Wambura Mtani aondoka RFA baada ya miaka 22

Wambura Mtani aondoka RFA baada ya miaka 22

Daaah!! Enzi kweli zimepita imebidi niingie Youtube nimekuta watangazaji wengi wa Rfa wamevuta aisee na wengi wamehama,

Mimi hiki ndio kilikuwa kituo changu cha redio ninachosikiliza kuanzia asubuhi nikiamka

1.Ilikuwa inaanza 12 asubuhi amka na BBC hadi 12:30 asubuhi inafatia Magazetini asubuhi unakutana na Agbert Mkoko,Tom Chilala (sijui wako wapi kwa sasa hawa) na Ahmed Ally huyu wa simba saivi

2.Saa moja kamili inafata Matukio na Rebecca Molesi au Rahabu Fredy hadi saa moja na Dkk 20 inaanza michezo na Steve moyo Mchongi,Deokaji Makomba au Baruan Muhuza

3.Mbili kamili Mukhtasari wa habari na Rebeca molesi halafu kinafata Sindano tano kali za moto na Freduwaa

4.Saba kamili Show time na akina Glory Robinson toto la mama sabuni na wenzake saa kumi anaingia Baragaza na Mambo mambo

Daaah Time flies tuishi tu wakuu[emoji22][emoji22][emoji22][emoji24][emoji24]
Umesahau R.F.A bonanza na anko Sam a.k.a the grandpa kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa sita mchana
 
Mkuu RFA haijaizidi Kiss Fm kwa ulocal... Yaani kiss fm imekua mpaka na vipindi vile vya umbea kama vya kina mwijaku na baba levo. Enzi zile The Morning Kiss ya John Karani na Irene Tilya.. nimeisikiliza majuzi hapa nikasikitika sana
My name is Joakim mwakarugulu this is kiss fm sauti moja nzito sana aisee R.I.P Joakim
 
Fredwaa kumbe kashafariki nilimsikia Clouds kipndi kile cha asubuhi na kina Babra..

Dah maisha haya...hebu mkuu kama kuna uzi ulianzishwa wa Fredwaa kuondoka naomba ni tag niupitie..Maisha haya.
 
Huyo Tom Chilala sijui atakuwa wapi siku hizi, ukiangalia top cream ya wanahabari waliopo nchini kwasasa ni wengi sana wamepita hapo RFA.

Kipindi ambacho nilikuwa nakipenda sana na nilikiwa sikikosi, ni kile cha jioni kimaitwa MAMBOMAMBO[emoji91].
Naitwa willy Obare kutoka musoma

Willy obare naaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam 😂😂😂
 
Fredrick Bundala alihamia KAHAMA fm, ila baadae alirudi tena RFA miaka ya 2016. Kwasasa sijui yuko wapi huyo jamaa. Alivyorudi mara mojamoja alikuwa anashika kipindi cha Mambomambo.
Skywalker mbona yupo ingia Instagram, mtafute skywalker mzee wa simulizi na sauti yupo anajitafuta
 
Nakumbuka tu watuma salami enzi hizo utasikia

Dereva tax marufu mbeya mafiat charse mbonge
Muuza vioo marufu mbeya bony mbamba
Mama Heren wa forest mbeya
Lawena nsonda baba mzazi wa makongorosi chunya
Willy obare wa musoma Tanzania
Checso mzee wa matunda
Aisee kweli time flies
 
dah RFA siku hizi imekua local sana!
zaman hii redio ilikua bab kubwa kuliko redio yoyote hapa nchini........

steve moyo aliendaGa wapi?
Steve Moyo Mchonge. Dah nimemkumbuka sana.

Naskia kuna redio local Iringa anafanya kazi.

Nikumbushe, hivi alikuwa anaendesha kipindi gani?
 
My name is Joakim mwakarugulu this is kiss fm sauti moja nzito sana aisee R.I.P Joakim
Mwamba alikua anaitwa Joakim Mungaligulu aka JML, alikuwa ni Mzambia. Alivyotoka Kiss alikwenda Iringa miaka ya 2009-2010 akawa anatangaza local radio inaitwa HOT FM (ilikufa kitambo) ikiwa ni pacha wa EBONY FM (Hii Ebony ipo mpaka sasa). Walimzingua akasepa Dar na ndipo tukapata habari kuwa ametutoka duniani 2013

Nimehang nae sana Iringa, alikua mwana sana.
 
Nakumbuka tu watuma salami enzi hizo utasikia

Dereva tax marufu mbeya mafiat charse mbonge
Muuza vioo marufu mbeya bony mbamba
Mama Heren wa forest mbeya
Lawena nsonda baba mzazi wa makongorosi chunya
Willy obare wa musoma Tanzania
Checso mzee wa matunda
Aisee kweli time flies
Unamsahau vipi King majuto wa Geita sokoni?

Huyo Willy Obare daah😁
 
Nguli wa utangazaji kutoka kituo cha Radio Free Africa (RFA) Wambura Mtani ameondoka katika kituo hicho alicho hudumu kwa miaka 22.

Mtani ni mkongwe aliyekuwa amebaki kwenye Radio hiyo baada ya watangazaji wengine nguli kuondoka humo na wengine walifariki kama vile Jumaa Ahmed Baragaza (R.I.P) Zuberi Msabaha (R.I.P), Prince Baina Kamukulu (R.I.P), Fred Fidelis aka Fredwaa (R.I.P) ambaye baadae aliondoka.

Binafsi nitamkumbuka kwa mazuri yake hapo na akapambane kutafuta changamoto mpya.
Wapenzi wa RFA Jiburudisheni na kionjo hiki maridhawa

View: https://youtu.be/KNubhJSc69g?si=GOSPNHbIbRwVhdnm
 
Steve Moyo Mchonge. Dah nimemkumbuka sana.

Naskia kuna redio local Iringa anafanya kazi.

Nikumbushe, hivi alikuwa anaendesha kipindi gani?
mimi nilikua napenda kipindi cha michezo so huko ndiko nilikua namsikiliza sana,.........
sema ile redio diallo ilimshinda kitambo
 
Nguli wa utangazaji kutoka kituo cha Radio Free Africa (RFA) Wambura Mtani ameondoka katika kituo hicho alicho hudumu kwa miaka 22.

Mtani ni mkongwe aliyekuwa amebaki kwenye Radio hiyo baada ya watangazaji wengine nguli kuondoka humo na wengine walifariki kama vile Jumaa Ahmed Baragaza (R.I.P) Zuberi Msabaha (R.I.P), Prince Baina Kamukulu (R.I.P), Fred Fidelis aka Fredwaa (R.I.P) ambaye baadae aliondoka.

Binafsi nitamkumbuka kwa mazuri yake hapo na akapambane kutafuta changamoto mpya.

Aise ahmed baragaza nae alifariki! إنا لله وإنا إليه راجعون

Pia nilikua sijui msabaha, kamukulu nao wamefariki, إنا لله وإنا إليه راجعون

RFA nilikua naikubali, for me ndio ilikua the best radio in East Afrika, nilikua nnaifuatilia.
 
Back
Top Bottom