Walipoanzisha Mpango wa biashara ya saa 24 Kariakoo walidhani nani atakesha na atamuuzia nani?

Kulipaswa kuhakikisha Usalama kwanza kabla ya jambo hili, kufunga Camera 40 kariakoo ikiwa sisi wateja tunaotokea vingunguti au Tandika Davis kona ni usanii wa kiwango cha chini sana.

Usalama wa Raia Tanzania ni jambo lisilowezekana, kwa mfano game za usiku pale panapoitwa kwa Mkapa ni kiama, watu wanaporwa kila kitu na Askari wamejaa wanaangalia mpira huku Muliro akiwa meza kuu akishabikia timu yake ya Yanga
 
Upo sahihi kabisa.
Camera hazizuii mtu kutokuibiwa ila zitaonesha tukio baada ya mtu kuibiwa ama kuchinjwa.
 
....wanasema kamanda Mafwele ameandaa mpango mzito dhidi ya wahalifu na VIBAKA hapo Kariakoo......
 
Ulinzi ukiimarishwa vibaka hawatakuwa na nafasi
 
Ni swala la muda tu.

Wanunuzi wa rejareja haiwezekani kwa kuwa muda huo wa usiku wanakuwa wamepumzika kwa usingizi. Lakini kwa wanunuzi wa jumla usiku ni muda mzuri kufuata mzigo kariakoo. Mchana inaweza kuwa kufanya malipo lakini usiku kupakia mzigo kwa kuwa msongamano wa watu na magari unakuwa umepungua. Serikali ikiamua kuweka wapiga doria eneo hilo pekee kama inavyofanywa kwenye viwanja vya mpira kwa usalama wa raia mambo yataenda. Kupitia tozo za soko posho zitapatikana kwa ajili ya polisi wa usalama wakati wa usiku. Huu ni mwanzo mzuri
 
Waimalishe ulinzi kwanza ,madefenda ya patrol yawe mengi ,control room za survillance ziwe active na nyingi ,mwendokasi zipige kazi usiku 24hrs na asubuhi hizo gari zipumzike kwa ajili ya performance.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…