Walipoanzisha Mpango wa biashara ya saa 24 Kariakoo walidhani nani atakesha na atamuuzia nani?

Kabla ya kuanzisha mpango huu sisi wengine tulidhani labda wangefanya utafiti wa kujua Wateja wa maduka ya kariakoo wanatoka wapi.

Ukijua wateja hao wanakotokea bila shaka utajua pia kama usafiri wa kuwaleta kariakoo usiku huo wa manane unapatikana.

Katika Nchi ambayo Usalama wa Raia siyo kipaumbele ni nani anaweza kutoka Mbagala, Bonyokwa, Mwanyamala kisiwani au Buza kwa Lulenge usiku mnene kwenda Kariakoo kununua bidhaa, Ili iweje?

View attachment 3250226
Hivi mlishawahi kuunga mkono wazo lolote la serikali?
 
..ila sio kitu kibaya kiongozi..ni kama usafiri wa mabasi ya usiku..now kila Mtanzania anaprefer kusafiri usiku..ni mwanzo mzuri..TUTAZOEA
Mkuu, unalinganisha vitu viwili visivyoendana.

K/koo unatakiwa uzunguke duka moja mpaka duka lingine, una pesa kibindoni, wavuta bangi, vibaka ndo muda wao.

Magari ya usiku unamwita boda chap, daladala ➡️stand/ofisi unadaka bus.

Kama mchana tu vibaka wanapita na vitu, huo usiku itakuwaje?
 
Kabla ya kuanzisha mpango huu sisi wengine tulidhani labda wangefanya utafiti wa kujua Wateja wa maduka ya kariakoo wanatoka wapi.

Ukijua wateja hao wanakotokea bila shaka utajua pia kama usafiri wa kuwaleta kariakoo usiku huo wa manane unapatikana.

Katika Nchi ambayo Usalama wa Raia siyo kipaumbele ni nani anaweza kutoka Mbagala, Bonyokwa, Mwanyamala kisiwani au Buza kwa Lulenge usiku mnene kwenda Kariakoo kununua bidhaa, Ili iweje?

View attachment 3250226
Ukikabwa,Siasa zingine jau!
 
Back
Top Bottom