Wamiliki wa lodge kuweni serious

Wamiliki wa lodge kuweni serious

Sometimes mtu anasafiri analazimika kuchukua chumba lodge Kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukaribu wa anapokwenda mfano kikazi mtu atachukua lodge karibu na ofisi, au ukumbi wa mikutano na kadhalika. Sometimes kwa sababu ya lodge zingine kuwa zimejaa n.k..

Lakini sasa unaona lodge nzuri Kwa nje na hata ndani Kwa macho unaona iko Sawa, unalipia ulale unashangaa na unayo kutana nayo.

1. Feni inapiga kelele.
2. Bomba bovu maji yanatiririka bafuni.
3. Vitasa vibovu.
4. Mlango wa bafuni haufungi.
5. Taa bafuni haiwaki
6. Kitanda kinatoa milio
7. Mto ngumu Sana au mlaini Sana..
8. Feni haipungui wala kuongezeka Ama uwashe au uzime.
9. AC inapiga kelele
10. Tiles bafuni zina kutu.
11. Wahudumu Wana makelele.

Mradi matatizo ni mengi ambayo mtu anaejali biashara yake ni rahisi kabisa kutatua.

Nashauri kama mtu unamiliki lodge au kuendesha uweke utaratibu wa kulala wewe mwenyewe kila chumba Kwa mda Fulani ukague ujirishishe na huduma unazotoa.

Kuna lodge chumba kimoja kina joto kuliko chumba kingine Nakadhalika.

Kuweni serious, lodge ni sehemu ya mteja kulala comfortable sio kuwaza wateja wote wanaenda kwa ngono tu na kuondoka.
haya mimi yamenikuta sana
 
tatizo mnalala lodge za kupigia short time.... unakuta room watu wanaingia kupigana mashine kila baada ya masaa mawili sasa huo usafi utakua observed vipi?
 
16. Vyoo vya kukaa vichafu
17. Kondom hamna
18. Mashuka hayafuliwi hata siku tatu
19. Sabuni ya kuogea hamna
20. Uvundo kama wote vyumbani
21. Maji hakuna
Bro ili tatizo lako binafsi .... unaendaje guest ya 5k - 7k usitegemee haya??
 
Bora Dar.
Dodoma pana hotel mbaya sijawahi ona toka dunia imeumbwa
😀😀Hoteli gani Dodoma hizo mbaya ebu tutajie kama ni St Gaspar Hotel,Morena Hotel,NAM Hotel,Bestern Western City Hotel,Dodoma Hotel,African Dreams,Dear Mama Hotel,Golden Crown Hotel,Nashera Hotel au zipi😀😀😀

Rudi shule kama huwezi kujua tofauti ya guest house,lodge,motel,rest house,inn na hotel
 
Siku moja Moshi mjini mitaa ya Majengo nilichukua room kwenye lodge moja, 20k. Nilipoingia tu nikafunga mlango wa room kwa funguo, nikavua nguo direct kuoga bafuni. Huko bafuni nililazimika kurudishia mlango maana bafu ni dogo sana. Ile nafunga mlango nikasikia kitu kinaanguka upande wa pili wa mlango (upande wa chumbani). Sikujali nikaendelea kuoga.

Nimemaliza kuoga nafungua mlango haufunguki. Kumbe handle ya kitasa upande wa nje na kile kijichuma kinaunganisha handles na kitasa ndio vinedondoka.

Niliita wahudumu kwa nguvu sana ila wasisikie mpaka koo likauma na matusi yote hapo nimeshamaliza, na hakuna hata mteja mwingine room jirani anisikie awaambie. Wamekuja baada ya nusu saa hivi ila hawawezi kuingia chumbani kwangu kwani nimefunga. Funguo za akiba hawana anazo boss mwenye guest house. Boss amepigiwa yupo mbali, shambani. Alikuja baada ya kama 3hrs hivi. Muda wote huo nipo chooni tu.

Walipofungua nikatoka. Jicho nililowakata wakaelewa namaanisha nini. Wakanirudishia hela yangu bila kusema chochote nikaondoka kutafuta lodge nyingine.
Ukotiwa lock up kwanza[emoji23][emoji23]
 
Maana ni tarehe uliyoingia na tarehe unayotakiwa toka, ila wengi huwa hawaandiki mtu anafika hotel saa 8 usiku eti saa 4 atoke
Nimefanya sana hivi kwa mwanza kikubwa ni kusema kabla hujalipa ili akikubali basi unatulia mazima
Nilikuwa nafika mwanza saa 7 na by time hadi saa 8 au tisa nasogea kilatira nachukua chumba kwa makubaliano ya kuondoka kesho nyingine
Yule dada alinizoea hadi kimasihara ikapitia humo humo.
 
Sometimes mtu anasafiri analazimika kuchukua chumba lodge Kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukaribu wa anapokwenda mfano kikazi mtu atachukua lodge karibu na ofisi, au ukumbi wa mikutano na kadhalika. Sometimes kwa sababu ya lodge zingine kuwa zimejaa n.k..

Lakini sasa unaona lodge nzuri Kwa nje na hata ndani Kwa macho unaona iko Sawa, unalipia ulale unashangaa na unayo kutana nayo.

1. Feni inapiga kelele.
2. Bomba bovu maji yanatiririka bafuni.
3. Vitasa vibovu.
4. Mlango wa bafuni haufungi.
5. Taa bafuni haiwaki
6. Kitanda kinatoa milio
7. Mto ngumu Sana au mlaini Sana..
8. Feni haipungui wala kuongezeka Ama uwashe au uzime.
9. AC inapiga kelele
10. Tiles bafuni zina kutu.
11. Wahudumu Wana makelele.

Mradi matatizo ni mengi ambayo mtu anaejali biashara yake ni rahisi kabisa kutatua.

Nashauri kama mtu unamiliki lodge au kuendesha uweke utaratibu wa kulala wewe mwenyewe kila chumba Kwa mda Fulani ukague ujirishishe na huduma unazotoa.

Kuna lodge chumba kimoja kina joto kuliko chumba kingine Nakadhalika.

Kuweni serious, lodge ni sehemu ya mteja kulala comfortable sio kuwaza wateja wote wanaenda kwa ngono tu na kuondoka.
Naongeza namba 12.Unaoga maji hayatoki kwenye kishimo cha kutolea maji machafu,unaanza kutembea kwa kuchuchumia...
 
Hiki kiingereza tukiache kando tumalize huu mjadala kwanza.
Ulisoma St. Kayumba mzee sio kosa lako na sample ya watu kama ninyi ndio mnaolipwa hela nzuri ila kutokana na tamaa zenu mnaenda kutafuta lodges za bei nafuu kuliko bajeti mliotengewa...

Tafsiri ya hicho kingereza ni hii...
Shida ni wapi tunaulizia.. je tunaendana na hali na tulilipwa nini kwa Malazi na makazi.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Siku moja Moshi mjini mitaa ya Majengo nilichukua room kwenye lodge moja, 20k. Nilipoingia tu nikafunga mlango wa room kwa funguo, nikavua nguo direct kuoga bafuni. Huko bafuni nililazimika kurudishia mlango maana bafu ni dogo sana. Ile nafunga mlango nikasikia kitu kinaanguka upande wa pili wa mlango (upande wa chumbani). Sikujali nikaendelea kuoga.

Nimemaliza kuoga nafungua mlango haufunguki. Kumbe handle ya kitasa upande wa nje na kile kijichuma kinaunganisha handles na kitasa ndio vinedondoka.

Niliita wahudumu kwa nguvu sana ila wasisikie mpaka koo likauma na matusi yote hapo nimeshamaliza, na hakuna hata mteja mwingine room jirani anisikie awaambie. Wamekuja baada ya nusu saa hivi ila hawawezi kuingia chumbani kwangu kwani nimefunga. Funguo za akiba hawana anazo boss mwenye guest house. Boss amepigiwa yupo mbali, shambani. Alikuja baada ya kama 3hrs hivi. Muda wote huo nipo chooni tu.

Walipofungua nikatoka. Jicho nililowakata wakaelewa namaanisha nini. Wakanirudishia hela yangu bila kusema chochote nikaondoka kutafuta lodge nyingine.
 
Kuna kipindi nilikua mwanza ikabidi nichukue chumba maeneo ya nyegezi kwa ajili ya kuwahi usafiri
Nikaenda hotel moja inaitwa "Passion hotel" ile hotel chumba nilichukua 35k ila cha ajabu maji yakawa hayatoki bafuni ikabidi nimfate mhudumu akaishia kunijibu kwamba kama hayatoki unachukua ndoo unaenda kuchota chini kwenye kisima unapump ukizingatia nilikua vyumba vya ghorofani
Mda huo huo nikamwambia rudisha pesa haraka kabla haijawa vurugu, ikabidi nichukue pesa niende lodge nyingine za karibu nilipata huduma nzuri sana zaidi ya hotel ile ya kijinga tena kwa bei ya kawaida ya 20k.
 
Back
Top Bottom