Wamiliki wengi wa majokofu/friji wanauelewa mdogo juu ya utendaji kazi wake

Wabongo bhana,
Mtoa mada amesema anatupa maarifa mepesi na uelewa wa kawaida kwa wanaotumia majokofu na viyoyozi ili tuelewe utendaji kazi wa hivyo vifaaa, pia mafundi wasitudanganye na kutuibiaa.

Sasa ndugu yangu hayo mambo ya valvu sijui nini fungua uzi wa mpya kwa ajili ua mafundi
 
Hii ni elimu huru wapo watakao hitaji kujua zaid kupitia uzi huu. Halaf hyo valve niliyoitaja hapo ni vile umeichukulia poa tu ila nayo ikizingua na ukikutana fundi wa hovyo ataweza kukumalizia hela zako bure.

Thanks in advance
 
Je naweza kutumia freezer kujiomgezea ubaridi ndani wakati wa joto? Yani unalifungulia tu unaacha lifanye kazi yake
Hapana, Hewa ya nje itakapoingia Kwa muda mrefu itadhoofiaha utendaji kazi, Kwahiyo badala ya Friji kutengeneza Baridi litatengeneza joto na litatumia Umeme mara 3 zaidi ya kawaida
 
Shukrani kwa elimu.
Kwangu gesi inaisha na ninajaza kila baada ya miezi 3 au 4, kama wewe ni fundi na upo Dar es salaam au sehemu za karibu, naomba namba yako.
 
Shukrani kwa elimu.
Kwangu gesi inaisha na ninajaza kila baada ya miezi 3 au 4,Kama wewe ni fundi na upo Dar es salaam au sehemu za karibu,naomba namba yako.
Pole sana kiongozi, bahati mbaya sipo huko kwa sasa halafu pia sifanyagi kazi za individual. Ila naweza kukusaidia kutambua leakage

Fanya hiv

Chukua maji weka kwenye ndoo kisha changanya na sabuni (napendekeza ya unga kwasabab ya povu).

Ukishachanganya hakikisha unapata povu jingi.
Pia tafuta sponji au kipande cha godoro.

Washa friji lako na hakikisha compresor inafanya kazi.

Baada ya kuwasha sasa unaweza kuanza kazi ya kuitafuta hiyo leakage

Unachukua lile povu kwa sponji halafu unalikamulia kwenye viungio vyote bila kusahau ile sehem unayoingizia gesi.

Ukishakamulia lile povu kama kuna leakage lazima itaonekana.

Kwa msaada zaid ingekua vema uniambie huwa unaona dalili zipi mpaka unamuita fundi akujazie gesi (mafundi wetu muda mwingne sio waaminifu).

Ref na chiller huwa zina matatizo mengi na mengine yanataka kufanana dalili hivyo ni venga ungefunguka kodogo nikuambie wapi ukaguse kwenye friji lako
 
Shukrani kwa elimu.
Naomba namba ya fundi aje kuziba kwangu,maana inaisha na kujaza kila baada ya miezi 3 au 4.
Pole sana kwa kuingia gharama za mara kwa mara. Nakutumia number ya mtaalamu ninayemuamini mimi. Ana nyenzo na weledi mkubwa tu. Natumai lazima utapata suluhisho.
 
Asante mtoa mada
Kuna mafundi baada ya kugundua kuwa kuna tundu kwenye pipe, wanashauri kununua pipe nyingine na kusuka upya.

Swali langu:
Hakuna njia tofauti ya kuziba ile pipe iliyokuja na jokofu, ukiacha hii ya kusuka upya na kuharibu muonekano wa ndani wa jokofu ?
 
Hata mimi kanichanganya sana pia nimeshangaa ameshindwaje hata kusoma hiyo picha aliyoiweka mwenyewe.
 
Mkuuu umejitahidi kufungua uzi lakini kuna baadhi ya maelezo nkusahihishe.. nikuhusu refrigerant circle..

Gas ya ac/fridge circle yake ina anzia kwenye compressor, then kwakua compressed gas inakua ya moto, so inabidi ipite kwenye condenser ili kuipoza gas , then inapita kwenye expansion valve au capillary au orifice tube (depends on system design) hapo gas u expand na ku drop temperature na ndipo baridi utokea, sasa gas ile ya baridi ndo inaenda jikusanya kwenye evaporator then ubaridiwa evaporator ndo unapoza compartment ya fridge na kupoza vitu vilivomo ndan ya fridge (so kama fridge ikiwa ni non frost itakua inatumia fan kusambaza ubaridi ulio kwenye evaporator, na kama ni frost basi utakuta pipe za evaporator zimo ndani ya compartment zinazunguka-visible pipea kwa ajili ya kutengeza baridi)... Then gas ikisha toka kwenye evaporator inarudi kwenye compressor kipitia low side pipe , then the circle continues endlessly... But ku-control temperature kuna kua na thermostat.

Kuhisiana na ujazaji wa gas ni kweli kabisa mafundi wengi hawafanyi vacum kutoa moisture na hewa ndani system, na pia hawapimi oil ya compressor vizur, na hawana vipimo vya kupima uwingi wa gasi, na hawatumii gaugesi matokeo yake wakijaza gas performance yake inakua na changamoto.hizi shida zipo hata kwa mafundi AC za magari...na ndo maana hata nikienda kufanya service ya ac ya gari yangu uwa naenda na vifaa vyangu mwenyewe...yaan manifold gauges, oil ya compressor, na condenser, original refrigerant, mzazi wa kupima gas..then namuelekeza fundi afanye vile namuelekeza..


Note; kama unaenda fanya marekebisho ya ac ya gari na gari iliua compressor kwa kuisaga, hiyo gari ili ipone inavotakiwa mi kubadilisha the entire system mpaka pipes..ukijifanya unabadili compressor na condenser alafu una flush evaporator na ac pipes basi ujue ndani ya muda mfuli ile compressor itakufa hata kama una compressor ya pump (fixed displacement compressor) au compressor ya kipumbu (lugha ya mafundi wetu bongo)
 
Fridge yako ni frost au non frost
 
Umeongea kitaalamu lakini unasahau kuwa hizo ni. Chemical reaction za specific elements
Pressure varies diirect proportional to temperature , freon inapokuwa compressed huzalisha joto, ndipo hapo hulazimika kupelekwa kwenye condenser ili ipunguzwe joto, ikitoka hapo ndipo inaenda kwenye expansion valve au evaporator ( ac) , kinachofanyika hapo sasa ndo kinyume cha compression, those freon molecules zinapoachwa huru huwa zina tabia ya kutoa baridi na ndo hasa huleta barafu.
 
Ndio sababu tunazisitiza elimu isiwe ya kukariri ili tupate wataalam wazuri , nimemsoma mtoa mada vizuri sana , anajua na kujitahidi , ila kuna vitu unaona kabisa kavimeza kama vilivyo , na hawezi tena kutoka nje ya hiyo knowledge cycle ,
Ubaridi kwenye freezer na fridge unaaznia kutoka kwenye expansion valve ,
 
Ahsante mkuu kwa kunisaidia maana mtoa mada alishaanza kuniona kirusi.

Mimi kila siku huwa nasema bongo tunachanganya sana kati ya experience na qualification.


Mtoa mada ana qualification ila hana experience ya kitu alichoanzishia uzi ndomaana nilivyo mrekebisha akaanza kuniletea uongo wake wa darasani as if sijui nilichomsahisha.

Siku akibahatika kufanya kazi kwenye plant lazima atakuja kufuta huu uzi wake
 
Naomba mtushauri na fridge nzuri ni lile linaloweka mabarafu au lisiloweka barafu?
 
Naomba mtushauri na fridge nzuri ni lile linaloweka mabarafu au lisiloweka barafu?
Inategemea na aina za kazi unazofanya, non frost ni nzuri na very efficient ila linataka kuwe na umeme wa uhakika ,
Yale ya frost ni ya kizamani na hayapo effiecient ila unaweza ukainjoi barafu hata kama umeme umekatika kwa muda
Kwa matumizi ya nyumbani non frost ipo poa ila kibiashara chukua tu yale ya kuweka barafu
 
Lawama zoote ni mfumo wa elimu unaotukuza pass marks na si uelewa ,
Watoto wapo busy kutafuta past papers na possible questions , unapataje experts kwa mtindo kama huo? Watu wanakariri na kufaulu imeisha hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…