Jana nilikuwa na binamu yangu kwenye party, yeye ni mlevi na mpenda starehe. Ni wale akitoka Ijumaa asubuhi kwenda kwenye ujasiriamali kwake anarudi Jumatatu usiku. Ile Ijumaa anaunga kazini hadi starehe, anaibuka asubuhi starehe anaenda kutafuta, hivyohivyo mpaka akirudi Jumatatu usiku ndio analala. Kwahiyo alikuwa anakaa mchafu na ananuka pombe.
Sasa jana nikashangaa mbona ametoka uzee, kanawiri, macho yamepungua wekundu na hajavimba uso. Kumbe ameoa sogea tuishi kaacha kulala viwanja na kunywa supu ya mapupu. Mke yuko strict hakuna kulala nje wala kurudi umelewa.
Binamu hadi jana tukazungumzia kilimo na viwanja, na kusafirisha mikoani. Akataja hela ambazo kabla hajawahi taja, na manunuzi ambayo hakuwa anafanya. Nikagundua tu hizi akili ni mchango wa mke wake.