Wamiliki wa vyombo vya usafiri tujitahidi kuzingatia matengenezo ya vyombo tunavyovimiliki

Wamiliki wa vyombo vya usafiri tujitahidi kuzingatia matengenezo ya vyombo tunavyovimiliki

Hongera mkuu. Kama vipi hamia mkoani ukapige hyo kazi
mkoa gani wenye population kama Dar...? maana siku fichi rafiki yangu boda boda hapa mjini inalipa sana...ile asubuhi tu nina uhakika wa kuingiza 30k na jioni vile vile nikifanya hadi saa 6 usiku naweza kupata hadi 45k...

sema ndio hivyo changamoto ni nyingi sana...😭😭😭​
 
kuna mtu alikuwa nae kwenye gari ndie alie sema...maana walikuwa wanajadiliana cha kufanya....pembeni ya barabara kulikuwa na watu wanaendelea na shughuli zao...si unajua Sinza africa sana ile barabara inayoingia kuelekea TRA panavyokuwa.

hivyo akaona bora aigonge bajaji maana angeilekeza gari kando ya barabara angechinja watu...sijui kama wametulisha tango pori au lah...!​
Tango pori kwa sababu ni nadra sana gari ndogo kufeli break haswa automatic
 
Ndugu zangu jana nilipata Ajari na pikipiki yangu nikiwa na abiria wangu {pole sana boss lady hope unendelea vizuri} ajari hiyo niliipata pale Sinza africa sana...kuna gari ilipoteza break ikagonga bajaji, bajaji ikapoteza uelekeo nikajikuta nagongana nayo uso kwa uso.😭😭😭

View attachment 2840307

Ndugu zangu wamiliki wa vyombo vya usafiri tujitahidi kuzingatia matengenezo ya vyombo tunavyo vimiliki kwasababu kama hainiingii akilini kuwa kama gari ina service nzuri Iferi break. jana nilikuwa nakichungulia kifo hivi hivi.

lakini namshukuru Mungu naendelea vizuri nilichubuka tu kidogo japo abiria wangu aliumia nae kidogo😭😭😭

hii imenifanya niiogope sana kazi yangu ya boda boda jana nimeiogopa sana pikipiki na barabara uendeshaji wangu ni wakistaarabu sana ila ndio hivyo bado nasababishiwa ajari...!

hata hivyo nimekumbuka kuwa huu ni mwisho wa mwaka matukio ya ajari huwa ni mengi...hivyo ndugu yangu msomaji kama huna umuhimu wa kusafiri ni bora tu ukae nyumbani hadi mwaka uishe...!

jana mwenzenu nilikichungulia kifo​
Ajali si ajari
 
Pole sana mkuu, ajali za bodaboda zinafikirisha hasa kusudio langu la kuimiliki.
 
Back
Top Bottom