowe, Mrema, Maria Sarungi na leo mzee Sarungi wanajulikana

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Magazeti ya Fahari Yetu, Tanzanite na Jamvi la Habari kila siku yanaandika habari za uzushi na uongo na mhariri wake Habibu Mchange anajulikana lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na serikali kukomesha tabia hii.

Juzi Waziri Mkuu alishangazwa na watu kukosa uzalendo na utu kwa kushangilia ugonjwa wa mtu, tusisahau kuwa tunapolea uandhishi kama huu tunalea tatizo lenyewe. Jeshi la polisi linapobagua wananchi kiutendaji linapelekea wananchi kuichukia serikali na viongozi wake.

Tunaiangamiza jamii yetu sisi wenyewe kwa ujinga wetu na kukosa maarifa, tunaacha kuwakemea wanaojulikana tunakimbilia kupambana na Kigogo wa Twita asiyejulikana.



D8E83DBD-87A6-4325-945E-1039BA314F9F.jpeg
 
Double standard unafiki mpaka kwenye mimbari,kujipendekeza na njaa.
Siasa chafu na propaganda walianzisha wao wenyewe, ila sasa meza imegeuka imekua wanaita watu sio wazalendo kutangaziana vifo na maradhi.

Wao walifikia hatua kuita watu mashoga na mbwa.

Hii ni sawa na mtu umpige konzi, halafu yeye akulime ngumi mpaka meno yote ya sebuleni yatoke. Then ulalamike amekuonea.
 
Hivi wanauza gazeti kwa habari kama hizi?

Ni akina nani wanaopenda kusoma habari za aina hii kwenye magazeti kama hayo, akina YEHHOODIYA na wenzake akina Jinga/Magonjwa?

Si ajabu magazeti haya yakawa yanapata ruzuku!
 
Hii habari ilimuhusu nguruwe Sarungi mkuki hauwezi kuwa mchungu. Ungemuhusu binadamu ungekuwa mchungu na hatua za kukamata mzushi zingechukuliwa. Lazima mjue Kuna nguruwe na binadamu. Hata nguruwe Lisu aliyepigwa risasi pale Dodoma Kuna hatua yoyote iloyochukuliwa? Angepigwa binadamu ungeona.

Nguruwe Mwangosi (RIP) alisambaratishwa na bomu na binadamu akapanda na vyeo. Alafu mnalia na UZALENDO. UZALENDO NGANI WA NGURUWE NA BINADAMU?. UZALENDO wa kweli utakuja wenyewe siku Mkitambua hakuna NGURUWE wote ni BINADAMU.
 
Hii habari ilimuhusu nguruwe Sarungi mkuki hauwezi kuwa mchungu.ungemuhusu binadamu ungekuwa mchungu na hatua za kukamata mzushi zingechukuliwa. Lazima mjue Kuna nguruwe na binadamu.hata nguruwe Lisu aliyepigwa risasi pale dodoma Kuna hatua yoyote iloyochukuliwa?...
Kumbe nikweli walivyosema wahenga malipo yapo hapahapa duniani wengi waliotenda maovu tumeshudua yakiwarudia 'back firing'
 
Back
Top Bottom