Pre GE2025 Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe

Pre GE2025 Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chokochoko huwa ni mithili ya hizi na mwishowe majuto kwetu sote.....

Tatizo si baadhi ya wakazi wa Ngororongo....tatizo ni walioko nyuma yao...ndani na nje ya nchi.....

Eee Tanzania yangu....inakabwa na fitina kila eneo...lengo tuparanganyike.......

Tusifike huko....hatua stahiki zichukuliwe.....

#JMT dumu daima[emoji7]
 
Kwani Wamasai hawana hela?
Kwani Wamasai hawana watoto walipenda shule?
Kwani Wamasai wa karne hii ni kama wa kipindi kile cha ujima?
Wamasai wanaoishi Ngorongoro hawajatengwa na ulimwengu! Wanajua kile wengine wanachokifanya huko duniani linapokuja suala la kudai haki.
Acha kuwaingiza wamasai kama kabila....

Kwanini usiseme ni baadhi ya wakazi raia wa Ngororongo?!!!

Kuwaita wamasai ni kuwabagua....

Nijuacho ni kuwa duniani watu hupiga pesa ndefu kwa kutaka tuwaite "WAMASAI" badala ya raia wa Ngororongo......

Think thrice
 
Nakumbuka Mstaf General Venance Mabeyo ndio Mwenyekiti ya Board ya Wazamini wa Ngorongoro conservation Authority.

I hope hakitaharibika kitu.
Hao ndio 'turn coats' wa nchi hii; ni watu wa kutumika tu kama vikaratasi vya chooni. Hovyo kabisa.
 
Usipindishe mambo. Wanyamlenge wenyewe wanataka waonekane kuwa tofauti na raia wengine wa nchi hiyo,
Sio kweli ule mgogoro ulianza 1994/95 walianza kuuwawa na kunyang'anywa Mifugo yao.
 
Unataka akatafute jeshi huko aje kuwapa adabu waTanzania?
Kwa kuwa neno adabu lipo katika maisha yetu basi hata mimi nikikengeuka nishikishwe adabu kwa njia za kibinaadamu......

Wewe ukikengeuka ,usishikishwe adabu kibinaadamu ?!!

Mwenzetu una "immunity" kutoka mbinguni ?!!!

#Nchi Kwanza[emoji7]
 
Dah madalali washachukua chao wanaishi mbele huko. Hii nchi ipo siku kotawaka tuu.
 
Kwa kuwa neno adabu lipo katika maisha yetu basi hata mimi nikikengeuka nishikishwe adabu kwa njia za kibinaadamu......

Wewe ukikengeuka ,usishikishwe adabu kibinaadamu ?!!

Mwenzetu una "immunity" kutoka mbinguni ?!!!

#Nchi Kwanza[emoji7]
Mtu kama wewe napata shida sana kujibishana nawe, kwa sababu akili zako siyo timamu.
Pamoja na kuwa na hali hiyo, elewa tu, kwamba wakati wenu umefika ukingoni. Hadaa na ulaghai mwingi haviwezi kudumu kulaza akili za watu wasione uovu mnao wafanyia.
Lia vyovyote utakavyo humu, haitasaidia kitu.
 
Hili liweke pembeni. Nilitaka kukustua tu ujue upotoshaji unao jaribu kuufanya hapa.
Haya ni maswala yasiyo husiana.
Lengo langu ni kuwakumbusha Viongozi haswa waliolewa Madaraka kuwa waangalie Nchi zingine za Kiafrika Armed Rebellions huwa zianaanza hivi hivi.
 
Natumaini umenielewa vizuri. Inapohusu maswala ya aina hii ya kuwadhalilisha waTanzania, naomba sana usinihimize tena na hizo staha.
I want to express my self as freely as I can the way I feel.
 
Hayo mabango sio ya wafugaji wa Kimaasai hiyo ni kazi ya large format printing kijijini Ngorongoro itoke wapi?!, hii maana yake kuna nguvu fulani behind the scenes inayowachochea hawa wamasai na sio Wamasai wenyewe tuu peke yao, na large format printing cost money, hivyo kuna watu wana fund!, ukisikia kitu kinaitwa fuelling ndio huku!.
P
Kama Kuna Watu wanawafadhili Wamasai wa Ngorongoro ili wàweze kulinda, kutetea au Kupigania Haki zao za msingi basi ufadhili huo unapaswa kuungwa mkono, ni ufadhili wenye Nia njema. Aidha, ufadhili huo utakuwa una baraka za Mungu kwa sababu vitabu vyote vya Maandiko Matakatifu vya makundi yote ya Imani zilizopo hapa duniani vinasisitiza kuhusu kutenda haki. Kitendo cha kutoa Ufadhili wenye lengo la kutetea au kulinda Haki za Watu ni kufanya kazi ya Mungu.
 
Back
Top Bottom