Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Hivi jamani kuna mtu ameshawahi kupita maeneo ya Karume sokoni opposite na TFF akakutana na wale jamaa wanaouza Juice?
Yaani jamaa wale ni wajinga sana kuna siku nimepita pale kwa mguu jamaa muuza juice akanichangamkia as if ananijua ananiongelesha Mambo vipi we jamaa? Habari za siku nyingi? Kitambo sana we jamaa upo?
Huku ananipimia juice ananiambia karibu sana mwanangu, nikiwa Sina hili na lile nikanywa Funda la kwanza, la pili mpaka la tatu huku navuta kumbukumbu huyu jamaa ni wapi Songea au Azania nilisoma nae? Nikawa sipati majibu. Jamaa akawa ameshawadaka wengine kwa mtindo huo huo. Nimekunywa imebaki robo glass namrudishia glass akaniambia buku tu. Ndio akili ikarudi nikajua kumbe hawa jamaa ndio ishu yao kufosi?
Nikamwambia nina jero akawa ananikomalia nikamwambia sikuuliza bei na wewe ukawa umeshanikaribisha . Chukua hii jero. Kuna mtu wa hapa Dar au aliyewahi kupita maeneo yale ikamtokea hii ishu?? 😂😂😂😂