Wambura Mtani aondoka RFA baada ya miaka 22

Wambura Mtani aondoka RFA baada ya miaka 22

Ngoja tuweke kambi tujue Mr.Wambura anenda wapi kama kujiajiri tuwahi nafasi za kazi kwenye kituo chake
 
Mkuu naomba kuuliza Juma Baragaza na Kamukulu wamefariki lini Daaah!! Kweli dunia tunapita sikuwa na taarifa za Baragaza kuwa amefariki nina mda kidogo sijasikiliza Redio
Baragaza nilikuwa namkubali sana enzi hizo, na rfa ilikuwa ni moja kati ya redio zilizofanya makubwa sana enzi hizo mpaka hivi karibuni ilipokumbwa na ukata.

Watangazaji wengine waliokuwa wa moto sana ni, Rebecca Molesi, Fredrick Bundala na Felister Kwilujira hawa nao sijui wako wapi tu.
 
Samadu Hassan, mchambuzi bora kabisa wa habari za mbali. R.I.P
Samadu Hassan alikuwa na kipindi chake kinaitwa JUNGU KUU kila jumapili saa moja usiku, hapo unakuta na habari mbalimbalibza wiki zikiambatana uchambuzi.

Aiseeh RFA ilikuwa ya moto sana enzi hizo.
 
Nguli wa utangazaji kutoka kituo cha Radio Free Africa (RFA) Wambura Mtani ameondoka katika kituo hicho alicho hudumu kwa miaka 22.

Mtani ni mkongwe aliyekuwa amebaki kwenye Radio hiyo baada ya watangazaji wengine nguli kuondoka humo na wengine walifariki kama vile Jumaa Ahmed Baragaza (R.I.P) Zuberi Msabaha (R.I.P), Prince Baina Kamukulu (R.I.P), Fred Fidelis aka Fredwaa (R.I.P) ambaye baadae aliondoka.

Binafsi nitamkumbuka kwa mazuri yake hapo na akapambane kutafuta changamoto mpya.

Zuberi Msabaha alifariki?

Huyu si ndio yule mtangazaji alikuwa kama anaongea Kilingala akitafsiri nyimbo za Kicongo?

Hii redio sijaisikiliza siku nyingi sana...
 
Amelipwaaa anachodai ? Maana boss wake ni zulumati mkubwa sana Africa.....atadai hadi atastaafu hajalipwa.....Hujawahi kusikia jamaa ana kesi kama zote.....halipiii akishinswa amesha declare kufilisila......halipi chochore daaa fiallo tapeliii....mkubwaa sanaa.....
Diallo ni mpuuzi sana , yaani hapa kweli ndio unaamini elimu ni muhimu
Yule mzee kichwa maji elimu zero we ona hata uendeshaji wa vile vyombo vya habari ,ni as if anaendesha vijiwe vya kahawa
Illiteracy ni shida sana
Hivi vyombo vya habari kwa jinsi alivyokuwa hana washindani enzi zile mpaka leo angekuwa na watu wanaojua kuongoza na kusimamia hiyo kitu kwa weledi na ubunifu unaoendana na mabadiliko ya kiteknolojia asingekuwa na mpinzani Bongo hii
 
Hii ndo radio nilikuwa naijua, kipindi hicho nilikuwa najua ratiba ya vipindi vyote, watangazaji wote kwa majina na sauti zao

Akianza kuongea tu najua huyo ni sauti ya fulani,

Sasa sijaisikiliza tangu 2012 zaidi ya miaka 10.

Nashangaa wadau wanasema wakina Fredy Waa(sindano 5 za moto), Samadu Hassan wamefariki aisee mda unatembea sana

Baruani(saiv namuona Azam)

Ivona naye Azam

Joyce Mwakalinga naye Azam

Rebecca Molesi sijui hata yuko wapi

Rahabu Fredy kuna siku nilisikia sauti yake Azam sijui yuko ama nilichanganya!

Wambura Mtani naye ndo hivo amesepa,

Kuna mwingine alikuwa anaitwa mtoto wa mama sabuni jina simkumbuki,

Hivi kile kipindi cha duniani wiki hii bado kipo? Nilikuwa nakipenda sana bora nikose sitosahau lakini kile hapana.
 
Samadu Hassan alikuwa na kipindi chake kinaitwa JUNGU KUU kila jumapili saa moja usiku, hapo unakuta na habari mbalimbalibza wiki zikiambatana uchambuzi.

Aiseeh RFA ilikuwa ya moto sana enzi hizo.
Anga za kimataifa
 
Hii ndo radio nilikuwa naijua, kipindi hicho nilikuwa najua ratiba ya vipindi vyote, watangazaji wote kwa majina na sauti zao

Akianza kuongea tu najua huyo ni sauti ya fulani,

Sasa sijaisikiliza tangu 2012 zaidi ya miaka 10.

Nashangaa wadau wanasema wakina Fredy Waa(sindano 5 za moto), Samadu Hassan wamefariki aisee mda unatembea sana

Baruani(saiv namuona Azam)

Ivona naye Azam

Joyce Mwakalinga naye Azam

Rebecca Molesi sijui hata yuko wapi

Rahabu Fredy kuna siku nilisikia sauti yake Azam sijui yuko ama nilichanganya!

Wambura Mtani naye ndo hivo amesepa,

Kuna mwingine alikuwa anaitwa mtoto mama sabuni jina simkumbuki,

Hivi kile kipindi cha duniani wiki hii bado kipo? Nalikuwa nakipenda sana bora nikose sitosahau lakini kile hapana.
Rahabu yupo Azam hukuchanganya, mtoto wa mama sabuni ni Glory Robinson alikuwa anatangaza RFA Bonanza sehemu ya pili. Kipindi chake kilikuwa na instrument ya music of the sun.
 
Ukisikiliza wanaojiita watangazaji wa leo hovyo kabisa hivyo kuondoka kwa mtu kama huyu pale RFA ni pigo
 
Hivi Rahabu fungo bado yupo wa kipindi Cha matukio.!!??
 
Daaah!! Enzi kweli zimepita imebidi niingie Youtube nimekuta watangazaji wengi wa Rfa wamevuta aisee na wengi wamehama,

Mimi hiki ndio kilikuwa kituo changu cha redio ninachosikiliza kuanzia asubuhi nikiamka

1.Ilikuwa inaanza 12 asubuhi amka na BBC hadi 12:30 asubuhi inafatia Magazetini asubuhi unakutana na Agbert Mkoko,Tom Chilala (sijui wako wapi kwa sasa hawa) na Ahmed Ally huyu wa simba saivi

2.Saa moja kamili inafata Matukio na Rebecca Molesi au Rahabu Fredy hadi saa moja na Dkk 20 inaanza michezo na Steve moyo Mchongi,Deokaji Makomba au Baruan Muhuza

3.Mbili kamili Mukhtasari wa habari na Rebeca molesi halafu kinafata Sindano tano kali za moto na Freduwaa

4.Saba kamili Show time na akina Glory Robinson toto la mama sabuni na wenzake saa kumi anaingia Baragaza na Mambo mambo

Daaah Time flies tuishi tu wakuu[emoji22][emoji22][emoji22][emoji24][emoji24]
 
dah RFA siku hizi imekua local sana!
zaman hii redio ilikua bab kubwa kuliko redio yoyote hapa nchini........

steve moyo aliendaGa wapi?
Mkuu RFA haijaizidi Kiss Fm kwa ulocal... Yaani kiss fm imekua mpaka na vipindi vile vya umbea kama vya kina mwijaku na baba levo. Enzi zile The Morning Kiss ya John Karani na Irene Tilya.. nimeisikiliza majuzi hapa nikasikitika sana
 
Back
Top Bottom