Wamanyema ndio kabila pekee lenye watu majasiri, shupavu, na wajanja hapa nchini

Wamanyema ndio kabila pekee lenye watu majasiri, shupavu, na wajanja hapa nchini

Hauwezi kumjua mchawi kama na ww sio mchawi. Bila shaka mlishirikiana kuwala hao watu.
Kwanini asiye mchawi, hawezi kumjua mchawi, Una uhakika gani na hilo.
Kuna maneno kwenye Bibilia yanasema, usimuache mwanamke mchawi aishi, je inawezeka mlozi amuue mlozi mwenzie kwa ulozi?
 
Kama wewe ni wa kijijini hauwezi kuwajua wamanyema. Hawa huwa wanaishi zaidi mijini kama vile Kigoma mjini na kwa Dar wao ndio wageni wa kwanza au wa mwanzo mwanzo kabisa kukamata maeneo muhimu ya kati kati ya center kama vile Kariakoo ambapo walijenga mpaka msikiti unaoitwa msikiti wa manyema, pia maeneo ya ilala ambayo ndio inajulikana kama jiji. Sasa wewe wa huko vijijini karibu na mpaka wa malawi au msumbiji utawajuaje wamanyema bruh?
Haijalishi mtu anatokea mpakani Songea huko au Mtwara, makabila makubwa Tanzania yanajulikana, Wamanyema Siyo kabila kubwa Tanzania.
Bali ni kabila lilikua maarufu miaka ya nyuma, na umaarufu wao, sasa umemezwa na makabila mengine.

Upande wa ujanja, sina hakika ingawa wapo siku nyingi mjini, sijawahi kusikia mambo makubwa makubwa yanamilikiwa na wamanyema, biashara. hata nyumba za maana, nyumba za wamanyema, zilikua za kawaida tu, zimebadilishwa na wawekezaji, ambao siyo wamanyema kwa ubia, kwa kuzinunua.
 
Kitendo cha mtu kuamini Individual characteristics za binadamu zinakuwa determined na identifications zake tayari amekosa akili. Binadamu ni viumbe wenye ubongo ambao ni very sophisticated hiyo inawafanya kuwa wanaobadilika kulingana na mazingira accordingly.
Wana sifa za adaptability, flexibility na individualism.

Point kuu ni ukabila ni ujinga.
 
Natoa salamu kwenu marafiki na ndugu zangu. Kwa wale wasiolifahamu hili kabila. Wamanyema ni kabila linalopatikana katika mkoa wa Kigoma, hasa hasa maeneo ya mjini kama vile Kigoma mjini, Ujiji, Mwanga, Gungu na baadhi ya maeneo ya Kasulu mjini.

Yani toka enzi za ukoloni mpaka leo hii, mtoto wa mjini pale Kigoma ni mmanyema, japo miaka hii kuna waha wachache waliojisogeza sogeza na kufoji uenyeji wa mjini kwa kuiga mienendo na tamaduni za kimanyema nk.

Pia kabila hili la Wamanyema linapatikana katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Tabora, na huko Ufipa mkoani Rukwa.

Wamanyema ni kabila la pili kwa ukubwa mkoani Kigoma, kabila la kwanza kwa ukubwa mkoani humo ni Waha ambao wengi wanaishi vijijini, pamoja na makabila mengine madogo madogo.

Wamanyema ni kati ya makabila ya mwanzo mwanzo kabisa kufika katika mkoa wa Dar es salaam enzi hizo ikiitwa mzizima, kabla hata Tanganyika haijawaza au hata kufikiria kuwa kuna siku itapata uhuru.

Pia Wamanyema ndio lilikuwa kabila la kwanza la wageni kumiliki maeneo yote muhimu ambayo sasa ndio mjini kama vile Kariakoo, Ilala na Tabata.

Kwa watu wanaoishi au waliowahi kufika Dar es salaam nafikiri mnaufahamu msikiti wa Manyema uliopo katika katika ya mjini yani kariakoo, ule msikiti ulijengwa kabla ya uhuru na hakuna mkoloni yeyote aliethubutu kuugusa kwa vile hata wakoloni walilifahamu vizuri hili kabila, kwamba sio la kulifanyia mzaha hata kidogo.

Kabla mambo ya utandawazi hayajaeneo na kupelekea waha kuvamia miji kwa fujo hasa kwa mkoa wa Dar es salaam, watu wengi walikuwa wanajua kuwa Wamanyema ndio kabila pekee katika mkoa wa Kigoma.

Ila miaka inavyokwenda ndo na mambo yanavyozidi kujiweka wazi yenyewe, na kupelekea watu kujua makabila mengine ya mkoa wa Kigoma.

Wamanyema ni kati ya Makabila yaliopigania uhuru kwa kupambana na wakoloni, huku wakishirikiana na wenyeji wao wa Dar es salaam kama vile Wazaramo, Wandengereko na makabila mengine ya mkoa wa Pwani.

Tabia za wamanyema wake kwa waume ni 1] usafi 2] umaridadi 3]unadhifu. Wamanyema wengi ni maridadi sana kuanzia kwenye swala la mavazi, usafi wa mwili ndani na nje, pia huwa hawajinyimi kula.

Ni vigumu sana kumkuta mmanyema anatembeza mayai, sijui vikapu vya mafuta uzuri na biashara nyingine ndogo ndogo za kuzurula juani, hizi biashara kwa watu wanaotokea Kigoma iwe kwa mkoa wa Kigoma wenyewe, Dar au kwengineko huwa zinafanywa na waha.

Kwa mtu ambae ashawahi kuishi na wamanyema iwe jirani au nyumba moja nafikiri atakuwa amenielewa. Kama una mkeo au mumeo akinaswa na mmanyema tu basi andaa talaka, au kama mwanamke andaa kutalikiwa kabisa, maana mkeo au mumeo ndo umeshamkosa tayari.

Sifa nyingine 4]ubishi 5]kujiamini kupita kiasi. Mmanyema anaweza kutoa hela yake mfukoni akaununua ugomvi wa rafiki yake, na kuanza kupambana kwa niaba yake.

Watu maarufu kutoka katika kabila la Wamanyema ni 1]Sheikh Yahya Husein (aliekuwa mtabiri afrika mashariki) 2] Iddi Faiz Mafongo (aliekuwa mwekahazina wa chama cha TANU) 3] Iddi Tosiri 4] Iddi Simba (huyu mama alikuwa mmanyema, huku baba ni mdengereko) 5] Amri Abedi Karuta (meya wa kwanza jijini Dar) 6] Amani Kabouru (aliekuwa mbunge wa kwanza Kigoma mjini CDM) 7] Diamond 8] Ally Kiba 9] Ommy Dimpoz 10] mh Zitto Kabwe kiongozi wa ACT wazalendo (mbunge mstaafu) 11] Katibu mkuu kiongozi mh balozi Huseein A.
Katanga na wengine wengi serikalini, siasani, kwenye michezo, mziki na fani mbali mbali.

Tatizo kubwa la Wamanyema wa enzi hizo (yani mababu) ilikuwa ni ushirikina. Jambo lililosababisha wamanyema wengi kusambaa katika mikoa mingine hasa Dar es salaam na kujenga huko ili kuwaepuka vigagula hao.

Pia wamanyema hawana ushirikiano kivile katika mambo yanayohusu maisha. Iwe kazini, katika biashara na mambo mengi ya kimaendeleo huwa hawabebani kama yanavyobebana makabila mengine, yani kwa wamanyema kila mtu hubeba msalaba wake mwenyewe.

Kwa kukosa kushirikiano huo ndio maana mababu ambao ndio waliwahi kuwa wamiliki wa maeneo ya Kariakoo, Ilala, Tabata nk walipofariki, wale waliorithishwa maeneo hayo waliyauza yote kwa wahindi (K'koo) waarabu (Ilala) pia maeneo mengi ya Tabata waliorithishwa waliyauza kwa watu mbali mbali.
Matapeli sana
 
Haijalishi mtu anatokea mpakani Songea huko au Mtwara, makabila makubwa Tanzania yanajulikana, Wamanyema Siyo kabila kubwa Tanzania.
Bali ni kabila lilikua maarufu miaka ya nyuma, na umaarufu wao, sasa umemezwa na makabila mengine.

Upande wa ujanja, sina hakika ingawa wapo siku nyingi mjini, sijawahi kusikia mambo makubwa makubwa yanamilikiwa na wamanyema, biashara. hata nyumba za maana, nyumba za wamanyema, zilikua za kawaida tu, zimebadilishwa na wawekezaji, ambao siyo wamanyema kwa ubia, kwa kuzinunua.

Makabila makubwa tanzania ni nembo ya mikoa yao Kigoma- Waha hao wamanyema hawabebi jina la mkoa wao , Mwanza- wasukuma, Mara- wakurya, Mbeya- wanyakyusa, Iringa- wahehe, Njombe- wabena japo kwenye mikoa hiyo kuna makabila mengine madogomadogo.
 
Ndio maana wenzao waha wanajulikana kwa elimu na biashara kumbe alileta story tu za vijiweni imebidi nifanye tafiti zaidi, kumbe wamanyema walifika mjini kufanya kazi za uhousegirl na kupeleka mashuka na mawese huku wenzao waha wakiwa wanasafiri na mihogo na viazi vya kuchemsha kwenye treni ili wafuate bidhaa za duka na ndio watu hutoka makao makuu ya mkoa kwenda kununua vitu kwa waha vya jumlajumla na naambiwa waha ndio wengi huko kigoma
Acha uongo,Baba yangu mdogo yupo hapo Dar ni Mmanyema original kutoka Ujiji kwetu watu mashuhuri.....amesomea hapo Markaz Chang'ombe elimu yake ya dini....maika hiyo Dar haijastaarabika walikuwa wanaenda Dar na nguo kali,pafumu,Raba kali,sabuni za kunukia...wakifika hapo Dar vijana wakiarabu walikuwa wanawalilia wawauzie kwa bei yeyote ile kwa sababu walikuwa na vitu ghali ambavyo havipatikani Daslam...wenyewe walionekana wajanja sana kuliko wageni wengine kutoka Tanzania kwa sababu walipata hivyo vitu kutoka Congo ya mbelgiji.

Angalia watu mashuhuri wa miaka ya nyuma wote kutoka kigoma ni wamanyema mzee....achana na hawa kina Mpango na Ndalichako waliopata umaarufu hivi karibuni ndio waha...waliobakia wote ni Manyema moja,Idd Simba,Kanal Msabaha,Msambya(Naibu waziri wa nishati zamani)Dr Kaborou(Mbunge wa kwanza wa chadema) marehem,Meya wa kwanza wa jiji la Dar,Marehemu sheikh Yahya Hussein(Mnajimu mashuhuri Afrika mashariki na kati,
Wapo wengi sana wanamichezo waigizaji n.k
Wamanyema wengi wanaishi mjini kati hapo Dar ukilinganisha na Waha.
 
Yaani list yako imejaa waganga na wasanii et wajanja .wamanyema ndo watumwa waliobebeshwa ndovu na wazungu .muha namkubali alikuja mjini mshamba leo wamejua kuishi na watu .mjini wanaaminika sana muha mkikubaliana jamba linaisha
 
Kabisa wamanyema hawamfiki muha hata kidogo
Wamanyema mamwinyi tu wao hupenda kuletewa tu

Ova
 
Yaani list yako imejaa waganga na wasanii et wajanja .wamanyema ndo watumwa waliobebeshwa ndovu na wazungu .muha namkubali alikuja mjini mshamba leo wamejua kuishi na watu .mjini wanaaminika sana muha mkikubaliana jamba linaisha
Wamanyema utapeli mwingi

Ova
 
Acha uongo,Baba yangu mdogo yupo hapo Dar ni Mmanyema original kutoka Ujiji kwetu watu mashuhuri.....amesomea hapo Markaz Chang'ombe elimu yake ya dini....maika hiyo Dar haijastaarabika walikuwa wanaenda Dar na nguo kali,pafumu,Raba kali,sabuni za kunukia...wakifika hapo Dar vijana wakiarabu walikuwa wanawalilia wawauzie kwa bei yeyote ile kwa sababu walikuwa na vitu ghali ambavyo havipatikani Daslam...wenyewe walionekana wajanja sana kuliko wageni wengine kutoka Tanzania kwa sababu walipata hivyo vitu kutoka Congo ya mbelgiji.

Angalia watu mashuhuri wa miaka ya nyuma wote kutoka kigoma ni wamanyema mzee....achana na hawa kina Mpango na Ndalichako waliopata umaarufu hivi karibuni ndio waha...waliobakia wote ni Manyema moja,Idd Simba,Kanal Msabaha,Msambya(Naibu waziri wa nishati zamani)Dr Kaborou(Mbunge wa kwanza wa chadema) marehem,Meya wa kwanza wa jiji la Dar,Marehemu sheikh Yahya Hussein(Mnajimu mashuhuri Afrika mashariki na kati,
Wapo wengi sana wanamichezo waigizaji n.k
Wamanyema wengi wanaishi mjini kati hapo Dar ukilinganisha na Waha.
Umemuelewesha vizuri huyo muha wa vijijini. Anajaribu kujitutumua mjini na wakati hana hata mwaka.
 
Yaani list yako imejaa waganga na wasanii et wajanja .
Karne ya 20 bado unawaza habari za uganga, kweli wewe ni mwanakijiji. Sisi watoto wa mjini tunawaza hela na sio uganga.

Usanii ni moja ya njia ya kijanja ya kumsaidia mtu kuishi vizuri mjini.

Leo hii Davido anaonekana bora na mjanja kuliko wanasiasa wengi kule Nigeria.
 
Sawa 🤣

Kila kabila linajiona bora kuliko mengine....🤣🤣

#Siempre JMT🙏
Nyerere alikua na akil sana kulidhibit hili suala mapema.
IMagine hizo fujo zingekuaje nchi hii! 😂
UKiwasikkliza wanyaki
Ukaja kwa wahaya
Ukaenda kwa wachaga
Njoo kwa wahehe
Haya mara wasukuma
Huyu tena mmanyema.

Yaki kila mtu anajiona bora.

Salute Nyerere
 
Back
Top Bottom