Wamarekani wenye maoni chanya kuhusu China waongezeka

Wamarekani wenye maoni chanya kuhusu China waongezeka

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
VCG111641635122.jpg

Shirika la Utafiti la Pew la Marekani hivi karibuni limetoa ripoti ikionesha kwamba, ikilinganishwa na mwaka 2023, Wamarekani wenye maoni chanya kuhusu China wameongezeka maradufu, na kufikia asilimia 27.

Ikilinganishwa na wakati China na Marekani zilipokuwa na uhusiano wa karibu, kiwango hicho cha asilimia 27 ni kidogo sana. Ripoti ya Pew pia inabainisha wazi kwamba katika muongo mmoja uliopita, Wamarekani wengi wamedumisha maoni hasi kuhusu China, lakini hata hivyo, sasa mabadiliko yametokea. Ikilinganishwa na kiwango cha mwaka wa 2023, idadi ya Wamarekani wenye maoni chanya imeongezeka maradufu, huku asilimia ya wale wanaoiona China kama “adui” imeshuka kutoka asilimia 33 hadi 28.

Jambo la kuvutia zaidi ni maoni tofauti kati ya watu wenye umri tofauti katika ripoti hiyo, ambayo inaonesha kwamba, asilimia 34 ya Wamarekani wenye chini ya umri wa miaka 50 wana maoni chanya kuhusu China, huku kiwango hicho kikiwa asilimia 19 tu kwa Wamarekani wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 50. Vijana wa Marekani hawana mawazo ya Vita Baridi, wanajua ukweli kuhusu China kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii kama TikTok, na kwa hivyo si rahisi kwao kupotoshwa sana na vyombo vya habari vya jadi vya magharibi.

Katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya Marekani na China umekuwa na wakati mgumu ambao haujawahi kuonekana tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili. Marekani si kama tu imeanzisha vita ya kibiashara dhidi ya China, na kuiwekea China vizuizi vya kiteknolojia, bali pia imechochea uhasama wa ndani dhidi ya China. Hata hivyo, ripoti ya Pew inaonesha kwamba ufanisi wa uhamasishaji hasi dhidi ya China unaanza kupungua.

Ripoti ya Utafiti wa Pew inafanya kazi kama kioo. Inaonesha ugumu na uthabiti wa mahusiano ya Marekani na China, ikifichua si tu mgawanyiko wa kina wa maoni tofauti ya Wamarekani kuhusu China, bali pia inaonesha chipukizi zinazochipuka kimya kimya za maelewano ya pande hizo mbili. Mahusiano ya Marekani na China hayatakuwa na mabadiliko ya ghafla na makubwa katika siku zijazo, kwa sababu tu ya kura moja ya maoni. Hata hivyo, kila mabadiliko chanya, bila kujali ni madogo kiasi gani, yanastahili kuthaminiwa na kulelewa kwa makini, kwani baada ya yote, msingi wa mahusiano mazuri kati ya nchi ni maelewano ya watu wao.
 
Back
Top Bottom