Waluguru wanafukia ufuo wa maiti chumbani

Waluguru wanafukia ufuo wa maiti chumbani

Aaaah, sili tena chakula msibani. Kumbeee!!!!😠😠😠
... sio misiba yote lakini! Pale unapoona roho yako inakataa, una haki ya kukataa kula.
 
Acha kudanganywa,ukadanganyika,hata wakristo wanaoshwa na kusafishwa,unafikiri wakristo hawaoshwi.Sasa wanapooshwa hayo maji,pia wanachanfanya kwenye chakula cha msiba.Tumieni akili wakristo,sio kila mnalodanganywa mnadanganyika,ndio mkaamini kuwa Yesu,alipigwa na kusulibiwa,bila hatakujiuliza,alipigwaje na kusulibiwa ,wakati yeye ndio mkombozi,mkombozi anashindwa kujikomboa.
Kwahiyo hamtolewi mavi mkidedi?
 
Achana na mawazo ya kipumbavu, mungu hayupo na hata kama yupo hana mawazo ya kitaahira kama yaliyoandikwa kwenye vitabu vyenu vya dini. Kwamba mungu yuko very much interested na mavi ya mtu, ana akili kweli?
Dini Nizawatu Wenye Akili Kuja Kuwaibia Wapumbavu

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Acha kudanganywa,hakuna kitu kama hicho,mbona wakristo mko wepesi kudanganywa mkadanganyika.Ndio maana,mkaamini mkombozi wentu,alipigwa na kusulubiwa,vipi ashindwe kujikomboa mwenyewe kwenye kipigo na kusulubiwa,aje akukombowe wewe.
Akili yako ni sawa na ya mungu wako.

Wewe mtu yoyote anaeponda dini yenu na mungu wenu wa qiquma lazima awe mkiristo?

Huwezi kua na akili timamu ukawa mfuasi wa huyo mungu.
 
Mtu yoyote anapofariki,misuli ya mwili wake,haifanyikazi tena.Kila kuliko na tundu,kama kuna uchafu,kinyesi,damu,usaha,hutoka.Wapo wengi wanaofariki na haja kubwa inawatoka,haja ndogo pia huwatoka,inategemea na maiti amefariki vipi,wapo wanaofariki kwa ajali,wanaofariki hawakuumwa,au wameumwa mda mfupi,na wana nguvu,kwa hiyo ndani ya miilli yao kuna mabaki ya chakula(kinyesi),au mkojo au damu ya ajal,wengine wameumia kwa ndani,damu zinavuja mdomoni,puani,kwenye njia za haja kubwa na ndogo,unafikiri bila kusafishwa na kutolewa hivuyo vinavyotoka,hata kwa mkristo,utaweza kuuaga mwili,hiyo harufu ya vinyesi,damu,usaha,mikojo,si itakuwa mnabana pua.Hata maiti za kikristo,husafishwa,ila kwa vile hamsomi dini zenu,huwa hamjui.Na kwa vile kazi hiyo hufanywa na watu malukmu,wanaoliopwa,hamjui hayo.
Sijui maana ya reply yako. Labda ueleze unataka kumaanisha nini
 
Siyo hilo kabila tu, sema wote wanafanya hivyo ila mambo hayo wakati mwingine yanakuwa kimya kimya tu.

Kibaya zaidi ni matumizi ya hayo maji na waste products zake.
 
Vipi kuhusu matumizi ya hayo maji?
Mtoa mada acha uzwazwa, mtu kuoshwa ni taratibu ya lazima kwa muislam yoyote atayekufa na maiti yake kupatikana. Kuna heshima ya kumtendea marehemu haswa akiwa alikua na nyumba yake mwenyewe ambayo moja wapo ni kuoshewa nyumbani kwake nai inapendeza wakati kumuosha kama ni nyumbani lichimbwe shimo ili maji yatoyotokana na kuosha yaingie na kuyafukia kazi inapomalizika iwapoitashindikana basi unawekwa mchanga mfano wa beseni kuzunguka sehemu anayooshewa kisha wanafukia na kuzoa ule mchanga.

Sasa kama mtu nyumba ni yako kuna ubaya gani mtu ananyumba yake amefia nyumbani watu wakachimba shimo ili kutimiza sharti la marehemu kuoshwa!? Tena wengine huwa wanaandaa kabisa sehemu ambayo itafanyika hiyo shughuri.

Masharti ya uislam kwa mtu mwenye imani ya kiislam akifa ni Kuosha, kuvishwa sanda, kusaliwa na Kuzikwa. Katika kuosha ndio kuna kitendo cha kukafini ili kuondoa uchafu uliopo tumboni na sio lazima uchafu utoke ila kuoshwa ni lazima.

Sio vizuri kupotosha kitu ambacho hauna elimu nacho kama wewe ni mpenda nasaba basi usiwapangie watu namna ya kuagana na wapendwa wao kwa vile wewe unaogopa chumba alichooshewa marehemu.
 
Tumia akili,acha kudanganywa,ukadanganyika.Kama kinyesi kinachanganywa,kwenye chakula,hayo maradhi ya mlipuko,yangekuwa hayachezi mbali,sehemu hizo.
Na hao mabibi afya na mabwana afya,Waone hivyo,wakae kimya,bila kuwafungulia mashtaka wahusika.
Kweli siwezi kuamini,haiwezekani eti kinyesi kuchanganywa kwwnye chakula,

Coz mwenyewe napenda sana kupika msibani,sijawahi kuona hivyo,

Maneno ya watu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo hamtolewi mavi mkidedi?
Hata wewe ukifa unaweza kutolewa mavi,inategemea umekufa vipi.Kuna wanaokufa wakitoka mavi,mkojo,damu,usaha na kuharisha,udenda.Vifo vipo vya aina nyingi,kuna ajali,kuna kufa kwa kipindupindu,kuharisha,kufa kwa ghafla.Nk.
 
Mie naona labda ni mila

Hapa jirani,baba mwenye nyumba alivyofariki walimuoshea ndani,tena hicho chomba walkitindua kabisa,,na yale maji walinawishwa usoni wafiwa wote.na kabla ya gari iliyobeba jeneza kuondoka yale maji yanamwagwa barabarani. ,,niliuliza kwanini mnatumia hayo maji kunawishwa usoni??.......wakaseme eti wakinawishwa yale maji wanakuwa hawaogopi.

Huu ulikuwa msiba wa KIKRISTO.

Nyie endeleeni kukariri,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo nimehudhuria msiba wa waluguru nimeona mambo ya kushangaza naomba mnisaidie maelezo.

Mtu amefia nyumbani kwake tena chumbani kwake anapolala na mke wake.
Sasa kwakuwa marehemu ni muislam wameamua kupitia mila ya waluguru kumuosha mwili wake mulemule chumbani.

Kilichotokea wamechimba shimo mule chumbani kwake na ni nyumba ya smenti wametindua smenti mpaka kukawa na shimo halafu marehemu wakamkafini hapohapo kwenye shimo chumbani. (wasiojua maana ya kukafini ni kumtoa mavi marehemu kabla ya kumzika) walipomaliza kumkafini yale maji yakaachwa mulemule chumbani alipofia marehemu.

Nikauliza sasa hayo maji inakuwaje wakasema hiyo ni mila ya waluguru yani mtu anaacha wosia kabisa kwamba nikifa ufuo wangu uachwe humuhumu chumbani. (Ufuo ni mavi ya marehemu)

Sasa kitakachofanywa baadae eti pale patasakafiwa hivyohivyo na maji ya marehemu pamoja na kinyesi kilichotoka baada ya kukafiniwa.
Aisee upuuzi mkubwa sana huu tena uchafu
 
Back
Top Bottom