Wamachinga wauza Juice Karume Ilala

Wamachinga wauza Juice Karume Ilala

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Hivi jamani kuna mtu ameshawahi kupita maeneo ya Karume sokoni opposite na TFF akakutana na wale jamaa wanaouza Juice?
Yaani jamaa wale ni wajinga sana kuna siku nimepita pale kwa mguu jamaa muuza juice akanichangamkia as if ananijua ananiongelesha Mambo vipi we jamaa? Habari za siku nyingi? Kitambo sana we jamaa upo?

Huku ananipimia juice ananiambia karibu sana mwanangu, nikiwa Sina hili na lile nikanywa Funda la kwanza, la pili mpaka la tatu huku navuta kumbukumbu huyu jamaa ni wapi Songea au Azania nilisoma nae? Nikawa sipati majibu. Jamaa akawa ameshawadaka wengine kwa mtindo huo huo. Nimekunywa imebaki robo glass namrudishia glass akaniambia buku tu. Ndio akili ikarudi nikajua kumbe hawa jamaa ndio ishu yao kufosi?

Nikamwambia nina jero akawa ananikomalia nikamwambia sikuuliza bei na wewe ukawa umeshanikaribisha . Chukua hii jero. Kuna mtu wa hapa Dar au aliyewahi kupita maeneo yale ikamtokea hii ishu?? 😂😂😂😂
 
Jamaa yuko Barabarani na wenzake alivyonidaka na kunichangamkia nilidhani ni mtu tunafahamiana.
Ilishanitokea Mimi Hadi nikapiga nae story za shule kuhusu Benjamin Mkapa high school.

Kumbe jamaa ananiseti aniuzie juice... Sema juice zao naonaga Kama wanatengeneza kwenye mazingira machafu ndo maana sikunywa licha ya yeye kunipa Glass.

Wako charming na wanajua saana kuunganisha story.
 
Ilishanitokea Mimi Hadi nikapiga nae story za shule kuhusu Benjamin mkapa high school.

Kumbe jamaa ananiseti aniuzie juice... Sema juice zao naonaga Kama wanatengeneza kwenye mazingira machafu ndo maana sikunywa lucha ya yeye kunipa Glass.

Wako charming na wanajua saana kuunganisha story.
[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Hapo hapo Karume 2012 walishawahi kunifanyia kama wewe nimechoka nimechakaa na bahasha yangu ya khaki natafuta kazi maofisini... jua limenipiga nina njaa si akajifanya kunijua full kunichangamkia nikajisemea kimoyoni itakuwa rafiki yangu wa utotoni huyu yeye amenikumbuka mimi nimemsahau.

Nimekunywa nimemaliza akaniambia toa 700 wakati huo sina nauli nimetoka posta kwa miguu naelekea Tandika lilitokea battle sio ya dunia hii, amechana shati mimi nimemwaga juice na keki.
 
Hapo hapo karume 2012 walishawahi kunifanyia kama wewe nimechoka nimechakaa na bahasha yangu ya khaki na tafuta kazi maofisini...jua limenipiga nina njaa c akajifanya kunijua full kunichangamkia nikajisemea kimoyoni itakuwa rafiki yangu wa utotoni huyu.
Nimekunywa nimemaliza akaniambia toa 700 wakati huo sina nauli nimetoka posta kwa miguu naelekea tandika lilitokea battle sio ya dunia hii amechana shati mimi nimemwaga juice na keki
[emoji28][emoji28][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Hapo hapo karume 2012 walishawahi kunifanyia kama wewe nimechoka nimechakaa na bahasha yangu ya khaki na tafuta kazi maofisini...jua limenipiga nina njaa c akajifanya kunijua full kunichangamkia nikajisemea kimoyoni itakuwa rafiki yangu wa utotoni huyu yeye amenikumbuka mimi nimemsahau.
Nimekunywa nimemaliza akaniambia toa 700 wakati huo sina nauli nimetoka posta kwa miguu naelekea tandika lilitokea battle sio ya dunia hii amechana shati mimi nimemwaga juice na keki
😂😂😂Mlianza kuzichapa aisee
 
Ilishanitokea Mimi Hadi nikapiga nae story za shule kuhusu Benjamin mkapa high school.

Kumbe jamaa ananiseti aniuzie juice... Sema juice zao naonaga Kama wanatengeneza kwenye mazingira machafu ndo maana sikunywa lucha ya yeye kunipa Glass.

Wako charming na wanajua saana kuunganisha story.
Ilikuaje kueje embu endelea
 
Back
Top Bottom