Wamiliki wa mabasi jiongezeni mpige pesa zaidi, kituo cha mabasi Mbezi Luis ni changamoto kwa abiria

Wamiliki wa mabasi jiongezeni mpige pesa zaidi, kituo cha mabasi Mbezi Luis ni changamoto kwa abiria

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Akichelewa bus ikamuacha shauri yake kitijeti chake cha elfu 30 kitakuwa kimeliwa
Tununue bus 300Million alaf we abiria wa elf 30 utupige mkwara? Utajiongeza tu mwenyewe na utafika tu stand la sivyo uwe na private car yako la sivyo wahi kapandie ofisin saa 03:30 alfajir kabla gar haijaenda stand
 
Hiyo sababu ya kuwa na wajanja au wamejenga sijui kila kitu ni uongo tu ingekuwa hivyo wangeijenga sinza au kinondoni.
Sema wameisogeza kule kwa sababu ndio uelekeo wa highway ya kwenda mikoa mingi ya Tanzania,hii ndio sababu kuu hakuna nyingine.
Maana yake wanapunguza msongamano wa magari makubwa mjini yaani mabus na malori ndio maana wakajenga bandari kavu pia kule maeneo ya mlandizi.
mimi mwenyewe ninampango wa kuhama kutoka huku G.mboto anagalu nitafute kiwanja maeneo ya mbezi, kibamba au kiluvya, maaana huo ndio mwelekeo wa kwenda kwetu huko mikoani.
naipongeza serikali kwa kuutanua mji maaana jiji lazima litanuke
 
Ni wazo zuri ila jiandae kuuziwa kiwanja juu ya mlima halafu kabla ya kujenga uanze kuchonga.
mimi mwenyewe ninampango wa kuhama kutoka huku G.mboto anagalu nitafute kiwanja maeneo ya mbezi, kibamba au kiluvya, maaana huo ndio mwelekeo wa kwenda kwetu huko mikoani.
naipongeza serikali kwa kuutanua mji maaana jiji lazima litanuke
 
Ungesema watu majirani waishio mbezi wakarabati nyumba zao na kuzigeuza kuwa gest ndo fulsa ninayoiona zaidi. Ni mawazo tuu.
 
Stand kuu lazma iwe nje ya mji ili kuupanua mji acha lawama
 
MI nafikiri waweke safari za usiku, mabasi mengine yasafiri usiku
Wakati umefika mabasi yaruhusiwe kuanza safari usiku.
Safari za usiku (kwa wanaokwenda bara) zitawapunguzia sana gharama.
Atatoka kwake kwa usafiri wa kawaida kwa gharama nafuu tofauti na sasa ambapo analazimika kukodi gari au kuhangaika sana.
Wanaokwenda Kigoma, Burundi, Rwanda, Bukoba nk warafika Kahama mchana ambapo wataendelea na safari.
Hivi sasa wanalazimika kulala Kahama ambapo hili linaongeza gharama kwa abiria.
Wanaokwenda Mwanza, Shinyanga, Mara na kwingineko watafika Mwanza mchana kisha kuendelea na safari zao badala ya kulala.
Ukifanya hesabu sawasawa utaona kuwa utaratibu wa kusafiri usiku utawapa nafuu abiria na wenye mabasi.
Nahisi pia itapunguza msongamano barabarani.
Vile vile kusafiri usiku kutaokoa muda wa usiku unaopotea bure kwa kulala (mfano Kahama) badala ya kusafiri.
Tumaini letu ni kwa Bwana.
 
sisi wa Chamazi, Chanika, Kigamboni tutapanda mabasi ya Saul, Kilimanjaro, newforce na mengine mengi ambayo centre zao ni shekilango.
 
Kwa nini bus zote 100 au 200 zitoke saa 12 asubuhi? Why???? Kwa nini mengine yasitoke saa moja, saa mbili, saa tatu, saa 4 au saa tano??
Unaenda mwanza utoke saa tano?
 
Mimi Dar nikija kwa sasa ntapotea kabisa ngoja nikaze huku huku alipo mkulu wa Nchi. Maana Enzi zetu tunakua huku kwetu kwa msuguri palikua zaidi ya porini. Kwenda kariakoo ni safari ndefu sana.
 
Hoja yako ina mashiko, kwanza sijawahi kuona mantiki ya Bus zote kuondoka saa 12 alfajiri. Iwekwe sheria Bus ziwe zinaondoka kwa intervals ya aidha nusu saa au saa moja. Yaani kuwe na ma Bus yanayoondoka Dar from saa 12 mpaka saa 5 asubuhi ili abiria wawe na choice kulingana na umuhimu wa safari yake na mahitaji mengine. Kwanza hii itapunguza ligi za kipuuzi huko barabarani.
we utakuwa sio msafiri, mbona basi zipo za muda wowote unaotaka wewe kusafiri, na pia inategemea unaenda mkoa gani, mfano mtu anaeenda mwanza, bukoba, uganda ni lazma iwe saa 12, mana wakitoka zaidi ya hapo watafika kesho yake au kesho kutwa lakii mikoa mingine ya karibu mabasi yapo ya mida tofauti tofauti
 
Kusema kweli kwa sasa wateja wa mabasi ya mikoani kupitia njia ya Morogoro rd. Watapata tabu sana.

Kwanza naipongeza serikali kwa juhudi zake katika mradi huo lakini location si rafiki kwa wateja wote.

Unatokea Mbagala,Mbande, Kisewe, Vikindu, Kisemvule, Gongo la Mboto na Chanika n.k unaenda Moshi/Arusha saa 11:30 asubuhi inatakiwa uripoti kituoni safari saa 12 hujachelewa?

Ubungo alieibuni basi hatosahaulika kwani ilikua center kabisa ya Dar.

Ni muda sasa wamiliki wa mabasi kufungua matawi maeneo ya mbali (mf. Tajwa juu hapo) ili kuwasogezea huduma wateja bila hivyo TRC wanaweza kukimbiza sana soko la usafiri.

Kuna kampuni kama Ester,Tilisho wameamua kufuata abiria walipo. Kampuni hizi zinatoa basi moja moja kwenda Mbagala na Chamazi asubuhi na mapema. Njia hii imefanya kupata wateja wengi sana, sasa endeleeni kukariri biashara kama hamjashindwa.
Kilimanjaro Truck Wanachukua abiria KIGAMBONI.
Nategemea sasa makampuni ya WAchagga kama Machame safari, MARUNGU COACH, DAR EXPRESSS, FRESH COACH, MANGORIKA, HATCI, CHAKITO, KIRUMO , ziweke vituo huko Kongowe, Kibada, Mikwambe, chanoka, Kongowe na kimbiji, watu ni wengi na watashangaa wenyewe na wapitie njia ya Bagamoyo
 
Hoja yako ina mashiko, kwanza sijawahi kuona mantiki ya Bus zote kuondoka saa 12 alfajiri. Iwekwe sheria Bus ziwe zinaondoka kwa intervals ya aidha nusu saa au saa moja. Yaani kuwe na ma Bus yanayoondoka Dar from saa 12 mpaka saa 5 asubuhi ili abiria wawe na choice kulingana na umuhimu wa safari yake na mahitaji mengine. Kwanza hii itapunguza ligi za kipuuzi huko barabarani.
Mbona aina interval isipokuwa sehemu zenye km nying zaidi!
 
Basi tuu nakasirikaga nikiona Uzi wa ajab ajab kama huu

Hata hapo ubungo wapo watu waliokua wanatokea chanika,kisemvule, majohe walikua wanalala zile hotel unazoziona pale Ubungo and vice versa HIVYO JARIBU KUFIKIRI WAKATI MWENGINE

By the way Ubungo is the second terminal baada ya Mnazi mmoja Miaka hio
Hapo mabasi ya moja kwa moja mpaka Ubungo, hakuna basi la mwendokasi moja kwa moja kwenda Mbezi hata daladala toka Mbagala.
 
Kwa nini watu wa Mbezi Beach, Tegeta, Bunju na sehemu zingine za mbali na Airport hawalalamiki kwamba Airport iko mbali?
Hawasemi mbali kwakua ndege zinaondoka muda unaochagua abiria kwa siku husika vp Mabasi, unaweza kuchagua muda unaotaka kuondoka mfano ya Mwanza Dar?
 
Back
Top Bottom