Waliozusha vifo vya Mbowe, Mrema, Maria Sarungi na leo mzee Sarungi wanajulikana

Waliozusha vifo vya Mbowe, Mrema, Maria Sarungi na leo mzee Sarungi wanajulikana

Magazeti ya Fahari Yetu, Tanzanite na Jamvi la Habari kila siku yanaandika habari za uzushi na uongo na mhariri wake Habibu Mchage anajulikana lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na serikali kukomesha tabia hii.

Juzi Waziri Mkuu alishangazwa na watu kukosa uzalendo na utu kwa kushangilia ugonjwa wa mtu, tusisahau kuwa tunapolea uandhishi kama huu tunalea tatizo lenyewe. Jeshi la polisi linapobagua wananchi kiutendaji linapelekea wananchi kuichukia serikali na viongozi wake.

Tunaiangamiza jamii yetu sisi wenyewe kwa ujinga wetu wa kukosa maarifa, tunaacha kuwakemea wanaojulikana tunakimbilia kupambana na Kigogo wa Twita asiyejulikana.



Ila mwananchi wa kawaida jichanganye uone watakachokufanya
 
Maadui Wa Nchi Yetu Ni Hawa:-
1. Umasikini
2. Ujinga
3. Maradhi




😑😐

Hao maadui wamekuwepo duniani kote,cha msingi CCM mtuambie toka tupate UHURU hadi leo mnapambanaje na hao maadui?
Mwl.Nyerere alituambia ili tuendelee tunahitaji vitu vinne,ardhi,watu,siasa safi na uongozi bora.Tunakwama wapi?Maana ardhi na watu tunavyo na haihitaji juhudi yoyote ile-Labda kudhibiti idadi ya watu kutokuongezeka kwa kasi.Kwa mantiki hiyo CCM imekosa siasa safi na uongozi bora na hii inaondoa uhalali wa kuiongoza Tanzania.Wapisheni wengine tunaowahitaji kutuongoza.
Nchi hii kwa raslimali ilizojaaliwa kuwa maskini na aibu kubwa kwa siasa zetu na viongozi wabinafsi waliotawala miaka yote hii huku wakifurahia nchi kuwa omba omba na kopa kopa.
 
Hili gazeti lina andika habari za kizushi na vyombo vya dola vinaliaacha.

Kwenye nakala zake wiki hii limetoa taarifa za misiba ya viongozi ambao bado wanaishi

1. Mbowe m/kiti chadema
2. MREMA kiongozi chadema
3. PROF sarungi waziri mstaafu

Hata kama kuna chuki juu ya wapinzani lakini police hata kwa unafiki wangeweza kuwachukulia hatua , maana hili gazeti linalichafua jeshi la police lionekane ni tawi la chama cha mapinduzi.

Swali langu, nani anamiliki hili gazeti maana inaonekana ana nguvu kuliko jeshi la police.
FB_IMG_1615700645151.jpeg
 
Kimsingi BABA ukishapoteza tu mwelekeo ndani ya nyumba! Kwa sababu yoyote ile, nyumba lazima iyumbe! Kila mtu atakuwa kambale.

By the way, hakuna Mtanzania asiye fahamu ya kwamba baadhi ya vyombo vya dola na hasa polisi na tiss vinatumika kwa maslahi ya ccm badala ya Nchi.
 
Kuna mtu akiondoka itakua shangwe badala ya huzuni maana wameonea sana wengi kwa uzushi
 
Back
Top Bottom