soine
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 2,113
- 2,329
Ukisema Kenya wanataka Serengeti ife wajidanganya, survival ya baadhi ya wanyama ktl hifadhi ya serengeti inategemea Maasai Mara, Vivyo hivyo kwa Mara inategemea Serengeti....this is how ecosystem works.Taingia lini Kenya akawa Beberu?
Al Jazeera Africa Mashariki Ofisi zao zipo Kenya na Kenya ndo mwenye maslahi makubwa na Ngorongoro maana Ngorongoro ikifa kifuatacho ni kufa kwa Serengeti na zikifa hizi mbili basi Kenya kakamata Soko la Utalii Africa Mashariki...
Hivyo sidhani kama utatamani uue kitu kinachokufaidisha. Labda ungesema Kenya wanatamani wangepewa Mlima Kilimanjaro!!
Pia, kuipa hoja yako ungekuja na statistics kuwa Tanzania inapokea wageni kiasi gani hadi Kenya wawatamani.
Kwa taarifa yako Kenya inajulikana duniani naweza sema mara 30 zaidi ya Tanzania (najua hapa nitatukanwa). Ziko sababu nyingi ya Kenya kujulikana mbali na riadha na ushirika mzuri na hao muitao mababeru ambao waliitangaza enzi zile hunting tourism ikiwa ni mojawapo ya pride kwa wakwasi wa majuu.
Wamasai wana haki ya kujitetea kwa sababu ni ardhi tangu vizazi na vizazi. Leo tende na halua za OBC zinataka watu wawatoe ndugu zetu kuwa kafara kwa pretext ya uwekezaji.
Ubuntu daima, I strongly stand with Maasai