Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Toka chanjo imetoka, serikali chini ya Magufuli imekuwa inaweka hofu kwa wananchi juu ya usalama wa chanjo. Rais alisema waziwazi kauli za kupinga chanjo. Alisema kama wazungu wanaweza kutengeneza chanjo basi wangetengeneza chanjo ya UKIMWI. Watu kama Kigwangalla wakatoa kauli kupinga chanjo kijanja.
Wakiunga mkono malimao na sauna kuwa ni salama huku wakipinga usalama wa chanjo. Gwajima askofu akapiga kelele bungeni kupinga chanjo huku Gwajima daktari akipiga meza kwa nguvu na kutingisha kichwa kuunga mkono. Na waliwaaminisha ugonjwa huo haupo Tz, wanafikiri ni rahisi kuwaaminisha watz kuwa upo te
Baadaye kidogo ndiyo wakaja na habari kuwa wanasubiri wataalamu wa ndani wapitie chanjo kuona kama ni salama. Ghafla bila hata kusema huo utafiti wa wataalamu wa ndani umesemaje wanaanza kuwaaminisha wananchi kuwa chanjo ni salama, na kushangaa watu kupinga kuchanjwa.
Watanzania hawajawahi tilia shaka usalama wa dawa wala chanjo mpaka serikali ilipoanzisha hilo. Serikali inabidi iombe msamaha kuwa ilikosea namna ya kupambana na Korona, na iwekeze nguvu kweli kuwapa watu elimu na kuwaaminisha watu kuwa chanjo ni kitu kizuri, na si stunts za kina Gwajima daktari kukimbia.