Mapinduzi ya1964 hapa ZNZ yamekuwa kisingizio tuu cha kuitia nchii katika ukoloni, Uhuru wa nchi hii uliotarajiwa kuendelezwa baada ya Mapinduzi, Hatimae ulitoweka kwa Muungano wa wanamapinduzi kuiunga nchi na Tanganyika.
Lengo ilikuwa kuipoka madaraka yake ili kuikabidhikwa Tanganyika.
Muungano imekuwa kama kihalalisho cha dhamira nzima ya Ukoloni wa Mtuu mweusi kwa mweusi.
Haya yote yanayofanyika ,ni muendelezo wa kututowa kwenya ajenda ya kujikomboa, na kutufanya tuanze kusigana wenyewe kwa wenyewe .
Kwa hakika vitambulisho hivi vya Mzanzibar havina maslahi yoyote zaidi ya siasa.
Ilitarajiwa viwe kitambuzi cha cha Utaifa wetu ili kujulikana ni nani mzanzibari kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri, na nani si mzanzibari ,lakini hivi sasa hata wamasai na wamachinga wanavyo.
Kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mkoloni wala hakina masharii, unaweza kukipata hata kwa Mtandao ,
ili lengo la kuifanya nchi hii kuwa Moja, huku Utaifa wa Zanzibar ukibakia kama Laana ,na chanzo cha kusigana na kutiana hatiani wenyewe.
Kwa kina utaona kuwa Waznzibari Mapandikizi ndio vinara wa kutengeneza mizengwe hii kwa maslahi ya Kuimaliza Hadhi ya Zanzibar.
Mithili ya kuku wanaopelekwa sokoni kwenye susu, utakuta majogoo wanapigana mule na wengine kudonoana.
Wakifika sokoni wote huuzwa na kuchinjwa kwa ajili ya kitoweo cha mnunuzi.
Hata Uraisi wa nchi hii Kila siku tunawekewa Makando kando ,watu wasiokuwa wazanzibari halisi,
Karibuni hivi utasikia ,Mzaramo, au Mmakonde au Mkwere wanataka uraisi Zanzibar.
Akisimama Mmakunduchi, Mtumbatu,Muhadimu, Mshirazi au Mpemba wote watatupwa kapuni na atapewa mwenye asili ya Kando kando ili kuepuka ushawishi wa Kuleta mageuzi katika visiwa hivi, na awe mtiifu wa kwenye asili ya alikotoka.