Wamarekani wanamuhitaji Donald Trump sasa kuliko walivyomuhitaji mwaka 2016

Wamarekani wanamuhitaji Donald Trump sasa kuliko walivyomuhitaji mwaka 2016

Nimeona mahali anazungumza na ma tycoon wa biashara ya mafuta anawaomba wamchangie dola billion moja arudi white house

Ma Don hao wanalalamika kwa mwaka jana tu walitumia dola million 400 kufanya lobbing kwenye serikali ya Biden ili kupunguza vikwazo vya ki mazingira

Bila shaka Trump atarudi white house, rais huchaguliwa na wenye pesa
 
Trump all the way. Wakati wa Trump Dunia ilitulia. Halafu Kama sio corona Biden asingemtoa Trump madarakani
Unakumbuka alivyodili na vitisho vya Korea Kaskazini?

Sidhani kama Democratic wangevimudu hivyo vitisho.
 
Kafanya mengi Sana Trump kipindi chake. Sema democrats walikomaa na impeachment waka overshadow utandaji wake.
Kama walimshindwa kipindi hicho, hawatamuweza kwenye sanduku la kura.
 
Sera za Trump kwa wahamiaji wa mataifa mengine sio nzuri.
Hakuwa mnafiki!

Aliweka wazi tangu mwanzo kuwa lengo lake ni kuifanya America great again.

Alikuwa mzalendo kwa nchi yake.
 
Alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 2016, na kuingia Ikulu 20/01/2017 baada ya kula kiapo.

Katika kipindi cha uongozi wake, alifanya mengi, yakiwemo yaliyowafurahisha na yaliyowakwaza Wamarekani.

Ingawa alionesha chuki kwa baadhi ya Mataifa, hasa ya Kiafrika, lakini alilifaa sana Taifa lake la Marekani.

Mwaka huu Wamarekani watapiga kura ya kumchagua Rais.

Bila shaka, wengi wanajua kuwa wanamuhitaji sana Trump kuliko wakati mwingine wowote.

Uthubutu wake utawezesha vita vya Urusi na Ukraine kufikia ukomo. Anaweza kusaidia kuleta amani Mashariki ya Kati, japo itakuwa ni kwa muda tu.

Atamdhibiti Rais wa Korea Kaskazini asiwe tishio kwa Marekani na maslahi ya Marekani.

Japo si nabii, lakini naamini Trump atashinda Kiti cha Urais wa Marekani mwaka huu

Hata Wamarekani waliomo humu JF, japo ni wachache, lakini wanalijua hilo.

Hawatafanya kosa. Wameamua kwenda na bilionea Donald Trump.
WAMAREKANI HAWAJAAHI KUWA WAJINGA MARA MBILI
 
hao si watanzania wanaohitaji mtu mkali ili wasonge mbele. Walishavuka hiyo stage miaka mingi, wanachohitaji ni mwenye udhubutu, tofauti na sisi wao wana dira na sera za nchi , trump alikuwa hazifuati sana
Lakini aliyasimamia maslahi ya Taifa lake Marekani.
 
Trump ni msela muoga asiyetimiza ahadi zake sidhani kama anaweza kuaminiwa upya ilihali Yale aliyoyaaahidi katika kampeni zake hakuwahi kutekeleza alipopata madaraka.
Trump akili zake ni sawa na mshikaji wake kanye west
 
Ana utu wa kuwavuta wanawake kwa kutia mkono katika uchi wao na kuwavuta, tena anaongea hadharani!
Sidhani kama hayo Yana ukweli.

Ni kawaida watu maarufu kusingiziwa mengi. Wana maadui kila kona.
 
Ingawa kantishaaaleo makosa 34 hana hatia kaziipoo
 
Back
Top Bottom