Wamiliki wa mabasi jiongezeni mpige pesa zaidi, kituo cha mabasi Mbezi Luis ni changamoto kwa abiria

Wamiliki wa mabasi jiongezeni mpige pesa zaidi, kituo cha mabasi Mbezi Luis ni changamoto kwa abiria

Kwa nini bus zote 100 au 200 zitoke saa 12 asubuhi? Why???? Kwa nini mengine yasitoke saa moja, saa mbili, saa tatu, saa 4 au saa tano??
Wapi basi zote zinatoka sa 12 asubui. Mbona za 1,2,3,4 zipo. Hadi sa nane kuna gari zinaenda Moshi. Tanga kuna Tashriff hadi ya sa 11 jioni
 
Kiukweli Hoja ya mabasi kuondoka asubuhi kisa yanakwenda mbali ni hoja mfu... hivi faida ipo kwenye KM au kwenye majina Ya Siku?

Kama kuondoka mtu anatakiwa adamke saa 10 alfajiri, ugumu ni nini kwa mtu kufika aendapo saa 10 alfajiri kama hiyo?

Mwanza mbali ndio, lakini mabasi mengi yanayoondoka saa12 asubuhi kwenda Mwanza au Kuja Dar kutoka huko, mengi yao hayageuzi kesho yake.. sasa kinachohitajika kufika saa 6 usiku ni kipi Ikiwa gari halitahitajika kusafiri asubuhi yake?

Tukubali tukatae, huu utaratibu wakutokusafirisha abiria usiku ni Uzembe wa watu na ni kukwepa majukumu na wajibu wao. Lakini kusema mtu atatumia Siku mbiki si kweli, labda siku kwa maana ya majina aliondoka jumatatu kafika jumanne ila siku kama masaa, Hakuna kitakachobadilika.

Nikirudi kwa Uzi..
Safari ni Safari na Kuna wasafiri na Waendaji.
Kama we ni Msafiri kiukweli utaona changamoto ila kama ni muendaji lazima utazikabili changamoto zote ili mradi uweze kwenda uendako.!
 
sisi wa Chamazi, Chanika, Kigamboni tutapanda mabasi ya Saul, Kilimanjaro, newforce na mengine mengi ambayo centre zao ni shekilango.
Kuna Sauli inayoenda kaskazini? Ningekuwa mteja wao,naskia inasifiwa sana
 
Kwa nini watu wa Mbezi Beach, Tegeta, Bunju na sehemu zingine za mbali na Airport hawalalamiki kwamba Airport iko mbali?
kwasababu ndege haziwezi kuwafuata walipo, na pia wanaopanda ndege wote wana uwezo wa kukodi taksi, bodaboda na kuwahi.

Hivi wewe unakaa CHAMAZi, umekata MARANGU COACH ya saa 11 :45 alfajiri , upo na familia yani mpo 6 na unakwenda Marangu kilimanjaro kuhesabiwa, it means unatakiwa utoke NANE USIKU kuwahi Mbezi, na muda huo hupati daladala za moja kwa moja, inabidi kuunga na hupati daldala la kubeba familia nzima, wengine watabaki huko mizigo ukiilipia, in short ni shidaa
 
Nakazia hapa.
Mtoa mada amekurupuka na kutoa lawama kama za wauza nyanya sokoni.
Kwa kifupi hakuna mahali ambapo ni karibu na patamfurahisha kila mtu.
Lazima kuna baadhi watafurahia kwa ukaribu na wengine watapaona mbali.
Na kuhusu swala la sijui kuamka saa ngapi ndio uwahi mmiliki wa basi au serikali haliwahusu ukiogopa kuchelewa kwa umbali amka saa tisa.
Kwa mfano hata hapo ubungo ambapo unasema ni karibu ulishawahi kuwaza mtu anayekaa bagamoyo au kimbiji anafikaje hapo ubungo ili awahi safari yake?Jiongeze
Mim sijalalamika wala kukosoa ujengaji wa kituo hicho,elewa kwanza.
Nimesifia ila nimetoa ushauri kwa wamiliki wa mabasi wajiongeze ili kutanua wigo kibiashara na kiushindani.
Ushauri wangu sio sheria useme ni lazma ufatwe
 
Hakuna mmiliki wa bus atachoma mafuta yake akufuate wewe kimbiji.
Ukishindwa kusafiri ujue hauna safari ya umuhimu
 
hii ni fursa kwa wachawi kuanza kusafirisha abiria kwa ungo kuwahi stendi
 
Hoja yako ina mashiko, kwanza sijawahi kuona mantiki ya Bus zote kuondoka saa 12 alfajiri. Iwekwe sheria Bus ziwe zinaondoka kwa intervals ya aidha nusu saa au saa moja. Yaani kuwe na ma Bus yanayoondoka Dar from saa 12 mpaka saa 5 asubuhi ili abiria wawe na choice kulingana na umuhimu wa safari yake na mahitaji mengine. Kwanza hii itapunguza ligi za kipuuzi huko barabarani.
Kwani bus zote zinaondoka saa 12 mbona kuna bus zinaondoka hadi mchana,mi naona ziwekwe bus zinaondoka kuanzia saa 1/2 mbili usiku kuendelea
 
Hakuna mmiliki wa bus atachoma mafuta yake akufuate wewe kimbiji.
Ukishindwa kusafiri ujue hauna safari ya umuhimu
🤪🤪😂😂😂...mbona kina Tilisho wanafata watu Mbande huko,wao hawachomi mafuta?
 
Kusema kweli kwa sasa wateja wa mabasi ya mikoani kupitia njia ya Morogoro rd. Watapata tabu sana.

Kwanza naipongeza serikali kwa juhudi zake katika mradi huo lakini location si rafiki kwa wateja wote.

Unatokea Mbagala,Mbande, Kisewe, Vikindu, Kisemvule, Gongo la Mboto na Chanika n.k unaenda Moshi/Arusha saa 11:30 asubuhi inatakiwa uripoti kituoni safari saa 12 hujachelewa?

Ubungo alieibuni basi hatosahaulika kwani ilikua center kabisa ya Dar.

Ni muda sasa wamiliki wa mabasi kufungua matawi maeneo ya mbali (mf. Tajwa juu hapo) ili kuwasogezea huduma wateja bila hivyo TRC wanaweza kukimbiza sana soko la usafiri.

Kuna kampuni kama Ester,Tilisho wameamua kufuata abiria walipo. Kampuni hizi zinatoa basi moja moja kwenda Mbagala na Chamazi asubuhi na mapema. Njia hii imefanya kupata wateja wengi sana, sasa endeleeni kukariri biashara kama hamjashindwa.
Uanze kufuga jogoo linalowikaga ovyo ovyo pengine linaweza kukusaidia uamke saa 8 za usiku uwahi Mbezi
 
Wakati umefika mabasi yaruhusiwe kuanza safari usiku.
Safari za usiku (kwa wanaokwenda bara) zitawapunguzia sana gharama.
Atatoka kwake kwa usafiri wa kawaida kwa gharama nafuu tofauti na sasa ambapo analazimika kukodi gari au kuhangaika sana.
Wanaokwenda Kigoma, Burundi, Rwanda, Bukoba nk warafika Kahama mchana ambapo wataendelea na safari.
Hivi sasa wanalazimika kulala Kahama ambapo hili linaongeza gharama kwa abiria.
Wanaokwenda Mwanza, Shinyanga, Mara na kwingineko watafika Mwanza mchana kisha kuendelea na safari zao badala ya kulala.
Ukifanya hesabu sawasawa utaona kuwa utaratibu wa kusafiri usiku utawapa nafuu abiria na wenye mabasi.
Nahisi pia itapunguza msongamano barabarani.
Vile vile kusafiri usiku kutaokoa muda wa usiku unaopotea bure kwa kulala (mfano Kahama) badala ya kusafiri.
Tumaini letu ni kwa Bwana.
Mwenyewe napendekeza kusafiri usiku ni kuzuri imagine una issue yako imetokea saa kumi na tukio lako ni kesho, kuliko kupoteza siku heri kusafiri huo usiku, udamkie huko mapema uendako
 
Mwenyewe napendekeza kusafiri usiku ni kuzuri imagine una issue yako imetokea saa kumi na tukio lako ni kesho, kuliko kupoteza siku heri kusafiri huo usiku, udamkie huko mapema uendako
ishu ya kuzuia mabasi kusafiri usiku ni ya kiusalama zaidi.
Kuna wale majangiri wa kuweka magogo barabarani
Lakini pia hamna Traffic wa kukesha Usiku
Lakini Pia madereva watakuwa wanakimbiza mno mabasi na Usiku kwenye mwanga hafifu ni rahisi kupata ajali
Pia mkipata Shida ni ngumu kupata msaada saa nane za usiku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hzo sababu ni za kiuoga tu kwanini traffic wasiwepo na ni majukumu yao, nimesafiri usiku magari huenda tu taratibu, hii kusubiria tu mchana sio sahihi, kabisa
 
Kabisa.... Maana kutoka Chanika hadi ufike Ubungo saa 12 asubuhi, gharama yake inaweza ikawa sawa na nauli ya unakokwenda... Hata ukiamua kulala Mbezi ili uwahi badoo..!!!
Kuna barabara inatokea mbezi kupitia kinyerezi Hadi gongolamboto
 
Wanawake wengi hawana hela,wanawezaje kujilipia hizo mahari?
 
Kusema kweli kwa sasa wateja wa mabasi ya mikoani kupitia njia ya Morogoro rd. Watapata tabu sana.

Kwanza naipongeza serikali kwa juhudi zake katika mradi huo lakini location si rafiki kwa wateja wote.

Unatokea Mbagala,Mbande, Kisewe, Vikindu, Kisemvule, Gongo la Mboto na Chanika n.k unaenda Moshi/Arusha saa 11:30 asubuhi inatakiwa uripoti kituoni safari saa 12 hujachelewa?

Ubungo alieibuni basi hatosahaulika kwani ilikua center kabisa ya Dar.

Ni muda sasa wamiliki wa mabasi kufungua matawi maeneo ya mbali (mf. Tajwa juu hapo) ili kuwasogezea huduma wateja bila hivyo TRC wanaweza kukimbiza sana soko la usafiri.

Kuna kampuni kama Ester,Tilisho wameamua kufuata abiria walipo. Kampuni hizi zinatoa basi moja moja kwenda Mbagala na Chamazi asubuhi na mapema. Njia hii imefanya kupata wateja wengi sana, sasa endeleeni kukariri biashara kama hamjashindwa.
Mtoa mada utakuwa mkazi wa Buza bila shaka
 
Hata baada ya miaka kadhaa mbezi stand apatofaa itabidi kituo kihamie chalinze.
Muhimu ni kuboresha miundombinu hasa mabus ya mwendokasi
 
Back
Top Bottom