NATO wanachanganyikiwa: Kila wakipeleka silaha wanayoamini kuwa ni game changer (itabadili matokeo), baada ya muda si mfupi utasikia kimyaaa!!! Sifa kede kede zilizokuwa zinatolewa kusifia silaha hizo hazisikiki tena!! HIMARS-Zilipopelekwa Ukraine kwa sifa kedekede wakadhani sasa urusi imekwisha! Zimeishia kuwa zinadunguliwa sana kwa sasa. Zilisikika sana mwanzoni tu na sasa mwarobaini wake ushapatikana.
PATRIOT- Ndiyo hiyo ishadunguliwa tayari! mwali anarudi kwao kukarabatiwa baada ya kukumbana na kipigo!!
STORM SHADOW CRUISE MISSILES- Hizi ndo hazijachukua round, ziliingia kwa kishindo zikatumika kushambulia ndani ya urusi, lakini sasa hazisikiki tena, zinadunguliwa kama kawa!!
Kwa sasa UK wanasema watapeleka ndege za kivita F-16. Urusi inasema zileteni kwani hiyo ni chakula cha S-400.