Wamiliki wengi wa majokofu/friji wanauelewa mdogo juu ya utendaji kazi wake

Wamiliki wengi wa majokofu/friji wanauelewa mdogo juu ya utendaji kazi wake

Naomba mtushauri na fridge nzuri ni lile linaloweka mabarafu au lisiloweka barafu?
Friji kuweka mabarafu sio dalili nzuri mara nyingi inaashiria kuna upungufu wa freon

Siku nikipata muda nitaelezea kwann barafu inatokea na wakati freon imepungua.

Ukipata muda unaweza hata kugoogle low pressure na high pressure inatakiwa iwe na uwiano gani ili nikishusha nondo kusiwe na maswali mengi.
 
Nashukuru kwa pongezi kaka. Wakati naandika huu uzi niliwalenga watumiaji wa majokofu. Hivyo sikutaka kuwachosha sana na habari za kitaalamu.
Mkuu Buzitata kazi ya Thermostatic expansion valve ni kuibadili gesi kutoka maji maji na kuwa mvuke. Hii gesi ikiwa katika mfumo wa mvuke ina tabia ya kufyonza joto, hata liwe kidogo italifyonza. Yaani inatabia ya kuhitaji joto ikiwa kwenye mfumo wa mvuke ndani ya evaporator. Baada ya hapo ikipita kwenye compressor huwa imesharudia tena kwenye hali yake ya kimiminika. Na ikiwa kwenye hali ya kimiminika, gesi ya Freon huwa na tabia ya kutoa joto. Yaani inakuwa kinyume na wakati ikiwa kwenye hali ya mvuke. Inakuwa inafyonza au inahitaji zaidi ubaridi. Baada ya hapo inapita tena kwenye expansion valve, expansion valve inaigandamiza na kui-spray ndani ya evaporator kuwa hali ya mvuke na mzunguko unaendelea.
Jokofu hutumia kanuni ya kuondoa joto ili kupata ubaridi. Nikupe mfano wa giza na mwanga. Kwa asili dunia ni giza. Taa au jua likiwaka ndio hulizidi giza japokuwa wakati wote giza lipo. Kinachotokea ni kwamba mwanga unalizidi uwiano giza, basi giza halionekani.
Na kwa habari ya joto na baridi ni hivyo hivyo. Dunia yetu ni baridi isipokuwa msuguwano ndio husababisha joto na kuja kuiondoa baridi, japo baridi wakati wote ipo ila uwiano na joto au jotoridi huegemea upande wa joto hivyo tunahisi joto zaidi. Ama jotoridi ikiegemea upande wa baridi tunasema kuna baridi.
Kwahiyo jokofu hutumia kanuni ya kuliondoa joto, kinachobaki ni ubaridi. Hakuna kitu kinachotengeneza ubaridi kwenye jokofu.
Daah nilikuwa sijui kbs haya madini,umetisha Sana mkuu
 
Inategemea na aina za kazi unazofanya, non frost ni nzuri na very efficient ila linataka kuwe na umeme wa uhakika ,
Yale ya frost ni ya kizamani na hayapo effiecient ila unaweza ukainjoi barafu hata kama umeme umekatika kwa muda
Kwa matumizi ya nyumbani non frost ipo poa ila kibiashara chukua tu yale ya kuweka barafu
Shukrani
 
Friji kuweka mabarafu sio dalili nzuri mara nyingi inaashiria kuna upungufu wa freon

Siku nikipata muda nitaelezea kwann barafu inatokea na wakati freon imepungua.

Ukipata muda unaweza hata kugoogle low pressure na high pressure inatakiwa iwe na uwiano gani ili nikishusha nondo kusiwe na maswali mengi.
Utupe madini mkuu,Mda unatafutwa kaka
 
Hivi friji ukiliacha tu liwake kila siku kuna shida?

Ngoja waje wakujibu
Binafi hiki cha kwangu (boss) ile ndogo
Ina kama selector hivi
Ukiweka kwenye number2 hua inakuaunguluma afu inakata yenyewe
Na hua siizimi
Asubuh had jion hua inakula poins 9’10 yaan mfano nlikua na units 10.12 jion nakuta 10.10 hiv[emoji16]
 
[mention]buzitata [/mention]
Hakuna shida kwasabab friji lina timing yake. Muda gani liwake na muda gani lizime au muda gan lifanye defrost hiyo yote ni kazi ya thermostat.

Kwa kuongezea Solenoid valve huwa inafunguka kwa kusense low pressure line, so solenoid ikifunga compresor nayo huwa inajizima

Solenoid ikifunguka inaruhusu freon kuendelea na mzunguko wake na kuiruhusu kupita kwenye expansion valve ili kuzalisha ubaridi kwenye friji lako.
 
Friji kuweka mabarafu sio dalili nzuri mara nyingi inaashiria kuna upungufu wa freon

Siku nikipata muda nitaelezea kwann barafu inatokea na wakati freon imepungua.

Ukipata muda unaweza hata kugoogle low pressure na high pressure inatakiwa iwe na uwiano gani ili nikishusha nondo kusiwe na maswali mengi.
Naomba kkutofautiana kidogo nawe , kuna mifumo kadhaa katika utengenezaji wa fridges ,
Frost type na non frost , non frost ni zile kama fridge za coca cola , hIzi hazieki barafu kwenye kuta zake, na hata ugandishaji wake inaweka dry ice kwa bidhaa husika yani kama uliweka samaki kadhaa basi wataganda bila kushikana

Frost type ni mfumo wa zamani ambao barafu hutembea kwenye kuta za fridge ,hiI ndo husumbua sana na leakage na mafundi kwa kutumia shortcut huwa wana fanya external copper piping
Naomba kuwakilisha
 
Ni kweli ila na mimi naomba nikuongezee kaujizi kidogo ambako kapo ulimwenguni

Mostly now days tunasema kuna freezer na chiller. Hizo za coca cola ulizozitaja ni chiller na sio freezer

Hapo wanacheza na range tu muda gan iwake na muda gan izime.

Mara nyingi chiller hufanya kazi kwa muda mfupi kwasababu inakuwa rahisi kufikia temperature na nyingi zina range kuanzia 16c to 20c ila freezer nyingi huanzia 10c kushuka chini.
 
Mkuuu umejitahidi kufungua uzi lakini kuna baadhi ya maelezo nkusahihishe.. nikuhusu refrigerant circle..

Gas ya ac/fridge circle yake ina anzia kwenye compressor, then kwakua compressed gas inakua ya moto, so inabidi ipite kwenye condenser ili kuipoza gas , then inapita kwenye expansion valve au capillary au orifice tube (depends on system design) hapo gas u expand na ku drop temperature na ndipo baridi utokea, sasa gas ile ya baridi ndo inaenda jikusanya kwenye evaporator then ubaridiwa evaporator ndo unapoza compartment ya fridge na kupoza vitu vilivomo ndan ya fridge (so kama fridge ikiwa ni non frost itakua inatumia fan kusambaza ubaridi ulio kwenye evaporator, na kama ni frost basi utakuta pipe za evaporator zimo ndani ya compartment zinazunguka-visible pipea kwa ajili ya kutengeza baridi)... Then gas ikisha toka kwenye evaporator inarudi kwenye compressor kipitia low side pipe , then the circle continues endlessly... But ku-control temperature kuna kua na thermostat.

Kuhisiana na ujazaji wa gas ni kweli kabisa mafundi wengi hawafanyi vacum kutoa moisture na hewa ndani system, na pia hawapimi oil ya compressor vizur, na hawana vipimo vya kupima uwingi wa gasi, na hawatumii gaugesi matokeo yake wakijaza gas performance yake inakua na changamoto.hizi shida zipo hata kwa mafundi AC za magari...na ndo maana hata nikienda kufanya service ya ac ya gari yangu uwa naenda na vifaa vyangu mwenyewe...yaan manifold gauges, oil ya compressor, na condenser, original refrigerant, mzazi wa kupima gas..then namuelekeza fundi afanye vile namuelekeza..

Note; kama unaenda fanya marekebisho ya ac ya gari na gari iliua compressor kwa kuisaga, hiyo gari ili ipone inavotakiwa mi kubadilisha the entire system mpaka pipes..ukijifanya unabadili compressor na condenser alafu una flush evaporator na ac pipes basi ujue ndani ya muda mfuli ile compressor itakufa hata kama una compressor ya pump (fixed displacement compressor) au compressor ya kipumbu (lugha ya mafundi wetu bongo)
Tatizo humu JF kila mtu anajifanya anajua .

mtu katoa uzi simple watu tuelewe ila wanaojifanya kukosoa na kupost vitu vya google ni wengie sana.

KAMA HAURIDHIKI NA HILI FUNGUA UZI WAKO
 
Asanteni mafundi wote mlioingia kwenye huu uzi. Naona uzi umebadilika na umekuwa ni uzi wa mafundi, ni vizuri pia. Lakini ukiangalia kwa makini lengo la huu uzi, ilikuwa ni kuongea na watumiaji wa majokofu na siyo mafundi. Hata kichwa cha uzi kinajieleza hivyo. Kwenye maelezo yangu nimejaribu sana kupunguza mambo mengi ili nisimchoshe muhusika mwisho akose hamu ya kusoma mpaka mwisho na mimi kutimiza madhumuni ya uzi wangu.
Nadhani ni tatizo letu mafundi wetu wa Kitanzania, hatuna weledi wa kuwasiliana na wateja wetu. Watumiaji ambao hawana ujuzi mwingi wa vifaa, huhitaji vitu vichache na maneno machache ili waelewe. Nadhani hii yote ndiyo ikapelekea swala la masoko likawa ni weledi unaojetegemea. Nawashukuru sana mafundi na wataalamu wote waliochangia.
 
Tatizo humu JF kila mtu anajifanya anajua .

mtu katoa uzi simple watu tuelewe ila wanaojifanya kukosoa na kupost vitu vya google ni wengie sana.

KAMA HAURIDHIKI NA HILI FUNGUA UZI WAKO
Asante sana mkuu kwa kusaidia kuelewesha mafundi. Bado tuna mapungufu kwenye nyanja ya mawasiliano kati ya wataalamu wa vifaa na watumiaji wa vifaa. Mafundi waliochangia kwenye huu uzi ni mfano tosha.
 
Asanteni mafundi wote mlioingia kwenye huu uzi. Naona uzi umebadilika na umekuwa ni uzi wa mafundi, ni vizuri pia. Lakini ukiangalia kwa makini lengo la huu uzi, ilikuwa ni kuongea na watumiaji wa majokofu na siyo mafundi. Hata kichwa cha uzi kinajieleza hivyo. Kwenye maelezo yangu nimejaribu sana kupunguza mambo mengi ili nisimchoshe muhusika mwisho akose hamu ya kusoma mpaka mwisho na mimi kutimiza madhumuni ya uzi wangu.
Nadhani ni tatizo letu mafundi wetu wa Kitanzania, hatuna weledi wa kuwasiliana na wateja wetu. Watumiaji ambao hawana ujizi mwingi wa vifaa, huhitaji vitu vichache na maneno machache ili waelewe. Nadhani hii yote ndiyo ikapelekea swala la masoko likawa ni weledi unaojetegemea. Nawashukuru sana mafundi na wataalamu wote waliochangia.
Fact!.[emoji106]
 
Mkuu hii mada inahitaji utulivu kwasababu inatakiwa kutumia lugha nyepesi ambayo mtu wa kawaida ataweza kuielewa ili lengo la muanzisha uzi litimie
Angalizo
Ukitumia lugha nyepesi ni vigumu kuelezea mambo mengi. Na wataalamu wenzako watakukosoa. Lakini usijali, lengo lako titatimia kwa asilimia nyingi sana.
 
Asante sana mkuu kwa kusaidia kuelewesha mafundi. Bado tuna mapungufu kwenye nyanja ya mawasiliano kati ya wataalamu wa vifaa na watumiaji wa vifaa. Mafundi waliochangia kwenye huu uzi ni mfano tosha.
mkuu nilinunua friji used town, nkalitumia kwa miezi mi3 likawa haliwaki kabsa just from nowhere

wiki iliyo pita nilimwiita Fundi ,akasema tatizo ni filter(kwa mujibu wa maelezo yake).
Akaendelea kwa kusema kuwa endapo atafungua hicho ki-filter na kukibadilisha atajaza gesi upya, na akadai ataweka oil( hapa hata sijui kazi ya oil).

Hivyo alibadilisha ( filter), akajaza gesi ,friji likawaka.
but kuna muda friji linajizima na kujiwasha.
Je? ndo mfumo wa friji au kuna kitu hakipo sawa

naweka picha ya hicho kifilter

Msaada mkuu.
Screenshot_20220706-074652_Google.jpg
 
Msaada mkuu.View attachment 2282216
Pole mkuu kwa kadhia za jokofu lako. Kuzima na kuwaka kwa jokofu ni utendaji wa kawaida. Pale jotoridi linapofikia kiwango ulichopimia, basi jokofu litazima. Na pale jotoridi litakapo shuka mpaka chini ya kiwango ulichopimia, basi jokofu lako litawaka na kuanza tena kupandisha au kuongeza ubaridi. Labda kama huko kuzima na kuwaka kunafanya jokofu lako lisipoze kama matarajio yako ama uwezo wake.
 
Ngoja waje wakujibu
Binafi hiki cha kwangu (boss) ile ndogo
Ina kama selector hivi
Ukiweka kwenye number2 hua inakuaunguluma afu inakata yenyewe
Na hua siizimi
Asubuh had jion hua inakula poins 9’10 yaan mfano nlikua na units 10.12 jion nakuta 10.10 hiv[emoji16]
Naomba kujua Zaidi kuhusu hizi number. Mimi Nina Pinetech ndogo Ina namba 1-7 ila sijui maama yake
 
Hivi friji ukiliacha tu liwake kila siku kuna shida?
Unless iwe ni hizi za mtumba ambazo zime njungwq jungwa na thermostat au timer haifanyi kazi...

Ipo hizi any refrigeration system ina kitu kinaitwa thermostat... Thermostat ina monitor temperature ya evaporator ambapo ndipo baridi utokea.. sasa kwenye fridge kuna knob ya kuchagua temperature unayotaka compartment yako iwe nayo.. mfano unataka compartment ya freezer iwe na temperature ya 3°c.. maana yake uta set ile thermostat to that temperature.. so compressor itafanya kazi mpaka ile temperature ifikiwe.. then ikifikiwa compressor itazima yenyewe.. then joto likipanda mfano to 4°c compressor itawaka tena ku maintain ile temperature..

Sasa hapa kwenye fridge kuna frost na non frost...

Sasa kwa fridge za non frost huwa zinakua na evaporator ambayo inakua ndani then kunakua na feni inayopuliza ule ubaridi wa evaporator kuja vitu vilivomo ndani ya fridge kuvigandisha.. sasa changamoto ya hapa ni kwamba kuna muda hii fridge hujaa barafu so kutoa hii changamoto fridge huwa zinakua na heater na timer, na sensors ya kuzuia ku trigger heater iwake. So timer inakua na circle ya kuwasha Heater ili kuyeyusha barafu inayokua imejaa kwenye evaporator ili evaporator isi restrict airflow, lakini pia mfano kipindi cha baridi kama hivi sasa kwakua joto si kubwa fridge huwai kutengeneza barafu kwenye evaporator kabla ya circle ya timer kuanza kazi, so hapa ile sensor ya ku ditect frost kwenye evaporator coil huzimisha compressor na kuwasha Heater ili kuyesha ile barafu... So hivo ndivo fridge hufanya kazi (but hizi ni kwa non frost fridges) kwa frost fridges (nyingi ni za kizamani) kidogo working principals zinautofauti kidogo hasa upande wa evaporator.. yenyewe evaporator yake unakuta ni part kitako mahala vitu vinakaa, na zingine unakuta kuna pipe zimepita ndani .

So to conclude ni kwamba hakuna shida fridge kuiacha kwenye umeme na by the way ndivo inavotakiwa iwe.. kwakua ukizima fridge ukaiwasha baadae fridge itakula umeme mwingi kwakua it will work harder kufikia temperature ile ulii set kwenye knob yake.. but ukiacha kwenye umeme, fridge itakua inafanya kazi ya ku-mantain temperature tu. So itawaka kidogo na kuzima yenyewe.. na circle itaendelea.

Ila ikitokea thermostat imekufa basi fridge itafanya kazi muda mwingi bila kuzima na haitakua na mechanisms ya ku control temperature.. na ikitokea na sensor ya Frost direction imekufa au timer imekufa situation ndo itakua worse kwakua after sometime fridge itajaza barafu na ita perform vibaya hasa kama fridge ni non frost... Lakini pia kumbuka refrigeration kwakua inafanya kazi on principles of pressure difference between low side and high pressure ... So evaporator ikiwa na barafu sana itafanya low pressure ipungue sana nakufanya gas inayotakiwa irudi kwenye compressor ili iwe compressed isiwepo au iwe ndogo sana so compressor inaweza ku overheat na kufa kwakua hakuna enough cold refrigerant inayo rudi kupoza compressor... Na ndo maana ukiangalia AC system ya gari inakua na sensors/switch inayo monitor pressure ya low na high side kwamba pressure zikiwa out of range (both sides yaan low au high) basi the system shuts off to protect itself.

So ndo hivo.. sorry nimejibu kirefu kidogo japo system ina mambo kidogo..
 
Back
Top Bottom