Wamanyema ndio kabila pekee lenye watu majasiri, shupavu, na wajanja hapa nchini

Wamanyema ndio kabila pekee lenye watu majasiri, shupavu, na wajanja hapa nchini

Hapa ananitajia maeneo ya kisima hewa na sijui mjini mwema ndio wako waha halafu pakishua kua wenyeji uliowataja ni fukara na wanaishi maeneo duni ni kweli?
Hapana bruh sio kweli. Kwa sasa kuna wamanyema kibao ambao washaanza kurudi kwao kujenga, kwahiyo maeneo ya kishua kuna mchanganyiko wa makabila yote ya Kigoma, na wengine kutoka mikoa mingine ya Tanzania.
 
Aslimia 75 ya wakazi Kigoma ni Wamanyema? Zaidi ya Kigoma Mjini wanapatikana wapi Mkoa wote, Waha unawakuta Kasulu, Kibondo, Buigwe, Uvinza
Soma vizur kabla ya ku comment bruh. Nimesema asilia 75 ya wakazi na wenyeji wa Kigoma mjini, sikuzungumzia Kigoma yote.
 
Infact Kuna mke wa mmanyema nilimpelekea Moto Hadi akamwacha mumewe,lakini ile familia baba anakula watoto,anakula wakwe
Hii avatar uliyoweka hapo inamaanisha ww ni jinsia gani bruh. Kwahiyo baada ya kumwacha mumewe uliendelea kuwa nae au baadae alikutoka akarudi kwa mumewe?
 
Ndo nawasikia leo
Kama wewe ni wa kijijini hauwezi kuwajua wamanyema. Hawa huwa wanaishi zaidi mijini kama vile Kigoma mjini na kwa Dar wao ndio wageni wa kwanza au wa mwanzo mwanzo kabisa kukamata maeneo muhimu ya kati kati ya center kama vile Kariakoo ambapo walijenga mpaka msikiti unaoitwa msikiti wa manyema, pia maeneo ya ilala ambayo ndio inajulikana kama jiji. Sasa wewe wa huko vijijini karibu na mpaka wa malawi au msumbiji utawajuaje wamanyema bruh?
 
Ewaaaa na hasa dini ya kiislamu ujue watu wa bara walikua wanatawazia magunzi ya mahindi na udongo zamani, hata mapishi wanawake wa kiislamu hata awe kijijini sana lazima atajua kupika , nikiwa mafinga hua nakula kwa mama mmoja anaitwa mama mwislamu hatari sana
Mkuu unapozungumzia swala la dini sijui ustaarabu, sijui mambo ya kujitawaza mapishi nk, ujue kwamba 99% ya wamanyema ni waislamu kabla mkoloni hajakanyaga Tanganyika na imebaki hivyo hata mkoloni alipoondoka. Kwahiyo mila na desturi zao kwa upande wa dini hazitofautiani sana na watu wa pwani. Pwani yenyewe hasa wilaya ya bagamoyo kuna wamanyema wengi tu waliofika enzi za utumwa, na ambao sasa hivi ni wenyeji wa wilaya hiyo ya bagamoyo. Kwahiyo swala la kutumia maji kwenda msalani, kupika nk kwa wamanyema lilikuwepo toka enzi na enzi.
 
Hapana bruh sio kweli. Kwa sasa kuna wamanyema kibao ambao washaanza kurudi kwao kujenga, kwahiyo maeneo ya kishua kuna mchanganyiko wa makabila yote ya Kigoma, na wengine kutoka mikoa mingine ya Tanzania.

Basi nimejiridhisha Waha wanawashinda jamii nyingine kila kitu ikiwepo wasomi na matajiri nimeambiwa katibu mkuu wizara ya fedha muha na makamo wa Rais muha na naambiwa wana matajiri wengi huko mikoani na ndio wachapa kazi ninyi wengine ni wavivu wavivu
 
Si ndo kina ommy dimpozi hawa.
Aisee kweli ni wajanja wajanja mno full mipesa kijanja janja tu.

Note. Ujanja usizidi, utaliwa.
Ya ndo hao kina Ommy Dimpoz, Diamond, Ali Kiba, Abdul Kiba, na wengine wengi watoto wa mjini.
 
Basi nimejiridhisha Waha wanawashinda jamii nyingine kila kitu ikiwepo wasomi na matajiri nimeambiwa katibu mkuu wizara ya fedha muha na makamo wa Rais muha na naambiwa wana matajiri wengi huko mikoani na ndio wachapa kazi ninyi wengine ni wavivu wavivu
Ya waha wapo vizuri kielimu maana 90% ni wakristo, kwahiyo walianza kujishughulisha na mambo ya elimu toka enzi za mkoloni up to now. wamanyema 99% ni waislamu na waliikataa elimu ya mkoloni toka miaka hiyo na hadi leo ni wachache sana wanaojishughulisha na mambo ya elimu hii ya dunia. Wamanyema wanapenda kuishi kwa kupiga hela kwa njia za ujanja ujanja ila sio kupitia shule au biashara kama wenzao waha.
 
Kama wewe ni wa kijijini hauwezi kuwajua wamanyema. Hawa huwa wanaishi zaidi mijini kama vile Kigoma mjini na kwa Dar wao ndio wageni wa kwanza au wa mwanzo mwanzo kabisa kukamata maeneo muhimu ya kati kati ya center kama vile Kariakoo ambapo walijenga mpaka msikiti unaoitwa msikiti wa manyema, pia maeneo ya ilala ambayo ndio inajulikana kama jiji. Sasa wewe wa huko vijijini karibu na mpaka wa malawi au msumbiji utawajuaje wamanyema bruh?
Watu kama ni maarufu watajulikana haijalishi ni wap
 
Watu kama ni maarufu watajulikana haijalishi ni wap

Ndio maana wenzao waha wanajulikana kwa elimu na biashara kumbe alileta story tu za vijiweni imebidi nifanye tafiti zaidi, kumbe wamanyema walifika mjini kufanya kazi za uhousegirl na kupeleka mashuka na mawese huku wenzao waha wakiwa wanasafiri na mihogo na viazi vya kuchemsha kwenye treni ili wafuate bidhaa za duka na ndio watu hutoka makao makuu ya mkoa kwenda kununua vitu kwa waha vya jumlajumla na naambiwa waha ndio wengi huko kigoma
 
Ya waha wapo vizuri kielimu maana 90% ni wakristo, kwahiyo walianza kujishughulisha na mambo ya elimu toka enzi za mkoloni up to now. wamanyema 99% ni waislamu na waliikataa elimu ya mkoloni toka miaka hiyo na hadi leo ni wachache sana wanaojishughulisha na mambo ya elimu hii ya dunia. Wamanyema wanapenda kuishi kwa kupiga hela kwa njia za ujanja ujanja ila sio kupitia shule au biashara kama wenzao waha.

Ndio nilifanya utafiti bahati nzuri umekiri kua waha ndio wanawabeba mkoa wa kigoma anzia elimu na biashara hapo tumefunga mjadala na naona waha ndio kabila kubwa kuliko wengine huko.
 
Mkuu Ommy Dimpoz ni Muha,anatokea Kijiji kimoja Kiko Kasulu Sema nmekisahau
 
Hii avatar uliyoweka hapo inamaanisha ww ni jinsia gani bruh. Kwahiyo baada ya kumwacha mumewe uliendelea kuwa nae au baadae alikutoka akarudi kwa mumewe?
Tuishie hapo,avatar achana nayo,huwa najiburudisha nikikumbuka vitu flani
 
Mada za hovyo ka hizi
Natoa salamu kwenu marafiki na ndugu zangu. Kwa wale wasiolifahamu hili kabila. Wamanyema ni kabila linalopatikana katika mkoa wa Kigoma, hasa hasa maeneo ya mjini kama vile Kigoma mjini, Ujiji, Mwanga, Gungu na baadhi ya maeneo ya Kasulu mjini.

Yani toka enzi za ukoloni mpaka leo hii, mtoto wa mjini pale Kigoma ni mmanyema, japo miaka hii kuna waha wachache waliojisogeza sogeza na kufoji uenyeji wa mjini kwa kuiga mienendo na tamaduni za kimanyema nk.

Pia kabila hili la Wamanyema linapatikana katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Tabora, na huko Ufipa mkoani Rukwa.

Wamanyema ni kabila la pili kwa ukubwa mkoani Kigoma, kabila la kwanza kwa ukubwa mkoani humo ni Waha ambao wengi wanaishi vijijini, pamoja na makabila mengine madogo madogo.

Wamanyema ni kati ya makabila ya mwanzo mwanzo kabisa kufika katika mkoa wa Dar es salaam enzi hizo ikiitwa mzizima, kabla hata Tanganyika haijawaza au hata kufikiria kuwa kuna siku itapata uhuru.

Pia Wamanyema ndio lilikuwa kabila la kwanza la wageni kumiliki maeneo yote muhimu ambayo sasa ndio mjini kama vile Kariakoo, Ilala na Tabata.

Kwa watu wanaoishi au waliowahi kufika Dar es salaam nafikiri mnaufahamu msikiti wa Manyema uliopo katika katika ya mjini yani kariakoo, ule msikiti ulijengwa kabla ya uhuru na hakuna mkoloni yeyote aliethubutu kuugusa kwa vile hata wakoloni walilifahamu vizuri hili kabila, kwamba sio la kulifanyia mzaha hata kidogo.

Kabla mambo ya utandawazi hayajaeneo na kupelekea waha kuvamia miji kwa fujo hasa kwa mkoa wa Dar es salaam, watu wengi walikuwa wanajua kuwa Wamanyema ndio kabila pekee katika mkoa wa Kigoma.

Ila miaka inavyokwenda ndo na mambo yanavyozidi kujiweka wazi yenyewe, na kupelekea watu kujua makabila mengine ya mkoa wa Kigoma.

Wamanyema ni kati ya Makabila yaliopigania uhuru kwa kupambana na wakoloni, huku wakishirikiana na wenyeji wao wa Dar es salaam kama vile Wazaramo, Wandengereko na makabila mengine ya mkoa wa Pwani.

Tabia za wamanyema wake kwa waume ni 1] usafi 2] umaridadi 3]unadhifu. Wamanyema wengi ni maridadi sana kuanzia kwenye swala la mavazi, usafi wa mwili ndani na nje, pia huwa hawajinyimi kula.

Ni vigumu sana kumkuta mmanyema anatembeza mayai, sijui vikapu vya mafuta uzuri na biashara nyingine ndogo ndogo za kuzurula juani, hizi biashara kwa watu wanaotokea Kigoma iwe kwa mkoa wa Kigoma wenyewe, Dar au kwengineko huwa zinafanywa na waha.

Kwa mtu ambae ashawahi kuishi na wamanyema iwe jirani au nyumba moja nafikiri atakuwa amenielewa. Kama una mkeo au mumeo akinaswa na mmanyema tu basi andaa talaka, au kama mwanamke andaa kutalikiwa kabisa, maana mkeo au mumeo ndo umeshamkosa tayari.

Sifa nyingine 4]ubishi 5]kujiamini kupita kiasi. Mmanyema anaweza kutoa hela yake mfukoni akaununua ugomvi wa rafiki yake, na kuanza kupambana kwa niaba yake.

Watu maarufu kutoka katika kabila la Wamanyema ni 1]Sheikh Yahya Husein (aliekuwa mtabiri afrika mashariki) 2] Iddi Faiz Mafongo (aliekuwa mwekahazina wa chama cha TANU) 3] Iddi Tosiri 4] Iddi Simba (huyu mama alikuwa mmanyema, huku baba ni mdengereko) 5] Amri Abedi Karuta (meya wa kwanza jijini Dar) 6] Amani Kabouru (aliekuwa mbunge wa kwanza Kigoma mjini CDM) 7] Diamond 8] Ally Kiba 9] Ommy Dimpoz 10] mh Zitto Kabwe kiongozi wa ACT wazalendo (mbunge mstaafu) 11] Katibu mkuu kiongozi mh balozi Huseein A.
Katanga na wengine wengi serikalini, siasani, kwenye michezo, mziki na fani mbali mbali.

Tatizo kubwa la Wamanyema wa enzi hizo (yani mababu) ilikuwa ni ushirikina. Jambo lililosababisha wamanyema wengi kusambaa katika mikoa mingine hasa Dar es salaam na kujenga huko ili kuwaepuka vigagula hao.

Pia wamanyema hawana ushirikiano kivile katika mambo yanayohusu maisha. Iwe kazini, katika biashara na mambo mengi ya kimaendeleo huwa hawabebani kama yanavyobebana makabila mengine, yani kwa wamanyema kila mtu hubeba msalaba wake mwenyewe.

Kwa kukosa kushirikiano huo ndio maana mababu ambao ndio waliwahi kuwa wamiliki wa maeneo ya Kariakoo, Ilala, Tabata nk walipofariki, wale waliorithishwa maeneo hayo waliyauza yote kwa wahindi (K'koo) waarabu (Ilala) pia maeneo mengi ya Tabata waliorithishwa waliyauza kwa watu mbali mbali.
Sizipi nafasi kichwani mada za hovyo sana
 
Back
Top Bottom