Papy ndombe
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 3,761
- 4,535
Buza mbezi usafiri upoMtoa mada utakuwa mkazi wa Buza bila shaka
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Buza mbezi usafiri upoMtoa mada utakuwa mkazi wa Buza bila shaka
Naifahamu, ya kupitia KIFURU, lakini hiyo haikupunguzii purukushani za kuwa asubuhi au gharama za kuwahi mabasi asubuhiKuna barabara inatokea mbezi kupitia kinyerezi Hadi gongolamboto
Mtundu huuita usalama uoga mpaka apatapo ajaliHzo sababu ni za kiuoga tu kwanini traffic wasiwepo na ni majukumu yao, nimesafiri usiku magari huenda tu taratibu, hii kusubiria tu mchana sio sahihi, kabisa
Asee jamaa nimekuelewa sana. Sikujuaga hizo sababu,kumbe ni hatari kiasi hicho, safari za 🌃 iachiwe treni tuMtundu huuita usalama uoga mpaka apatapo ajali
Mzaha mzaha huzaa kizaa zaa
Anyway Trafic hata wakilazimishwa wakeshe...unahisi usiku wataweza kugundua matatizo ya basi kirahisi?Anaweza kuona lile basi linalokuja halina site mirror au kioo cha mbele kimepasuka?
anaweza kupiga kitochi gari?picha za gari anaweza kupiga?
ishu ya mabasi kukimbia usiku kila mtu anajua...giza likianza kuingia tu madereva ndo kama huwa wanaanza kukanyagia..Huwezi kulinganisha mwendo wa usiku na mchana.
Dar-Moro ukiondoka saa 1 usiku unafika saa 3 au 4 kasoro ila ukiondoka saa 5 asubuhi unafika saa9 au 10 kasoro.Na nirahisi kupata ajali usiku kwasababu ya giza.
Na vipi kuhusu majambazi na kutopatikana kwa msaada usiku nao ni uoga?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ifikie siku ubunifu utumike Victoria bus terminal pale London ilijengwa miaka ya 1800 na kitu lakini mpaka Kesho kituo bado kinahudumia uingereza yote hasa mabasi ya National express.Mbezi nayo tutakuja kuona ni center itabidi wahamishe tena!
hua wanalala wale dadaz wa exotic,fursa ninayo iona ni kujenga hoteli za kisasa ktk maeneo hayo
Sahiv kariakoo dakika kumi tu ushafika, tena kutokea mbeziMimi Dar nikija kwa sasa ntapotea kabisa ngoja nikaze huku huku alipo mkulu wa Nchi. Maana Enzi zetu tunakua huku kwetu kwa msuguri palikua zaidi ya porini. Kwenda kariakoo ni safari ndefu sana.
Kwakupaa??Sahiv kariakoo dakika kumi tu ushafika, tena kutokea mbezi
...Na Kisutu..!Basi tuu nakasirikaga nikiona Uzi wa ajab ajab kama huu
Hata hapo ubungo wapo watu waliokua wanatokea chanika,kisemvule, majohe walikua wanalala zile hotel unazoziona pale Ubungo and vice versa HIVYO JARIBU KUFIKIRI WAKATI MWENGINE
By the way Ubungo is the second terminal baada ya Mnazi mmoja Miaka hio
Na hata Mbezi itabidi kituo kihamishiwe Kibaha au Bunju... Mji unakuwa sasa mkoa wa Pwani unaikabli Dar-es-salaam..Miaka michache nyuma tulisema kwamba wanahamisha stendi kuu kutoka mnazi mmoja Hadi ubungo..!!
Hakika tulipaona mbali zaidi.
Sikuzile nakumbuka mwisho wa mji ilikua tanki bovu, bagamoyo road.
Na pia chanika road, mwisho wa mji palikua gongo la mboto mzambarauni baada ya makaburi.
Na morogogoro road, mji ulikomea kimara ndipo tulipaita porini sana.
Huku temeke njia ya kwenda chang'ombe veta, town iliishia pale muembe yanga.....
Enzi zile pantoni ilikua moja na, pale swala ndipo tulipaona porini kabisa...
Nataka kusema kwamba.....
Vijana mnatakiwa mtulize boli, na mji ukikua basi huduma zitawafuata...
Watanzania bhana yaani kuwahi tu Usafiri tena kwa Siku moja wa Saa 11:30 Alfajiri ( Asubuhi ) huwezi ila angekuwa ni Mwanamke amekuahidi Penzi ( Mbunye ) muda huo huo wa Saa 11:30 nina uhakika hata kama unaishi Mbagala Kipati ungewahi tu kutoka huko hata Saa 7:00 Usiku ili uiwahi na ikiwezekana 'ungeikodia' hata Pikipiki / Bajaji au hata UBA. Tuacheni 'Unafiki' ukiwa na nia ya 'Kusafiri' kweli basi naamini utawahi tu.Kusema kweli kwa sasa wateja wa mabasi ya mikoani kupitia njia ya Morogoro rd. Watapata tabu sana.
Kwanza naipongeza serikali kwa juhudi zake katika mradi huo lakini location si rafiki kwa wateja wote.
Unatokea Mbagala,Mbande, Kisewe, Vikindu, Kisemvule, Gongo la Mboto na Chanika n.k unaenda Moshi/Arusha saa 11:30 asubuhi inatakiwa uripoti kituoni safari saa 12 hujachelewa?
Ubungo alieibuni basi hatosahaulika kwani ilikua center kabisa ya Dar.
Ni muda sasa wamiliki wa mabasi kufungua matawi maeneo ya mbali (mf. Tajwa juu hapo) ili kuwasogezea huduma wateja bila hivyo TRC wanaweza kukimbiza sana soko la usafiri.
Kuna kampuni kama Ester,Tilisho wameamua kufuata abiria walipo. Kampuni hizi zinatoa basi moja moja kwenda Mbagala na Chamazi asubuhi na mapema. Njia hii imefanya kupata wateja wengi sana, sasa endeleeni kukariri biashara kama hamjashindwa.
Kwenye hicho kituo wangeweka Guest ili hao wa Kisemvule walalie hapo stand siku moja kabla ya safari