Wamiliki wa mabasi jiongezeni mpige pesa zaidi, kituo cha mabasi Mbezi Luis ni changamoto kwa abiria

Wamiliki wa mabasi jiongezeni mpige pesa zaidi, kituo cha mabasi Mbezi Luis ni changamoto kwa abiria

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Kusema kweli kwa sasa wateja wa mabasi ya mikoani kupitia njia ya Morogoro rd. Watapata tabu sana.

Kwanza naipongeza serikali kwa juhudi zake katika mradi huo lakini location si rafiki kwa wateja wote.

Unatokea Mbagala,Mbande, Kisewe, Vikindu, Kisemvule, Gongo la Mboto na Chanika n.k unaenda Moshi/Arusha saa 11:30 asubuhi inatakiwa uripoti kituoni safari saa 12 hujachelewa?

Ubungo alieibuni basi hatosahaulika kwani ilikua center kabisa ya Dar.

Ni muda sasa wamiliki wa mabasi kufungua matawi maeneo ya mbali (mf. Tajwa juu hapo) ili kuwasogezea huduma wateja bila hivyo TRC wanaweza kukimbiza sana soko la usafiri.

Kuna kampuni kama Ester,Tilisho wameamua kufuata abiria walipo. Kampuni hizi zinatoa basi moja moja kwenda Mbagala na Chamazi asubuhi na mapema. Njia hii imefanya kupata wateja wengi sana, sasa endeleeni kukariri biashara kama hamjashindwa.
 
Miaka flani niliwai kumuaga mzee wangu kwamba naenda mjini, na kisha akaniuliza swali la kizushi kwamba "kwani mjini yako ni wapi??"
Tena akasisitiza kwamba nimwambie "nikisema mjini namaanisha nini??"
Bilashaka wakubwa wamenielewa.
Asante
 
Basi tuu nakasirikaga nikiona Uzi wa ajab ajab kama huu

Hata hapo ubungo wapo watu waliokua wanatokea chanika,kisemvule, majohe walikua wanalala zile hotel unazoziona pale Ubungo and vice versa HIVYO JARIBU KUFIKIRI WAKATI MWENGINE

By the way Ubungo is the second terminal baada ya Mnazi mmoja Miaka hio
 
Dar ina watu 6M.

Kuna kampuni zinatoa bus 2 tu kwa siku.

Ukipeleka Mbagala, Gongo la Mboto, Tabata, Kigamboni nao watataka.

Hiyo inakuwa ni kubahatisha labda asilimia kubwa ya abiria wako wawe wanatoka hayo maeneo unapoanzishia bus lako.

Kama Tahmeed anavyoanzia Lumumba kwasababu wateja wake wengi wanatokea hiyo mitaa. Huwezi mwambia akaanzie Mbagala kwasababu wateja wa huko ni insignificant.
 
Miaka michache nyuma tulisema kwamba wanahamisha stendi kuu kutoka mnazi mmoja Hadi ubungo..!!
Hakika tulipaona mbali zaidi.
Sikuzile nakumbuka mwisho wa mji ilikua tanki bovu, bagamoyo road.
Na pia chanika road, mwisho wa mji palikua gongo la mboto mzambarauni baada ya makaburi.
Na morogogoro road, mji ulikomea kimara ndipo tulipaita porini sana.
Huku temeke njia ya kwenda chang'ombe veta, town iliishia pale muembe yanga.....
Enzi zile pantoni ilikua moja na, pale swala ndipo tulipaona porini kabisa...

Nataka kusema kwamba.....
Vijana mnatakiwa mtulize boli, na mji ukikua basi huduma zitawafuata...
 
Hayo mabasi uliyoyataja sio kama yawawafuata abiria huko bali ndiko huanzia safari zao asubuhi, ukiliwahi kabla halijaondoka utapanda!! Kwa mtu wa vikindu, mbagala saa 10,unatakiwa uwe ndani ya daladala, ili uwahi mbezi!!
Mantiki ni ile ile ya kufuata abiria.kwanini waanzie huko wkt kituo ni ubt!?
 
Hoja yako ina mashiko, kwanza sijawahi kuona mantiki ya Bus zote kuondoka saa 12 alfajiri. Iwekwe sheria Bus ziwe zinaondoka kwa intervals ya aidha nusu saa au saa moja. Yaani kuwe na ma Bus yanayoondoka Dar from saa 12 mpaka saa 5 asubuhi ili abiria wawe na choice kulingana na umuhimu wa safari yake na mahitaji mengine. Kwanza hii itapunguza ligi za kipuuzi huko barabarani.
 
Apo ijengwe barabara ya oja kwa moja km ile ya marambamawili iunganishe gmboto,mbgala, chanika na mbez itasaidia coz saivi watu wanazunguka sana
 
Back
Top Bottom