Pre GE2025 Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Haya ni baadhi ya mabango yenye jumbe mbalimbali ambazo zimetolewa na wakazi tarafa ya Ngorongoro ambao wanafanya maandamano ya amani kupinga kile wananchodai ni ukiukwahi wa Haki za Binadamu dhidi yao.

Wakazi hao wa jamii ya kifugaji ya Wamasai wanaandamana hii leo 18 Aug 2024 kupinga kile wanachodai kuchoshwa na vitendo vya ukiukwaji wa Haki dhidi yao katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kunyimwa huduma za maendeleo ya jamii .

Wakazi hao wanadai kuwa wamevumilia kwa muda mrefu ukiukwaji wa Haki za Binadamu ikiwemo kusitishwa na kuzoroteshewa kwa huduma mbalimbali zikiwemo za afya, elimu na hata miradi mingine ya maendeleo.

Mbali na hivyo wanadai kuwa kilichowashtua zaidi ni kuondolewa kwa tarafa hiyo katika orodha ya vituo vinavyotumika katika maboresho ya daftari la mpiga kura jambo linalowaashiria kuwa watakosa Haki ya kushiriki chaguzi ikiwemo wa serikali za mitaa mwaka huu 2024 na hata ule mkuu wa 2025.


Ni muda sasa tangu wakazi hao watoe malalmiko yao juu ya kutotendewa Haki tangu kulipoanza zoezi la kuwahamisha kutoka tarafa hiyo kuelekea Kijiji cha Msomera mkoani Tanga.

Source: Watetezi tv
 
Hii nchi hii!

Loliondo scandal ilivuma na imetulia, sasa hivi Ngorongoro nayo pia ipo 'fire.'

RIP Stan Katabaro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…