Mkuu, hili jambo lijadiliwe nje ya siasa hizi za siku hizi.
Hakuna asiyependa uhifadhi. Hakuna anyependa kuvuruga 'ecology'; kila mmoja wetu anaelewa umuhimu wake. Kwa hiyo hili swala halipingiki.
Kinachoudhi ni haya mambo mengine ya nayojitokeza kuwa ndiyo kichocheo cha watu kuyumbishwa hovyo.
Hakuna sababu ya serikali kuonekana kutokuwa wawazi kwa wananchi wao.
Watu wa kwanza kabisa ambao wangeelezwa juu ya hiyo 'ecology', ni hao hao wananchi wanaoishi huko mika yote tokea wazaliwe.
Hawa ndio wangekuwa watu wa mwanzo kabisa kupambania raslimali hii isiharibiwe, na wao wenyewe ndio wangekuwa ni walinzi namba moja wa raslimali hiyo.
Hali ni tofauti kabisa, serikali inaamini kutumia uongo, na uongo ukikataliwa, wanatumia mabavu!
Ninaamini kabisa, kuwashirikisha wananchi kungefanya hali kuwa rahisi zaidi; lakini serikali haifanyi hivyo kwa sababu kuna watu wenye maslahi yao humo. Hili ndilo kosa kubwa.