Wamiliki wengi wa majokofu/friji wanauelewa mdogo juu ya utendaji kazi wake

Wamiliki wengi wa majokofu/friji wanauelewa mdogo juu ya utendaji kazi wake

Pia kama una AC, hapa panakuhusu.

Twende moja kwa moja kwenye mada. Watu wengi tunamiliki majokofu au friji lakini tunauelewa mdogo juu ya utendaji wa hichi kifaa. Kimsingi, kama mtumiaji hautakiwi kuwa na uelewa sana juu ya utendaji wa jokofu lako. Wataalamu au mafundi wanaohudumia jokofu lako wakati wa matatizo ndio wanatakiwa wawe na uelewa na wakupe miongozo mbalimbali juu ya kifaa chako. Kwa bahati mbaya sana, mafundi wengi wa majokofu hawana uelewa huo. Hapa ndipo tatizo linapoanzia na kukulazimu mmiliki wa jokofu uwe na ABC fulani juu ya kifaa chako, kitu ambacho si cha lazima sana. Na hapo ndipo nilipoona kuna haja ya kuleta kwenu uzi huu.

Kiini cha uzi huu ni kuhusu tatizo la ujazaji wa gesi kwenye majokofu yetu Pamoja na AC za majumbani kwetu.

Ili tuweze kuelewana vizuri, naomba nielezee jinsi mfumo wa upoozaji ndani ya jokofu unavyofanya kazi.

Kimsingi mfumo wa upoozaji kwenye jokofu lako una sehemu kuu kama tatu hivi. Yaani COMPRESSOR, CONDENSER, NA EVAPORATOR.

Compressor kazi yake ni kuisukuma gesi iweze kuzunguka kwenye mfumo wa upoozaji. Inaisukuma gesi kwenda kwenye EVAPORATOR, ikitoka kwenye EVAPORATOR inaenda kwenye CONDENSER na kurudi tena kwenye COMPRESSOR, mzunguko unaanza tena na kuendelea. CONDENSER na EVAPORATOR ni mirija au tube katika muundo wa zigizaga zilizotengenezwa kwa shaba au malighafi nyingine yoyote inayoweza kubadilishana jotoridi kwa wepesi kama kielelezo cha mchoro kinavyoonyesha hapo chini.

View attachment 2278705
Wakati gesi inafanya mzunguko au inazungushwa kati ya CONDENSER na EVAPORATOR ndipo inapofanya upoozaji. EVAPORATOR huwa iko ndani ya jokofu, yaani mule kwenye kabati ya baridi. CONDENSOR huwa nje ya jokofu upande wa nyuma. Gesi wakati inazunguka, ikipita kwenye EVAPORATOR inachukua lile joto na kwenda nalo nje kwenye CONDENSOR. Ikifika kwenye CONDENSOR inaliachia lile joto na gesi kuwa imepoa, inarudi tena kwenda kukusanya joto ndani ya jokofu na kulileta nje na kuliachia. Kwa gesi kufanya mzunguko huo na kazi ya kutoa joto ndani ya jokofu, ndani ya jokofu hubaki na ubaridi. Hapo chini kuna kielelezo cha picha
kikionyesha jinsi mpangilio wa COMPRESSOR, EVAPORATOR, na CONDENSER unavyokuwa kwenye jokofu.

View attachment 2278707

GESI

Tumeona kwamba, gesi kwenye jokofu kazi yake ni kuzunguka, kuchukua joto ndani ya jokofu na kulileta nje na kuliachia. Inasukumwa kurudi ndani kuchukua tena joto kupitia EVAPORATOR, inakujanalo nje na kuliachia kupitia CONDENSER.

TAMBUA

Katika hali ya kawaida, gesi katika jokofu lako haitakiwi kuisha. Tumeona hapo juu jinsi gesi inavyofanya kazi ndani ya jokofu lako. Haiungui kama mafuta ya gari tuseme kwamba inaisha. Gesi ipo kwenye mzunguko wa mduara ambao umefungwa na hufanya kazi kupitia mirija kama tulivyoelezana hapo juu. Yaani unaweza ukazaliwa mpaka unazeeka, jokofu lako likawa linapoza kama kawaida. Na bahati mbaya sana mafundi wengi wa mifumo ya kupooza hawajui kwamba gesi haitakiwi kuisha katika hali ya kawaida.

Sababu moja kubwa ya kuisha gesi kwenye jokofu ni kuvuja kwa gesi. Pale ambapo kunakuwa na tundu kwenye mfumo wa mzunguko wa gesi na gesi kuanza kuvuja.

Kwanza fundi anatakiwa atatue tatizo la kuvuja kwa gesi ndipo ajaze gesi kwenye kifaa chako. Tofauti na hapo anakupa suluhu ya muda mfupi tu kwa kujaza gesi bila kuzuia kuvuja. Baada ya muda mfupi utamtafuta akujazie tena gesi. Kisheria huu ni wizi. Yawezekana wanafanya makusudi, inawezekana pia hawajui kwamba lazima kutakuwa na tatizo la gesi kuvuja sababu katika hali ya kawaida gesi haitakiwi kuisha. Pia inawezekana fundi anajua ila hataki kujisumbu. Au anajua ila anauhakika hutamlipa gharama za kutafuta leakage au panapovuja.

Kama una jokofu lako ambalo unajaza gesi kila baada ya muda Fulani, sasa ni wakati wa kulitengeneza na kuzuia kuvuja ili kuepuka gharama zisizo za lazima. Fundi anatakiwa atafute gesi inapovujia, adhibiti hiyo sehemu. Baada ya hapo atafanya majaribio ya kuhakiki kama mfumo hauna sehemu inayovujisha gesi. Jaribio hilo atalifanya kabla ya kujaza gesi. Na jaribio hilo la kuhakiki afya ya mfumo linaitwa ‘pressure test’. Baada ya kufanya pressure test na kujiridhisha afya ya mfumo wa upoozaji, atafanya ‘vacuum’. Hapa ataondoa hewa iliyoingia kwenye mfumo wa upoozaji. Sababu baada ya gesi kuvuja na kuisha, hewa ya kawaida huchukua nafasi na kuingia kwenye mfumo. Hii hewa haitakiwi. Endapo gesi itajazwa bila kutoa hewa iliyoingia, ufanisi wa gesi kupooza utapungua na utashangaa kwamba jokofu langu sikuhizi halipoozi vizuri. Ni kama mafuta ya gari uchanganye na kimiminika kingine. Lazima ufanisi wa mafuta utapungua. Ndani ya mfumo wa kupooza inatakiwa iingie gesi peke yake ili ifanye kazi kwa ufanisi wa juu.

Katika pitapita yangu na kukutana na mafundi wa mifumo ya kupooza, sikumbuki kumuona fundi ana ‘vacuum pump’. Yaani pump au kifaa cha kuondolea hewa kwenye mfumo wa kupooza wa jokofu au AC.

Nawatakia upambanaji mwema.

Wakatabahu

Infopaedia
Maelezo mazuri, asante. Nimekumbuka sayansi yangu ya sekondari. Una ujuzi wowote wa ufundi kwenye Fridge/Air condition?
 
Maelezo mazuri, asante. Nimekumbuka sayansi yangu ya sekondari. Una ujuzi wowote wa ufundi kwenye Fridge/Air condition?
Asante kaka. Nina ujuzi ila siufanyii kazi kwa sasa. Lakini kama una tatizo la kiufundi na uko Dar es salaam usisite, tuwasiliane. Kuna kijana ninayemuamini atakusaidia.
 
Naomba kujua Zaidi kuhusu hizi number. Mimi Nina Pinetech ndogo Ina namba 1-7 ila sijui maama yake
Nqmba1_7 hizi ni namba ya ku set temperature unayotaka kwenye compartment ya fridge yako.. kadiri namba zinavo panda ndivo unavo ongeza ubaridi kwenye compartment ya fridge yako lakini pia the same applies to power consumption.. number kubwa maana yake fridge inafanya kazi muda mrefu ku attain ile temperature so more energy consumption..
 
Asante kaka. Nina ujuzi ila siufanyii kazi kwa sasa. Lakini kama una tatizo la kiufundi na uko Dar es salaam usisite, tuwasiliane. Kuna kijana ninayemuamini atakusaidia.
Asante. Nilitaka tu kuuliza. Kuna dhana kuwa mabasi ya abiria yenye air condition, hizo air condition hazidumu kwenye mazingira ya nchi kama Tanzania, je ni kweli? Basi likinunuliwa jipya na air condition zinaweza kudumu muda gani?
 
Nashukuru kwa pongezi kaka. Wakati naandika huu uzi niliwalenga watumiaji wa majokofu. Hivyo sikutaka kuwachosha sana na habari za kitaalamu.
Mkuu Buzitata kazi ya Thermostatic expansion valve ni kuibadili gesi kutoka maji maji na kuwa mvuke. Hii gesi ikiwa katika mfumo wa mvuke ina tabia ya kufyonza joto, hata liwe kidogo italifyonza. Yaani inatabia ya kuhitaji joto ikiwa kwenye mfumo wa mvuke ndani ya evaporator. Baada ya hapo ikipita kwenye compressor huwa imesharudia tena kwenye hali yake ya kimiminika. Na ikiwa kwenye hali ya kimiminika, gesi ya Freon huwa na tabia ya kutoa joto. Yaani inakuwa kinyume na wakati ikiwa kwenye hali ya mvuke. Inakuwa inafyonza au inahitaji zaidi ubaridi. Baada ya hapo inapita tena kwenye expansion valve, expansion valve inaigandamiza na kui-spray ndani ya evaporator kuwa hali ya mvuke na mzunguko unaendelea.
Jokofu hutumia kanuni ya kuondoa joto ili kupata ubaridi. Nikupe mfano wa giza na mwanga. Kwa asili dunia ni giza. Taa au jua likiwaka ndio hulizidi giza japokuwa wakati wote giza lipo. Kinachotokea ni kwamba mwanga unalizidi uwiano giza, basi giza halionekani.
Na kwa habari ya joto na baridi ni hivyo hivyo. Dunia yetu ni baridi isipokuwa msuguwano ndio husababisha joto na kuja kuiondoa baridi, japo baridi wakati wote ipo ila uwiano na joto au jotoridi huegemea upande wa joto hivyo tunahisi joto zaidi. Ama jotoridi ikiegemea upande wa baridi tunasema kuna baridi.
Kwahiyo jokofu hutumia kanuni ya kuliondoa joto, kinachobaki ni ubaridi. Hakuna kitu kinachotengeneza ubaridi kwenye jokofu.
Ila kaka uko unakokwenda sio unajua tabia za gesi? Unajua hata hii mitungi ya majumbani wakati inajazwa inakua katika hali gani? Na unajua gesi ingiwa kwenye mkandamizo kisha ukaifungulia gafla inakua kwenye hali gani?
 
Nina fridge yangu Hisense ilifika kipindi ghafla ikawa haipozi nikamwita fundi akasema gesi imeisha na kuna kijidude kilikuwa baina ya compressor na pipe za gas akasema nako ni kabovu akahamisha mfumo wa condenser kutoka ndani akaweka nyingine nje ila lilikuwa linakula umeme na kupiga kelele balaa.

Mimi nadhani vitu kama frij na umeitumia zaidi ya miaka nane kama mtu una uwezo usijihangaishe na mafundi wa kibongo nunua nyengine maana mimi nilimuuliza huyo fundi kitaalam kabisa kwamba ikiwa mwanzo ndani ya mwezi nilikuwa natumia umeme wa 20K nyumba nzima mbona baada ya wewe kuitengeneza huo umeme unaisha ndani ya siku 19?anasema nitakuja na kipimo kupima labda niliweka gas nyingi yupo “unajua gas ikiwa nyingi compressor inakula sana umeme” nikamwambia njoo upime akaja akapima still tatizo likaendelea.

Akasema ah ah tatizo litakuwa earth rod nikamwita fundi wangu wa umeme akakagua nyumba nzima hamna penye leakage fundi fridge akahamisha kesi akasema kile chuma cha earth rod ni fake madai yake ni nondo siyo copper halisi nikaita tena fundi akaichimbua akaikwaruza kwa sururu kiasi cha kuichimba kabisa ni original kwa ufupi hakuweza kutatua lile tatizo japokuwa fij ilikuwa inafanya kazi but target haikuwa lile umeme,nilijutia muda na gharama nilizotumia bora ningenunua jipya toka mwanzo.
 
Ndio sababu tunazisitiza elimu isiwe ya kukariri ili tupate wataalam wazuri , nimemsoma mtoa mada vizuri sana , anajua na kujitahidi , ila kuna vitu unaona kabisa kavimeza kama vilivyo , na hawezi tena kutoka nje ya hiyo knowledge cycle ,
Ubaridi kwenye freezer na fridge unaaznia kutoka kwenye expansion valve ,
Yeye ameanzisha wewe ongezea, iwe amekariri au laa!!

Tumenufaika na hili kwahyo ukiona kuna sehem pamesalia ongezea mkuu sio lazima yote tuyapate kutoka kwake
 
Lawama zoote ni mfumo wa elimu unaotukuza pass marks na si uelewa ,
Watoto wapo busy kutafuta past papers na possible questions , unapataje experts kwa mtindo kama huo? Watu wanakariri na kufaulu imeisha hiyo.
Huna shukrani,
We unafikiri huyo expert anapatikana darasani peke yake??

We subiri tu watu waanzishe ili ukosoe,,
 
buzitata
Mi naomba unifahamishe kuhusu hili,
Nina freezer ila hizi evaporator zimewekwa kwa nje(yaani zinaonekana ndani ya freezer Kuna shida ilitokea fundi akashauri kufanya hivo)

Sa shida ninayopata nikwamba halieleweki yaani Kuna siku unaweza kuweka namba moja(min) ikagandisha saana, siku nyingine ukiweka hapo utakesha.

Siku nyingine ukiweka namba saba(max) hakuna kitu au itachukua mda mrefu kugandisha

Sasa hi shida ni Nini na lipi suluhisho lake.
 
Inventor Compressor Friji/AC ulaji wake wa Units za Umeme ni mdogo mno zipo zinazotumia Units za Umeme wa kuanzia laki 3 kwa mwaka mzima (360 Days-Ikiwa ON siku zote hizo bila Kuzimwa).
Mawazo yako mazuri, lakini hujatoa hoja yako kitaalamu, Ulitakiwa useme itatumia unit kadhaa za umeme kwa mwaka badala ya kutaja pesa. Hapa Tanzania kuna viwango mbalimbali vya bei ya unit moja ya umeme, pia bei zinaweza kubadilika. Hivyo ungetaja kiwango cha unit ungeeleweka zaidi na mchango wako ungeishi miaka 100 ijayo.
 
buzitata
Mi naomba unifahamishe kuhusu hili,
Nina freezer ila hizi evaporator zimewekwa kwa nje(yaani zinaonekana ndani ya freezer Kuna shida ilitokea fundi akashauri kufanya hivo)

Sa shida ninayopata nikwamba halieleweki yaani Kuna siku unaweza kuweka namba moja(min) ikagandisha saana, siku nyingine ukiweka hapo utakesha.

Siku nyingine ukiweka namba saba(max) hakuna kitu au itachukua mda mrefu kugandisha

Sasa hi shida ni Nini na lipi suluhisho lake.
Pole sana mkuu japo sijajua tatizo la mwanzo lilikua ni lipi mpaka mkafikia huko ila ngoja nielezee kwa uchache

Hili swala la condenser wengi huwa wanalipuuzia sana (gesi ikitoka kwenye compressor lazma inahitaji kupoozwa)

Watu wengi tumezoea kuyabananisha mafriji yetu ukutani na tunasahau mafriji mengi yanatumia air cooling system iwe kwa fani au naturally.

Jaribu kuliweka friji lako kwenye space nzuri ili kuruhusu mzunguko wa hewa.

Freon isipopoozwa vizur ule upande wa high pressure nao unakua juu jambo linaloweza kupelekea trip au friji lako lisilete ubarid uliokusudiwa.

Pia sometimes hewa nayo huwa inachangia (hapa sielezei sana mafundi mchundo wasije kuniharibia mood)

Gesi ikiwa nyingi ni tatizo, ni vema inapojazwa vitumike vifaa husika.

I hope umepata mwanga kidogo.
 
Asante. Nilitaka tu kuuliza. Kuna dhana kuwa mabasi ya abiria yenye air condition, hizo air condition hazidumu kwenye mazingira ya nchi kama Tanzania, je ni kweli? Basi likinunuliwa jipya na air condition zinaweza kudumu muda gani?
Kwakweli sifahamu wala hiyo dhana sijawahi kuisikia. Ila penye wengi hapaharibiki jambo.
 
Huna shukrani,
We unafikiri huyo expert anapatikana darasani peke yake??

We subiri tu watu waanzishe ili ukosoe,,
Tulia nawe tupate madini acha ghubu! Tunawahitaji wote wanaojua kitu watoe maoni,sisi tusiojua tujifunze,mimi nipo makini hapa nina friji kimeo ,kwahiyo usiwatibue waache washushe nondo
 
Nina fridge yangu Hisense ilifika kipindi ghafla ikawa haipozi nikamwita fundi akasema gesi imeisha na kuna kijidude kilikuwa baina ya compressor na pipe za gas akasema nako ni kabovu akahamisha mfumo wa condenser kutoka ndani akaweka nyingine nje ila lilikuwa linakula umeme na kupiga kelele balaa.

Mimi nadhani vitu kama frij na umeitumia zaidi ya miaka nane kama mtu una uwezo usijihangaishe na mafundi wa kibongo nunua nyengine maana mimi nilimuuliza huyo fundi kitaalam kabisa kwamba ikiwa mwanzo ndani ya mwezi nilikuwa natumia umeme wa 20K mbona baada ya wewe kuitengeneza huo umeme unaisha ndani ya siku 19?anasema nitakuja na kipimo kupima labda niliweka gas nyingi yupo “unajua gas ikiwa nyingi compressor inakula sana umeme” nikamwambia njoo upime akaja akapima still tatizo likaendelea.

Akasema ah ah tatizo litakuwa earth rod nikamwita fundi wangu wa umeme akakagua nyumba nzima hamna penye leakage fundi fridge akahamisha kesi akasema kile chuma cha earth rod ni fake madai yake ni nondo siyo copper halisi nikaita tena fundi akaichimbua akaikwaruza kwa sururu kiasi cha kuichimba kabisa ni original kwa ufupi hakuweza kutatua lile tatizo japokuwa fij ilikuwa inafanya kazi but target haikuwa lile umeme,nilijutia muda na gharama nilizotumia bora ningenunua jipya toka mwanzo.
You had a very simple problem ambayo it could be fixed very easy... Fundi wako hajui alichokua anatakiwa afanye... Yawezekana fridge ilianza kula umeme kwakua ilikua inafanya kazi muda wote bila compressor kuzima... So fridge ilikua haina system inayo monitor temperature, na duty circle ya compressor.. kama fridge lako ni non frost maana yake pia yawezekana ali bypass sensor ya heater trigger lakini pia timer.. solution check kama thermostat inafanya kazi, timer kama ina fanya kazi, once replaced your problems will be solved
 
Safi sana, naomba kujua, nina fredge hapa, ili iwake ni lazima nizungushe ile timer, hapo itawaka kwa masaa yasiyozidi nane na inapoza vizuri na kugandisha pia. Ila baada ya hayo masaa kupita inajizima, na haiwaki tena mpk pale nikaizungushe ile timer.
Msaada wenu wataalamu. Kwanini isiwe inazima na kujiwasha yenyewe.
Natanguliza shukrani
Kwanza check kama ikiwa inawaka je ina circle on and off inapokua imefikia baridi ulio set kwenye knob yake? Kama ina circle vizuri but ikifika muda wa timer kuzimisha fridge (after every 8hrs standard) inazima na hairudi tena kuwaka (common problem kwa fridge with manual timer) basi timer itakua na shida..

Na kama hai circle "on" and"off" na mashine muda wote inapiga kazi bila kuzima mpaka wa Timer, basi check vifatavo check timer, check temperature sensor ya heater (ipo kwenye evaporator)
 
Lawama zoote ni mfumo wa elimu unaotukuza pass marks na si uelewa ,
Watoto wapo busy kutafuta past papers na possible questions , unapataje experts kwa mtindo kama huo? Watu wanakariri na kufaulu imeisha hiyo.
Kukariri ndiyo msingi wa kuelewa. Kwa maana hiyo huwezi kuelewa bila kukariri
 
Kukariri ndiyo msingi wa kuelewa. Kwa maana hiyo huwezi kuelewa bila kukariri
Ndio sababu Tanzania hatuna uvumbuzi, ukishakariri tayafi umeshajifungia kwenye duara na hutotoka humo I kamwe..
 
Nqmba1_7 hizi ni namba ya ku set temperature unayotaka kwenye compartment ya fridge yako.. kadiri namba zinavo panda ndivo unavo ongeza ubaridi kwenye compartment ya fridge yako lakini pia the same applies to power consumption.. number kubwa maana yake fridge inafanya kazi muda mrefu ku attain ile temperature so more energy consumption..
Asante sana mkuu
 
Hongera sana mtoa Mada, haya sasa tuendelee kusoma uzi mwingineee..."- Anna Makinda Voice.
 
Back
Top Bottom