Wamiliki wengi wa majokofu/friji wanauelewa mdogo juu ya utendaji kazi wake

Pia kama una AC, hapa panakuhusu.

Twende moja kwa moja kwenye mada. Watu wengi tunamiliki majokofu au friji lakini tunauelewa mdogo juu ya utendaji wa hichi kifaa. Kimsingi, kama mtumiaji hautakiwi kuwa na uelewa sana juu ya utendaji wa jokofu lako. Wataalamu au mafundi wanaohudumia jokofu lako wakati wa matatizo ndio wanatakiwa wawe na uelewa na wakupe miongozo mbalimbali juu ya kifaa chako. Kwa bahati mbaya sana, mafundi wengi wa majokofu hawana uelewa huo. Hapa ndipo tatizo linapoanzia na kukulazimu mmiliki wa jokofu uwe na ABC fulani juu ya kifaa chako, kitu ambacho si cha lazima sana. Na hapo ndipo nilipoona kuna haja ya kuleta kwenu uzi huu.

Kiini cha uzi huu ni kuhusu tatizo la ujazaji wa gesi kwenye majokofu yetu Pamoja na AC za majumbani kwetu.

Ili tuweze kuelewana vizuri, naomba nielezee jinsi mfumo wa upoozaji ndani ya jokofu unavyofanya kazi.

Kimsingi mfumo wa upoozaji kwenye jokofu lako una sehemu kuu kama tatu hivi. Yaani COMPRESSOR, CONDENSER, NA EVAPORATOR.

Compressor kazi yake ni kuisukuma gesi iweze kuzunguka kwenye mfumo wa upoozaji. Inaisukuma gesi kwenda kwenye EVAPORATOR, ikitoka kwenye EVAPORATOR inaenda kwenye CONDENSER na kurudi tena kwenye COMPRESSOR, mzunguko unaanza tena na kuendelea. CONDENSER na EVAPORATOR ni mirija au tube katika muundo wa zigizaga zilizotengenezwa kwa shaba au malighafi nyingine yoyote inayoweza kubadilishana jotoridi kwa wepesi kama kielelezo cha mchoro kinavyoonyesha hapo chini.

View attachment 2278705
Wakati gesi inafanya mzunguko au inazungushwa kati ya CONDENSER na EVAPORATOR ndipo inapofanya upoozaji. EVAPORATOR huwa iko ndani ya jokofu, yaani mule kwenye kabati ya baridi. CONDENSOR huwa nje ya jokofu upande wa nyuma. Gesi wakati inazunguka, ikipita kwenye EVAPORATOR inachukua lile joto na kwenda nalo nje kwenye CONDENSOR. Ikifika kwenye CONDENSOR inaliachia lile joto na gesi kuwa imepoa, inarudi tena kwenda kukusanya joto ndani ya jokofu na kulileta nje na kuliachia. Kwa gesi kufanya mzunguko huo na kazi ya kutoa joto ndani ya jokofu, ndani ya jokofu hubaki na ubaridi. Hapo chini kuna kielelezo cha picha
kikionyesha jinsi mpangilio wa COMPRESSOR, EVAPORATOR, na CONDENSER unavyokuwa kwenye jokofu.

View attachment 2278707

GESI

Tumeona kwamba, gesi kwenye jokofu kazi yake ni kuzunguka, kuchukua joto ndani ya jokofu na kulileta nje na kuliachia. Inasukumwa kurudi ndani kuchukua tena joto kupitia EVAPORATOR, inakujanalo nje na kuliachia kupitia CONDENSER.

TAMBUA

Katika hali ya kawaida, gesi katika jokofu lako haitakiwi kuisha. Tumeona hapo juu jinsi gesi inavyofanya kazi ndani ya jokofu lako. Haiungui kama mafuta ya gari tuseme kwamba inaisha. Gesi ipo kwenye mzunguko wa mduara ambao umefungwa na hufanya kazi kupitia mirija kama tulivyoelezana hapo juu. Yaani unaweza ukazaliwa mpaka unazeeka, jokofu lako likawa linapoza kama kawaida. Na bahati mbaya sana mafundi wengi wa mifumo ya kupooza hawajui kwamba gesi haitakiwi kuisha katika hali ya kawaida.

Sababu moja kubwa ya kuisha gesi kwenye jokofu ni kuvuja kwa gesi. Pale ambapo kunakuwa na tundu kwenye mfumo wa mzunguko wa gesi na gesi kuanza kuvuja.

Kwanza fundi anatakiwa atatue tatizo la kuvuja kwa gesi ndipo ajaze gesi kwenye kifaa chako. Tofauti na hapo anakupa suluhu ya muda mfupi tu kwa kujaza gesi bila kuzuia kuvuja. Baada ya muda mfupi utamtafuta akujazie tena gesi. Kisheria huu ni wizi. Yawezekana wanafanya makusudi, inawezekana pia hawajui kwamba lazima kutakuwa na tatizo la gesi kuvuja sababu katika hali ya kawaida gesi haitakiwi kuisha. Pia inawezekana fundi anajua ila hataki kujisumbu. Au anajua ila anauhakika hutamlipa gharama za kutafuta leakage au panapovuja.

Kama una jokofu lako ambalo unajaza gesi kila baada ya muda Fulani, sasa ni wakati wa kulitengeneza na kuzuia kuvuja ili kuepuka gharama zisizo za lazima. Fundi anatakiwa atafute gesi inapovujia, adhibiti hiyo sehemu. Baada ya hapo atafanya majaribio ya kuhakiki kama mfumo hauna sehemu inayovujisha gesi. Jaribio hilo atalifanya kabla ya kujaza gesi. Na jaribio hilo la kuhakiki afya ya mfumo linaitwa ‘pressure test’. Baada ya kufanya pressure test na kujiridhisha afya ya mfumo wa upoozaji, atafanya ‘vacuum’. Hapa ataondoa hewa iliyoingia kwenye mfumo wa upoozaji. Sababu baada ya gesi kuvuja na kuisha, hewa ya kawaida huchukua nafasi na kuingia kwenye mfumo. Hii hewa haitakiwi. Endapo gesi itajazwa bila kutoa hewa iliyoingia, ufanisi wa gesi kupooza utapungua na utashangaa kwamba jokofu langu sikuhizi halipoozi vizuri. Ni kama mafuta ya gari uchanganye na kimiminika kingine. Lazima ufanisi wa mafuta utapungua. Ndani ya mfumo wa kupooza inatakiwa iingie gesi peke yake ili ifanye kazi kwa ufanisi wa juu.

Katika pitapita yangu na kukutana na mafundi wa mifumo ya kupooza, sikumbuki kumuona fundi ana ‘vacuum pump’. Yaani pump au kifaa cha kuondolea hewa kwenye mfumo wa kupooza wa jokofu au AC.

Nawatakia upambanaji mwema.

Wakatabahu

Infopaedia
Ahsante kwa maelezo murua.

Binafsi Friji yangu ina partition 2. Juu na chini. Ila takribani miezi 2 nime baini, partition 1, ya chini haipoozi vitu (matunda, nk). Ila partition ya juu ina fanya kazi kama kawaida.

Bado sija tafuta fundi. Naomba mwanga ktk tatzo hili ndg.
 
Pole sana kwa kadhia ya jokofu lako. Kama jokofu lako lina kipima jotoridi sehemu ya chini. Basi yawezekana hakifanyi kazi ipasavyo au ni kibovu kabisa. Kama jokofu ni la familia pia angalia kipima jotoridi kipo nambari ngapi. Yawezekana kuna mtu kakizungusha na kuweka kipimo cha chini kabisa.
Vilevile yawezekana mzunguko wa gesi si mzuri na sehemu ya chini haipati mzunguko sahihi. Hapo kwenye mzunguko wa gesi kuna sababu anuwai zinazoweza kupelekea hilo tatizo. Ukipata fundi mzuri anaweza kusaidia kujua chanzo cha tatizo.
Ila kabla hujamuita fundi, pia angalia kama mlango wa chini unafunga na kusiliba. Nitakupa kisa kimoja mwishoni.
Kusiliba kwa mlango wengi tunaona ni swala dogo, lakini husababisha ufanisi mkubwa kwenye jokofu lako. Unaweza kupima kwa kuangalia juhudi unayotumia wakati wa kufungua mlango. Wakati jokofu linafanya kazi, fungua mlango halafu ufunge. Jaribu tena mara ya pili kuufungua muda huohuo. Angalia kiwango cha juhudi au nguvu unazotumia wakati wa kuufungua mara ya pili. Kama unatumia nguvu fulani kuufungua, basi mlango uko sawa. Yaani unafunga na kusiliba. Ila kama unaona mlango unafunguka bila juhudi yoyote, basi kuna walakini kwenye mlango. Shughulikia kwanza mlango, hakikisha ukifunga unasiliba na unatumia nguvu kidogo kuufungua. Kama shida itaendelea angalia swala la kipima jotoridi na hatimae tafuta mtaalamu aliyekaribu.
Pia nakushauri pitia uzi huu andino baada ya andiko. Nadhani kuna watu pia wana tatizo kama lako na kuna watu wamejaribu kuwasaidia. Kuna mambo mengi ya kujifunza hata utakapomuita fundi utakuwa na misingi itakayokusaidia kubaini kama fundi huyo atakupa kile unachotarajia. Hata mimi kuna vitu nimejifunza kwenye huu uzi. Ila vitu nilivyojifunza vimenisikitisha zaidi. Nimejifunza kuwa kuna mafundi wanaamini kwenye jokofu kuna kifaa kinachotengeneza ubaridi. Nilichukulia hilo na mengine mengi kama funzo kwangu.

Mlango
Nilisema nitakupa kisa cha mlango mwishoni. Basi bwana, ni kama majuma matatu yamepita. Siku hiyo nipo nyumbani na sikumbuki nilikuwa naangalia nini kwenye jokofu upande wa chini ambako ndiko kwenye ubaridi mkali. Nikakuta vitu havina ubaridi kabisa. Kuuliza nikaambiwa sikuhizi upande wa chini haupozi kabisa. Wakati naufunga ule mlango, nikahisi hali tofauti katika ufungaji wake. Nikaufungua, ukafunguka kama vile uliegeshwa tu. Nikaanza kufuatilia, nikagundua kuna viraba fulani kwenye wigo wa mlango havijakaa vizuri. Inaonekana vilichomoka na kuna mtu akaamuwa kurudishia lakini akapachika mahali tofauti. Matokeo yake vinazuia mlango kusiliba. Nikauliza wote mule ndani wakakana kugusa mlango wa jokofu. Na mule ndani ni mama watoto na msaidizi wetu. Vile viraba vina reli yake, wakati wa kusafisha jokofu kama hauko makini vinaweza kutoka na usijue vimetokea wapi. Basi baada ya muda wa kuwaza na kuwazua, nilifanikiwa kuvipachika vile viraba kwenye reli zake. Nikafunga mlango ukashika na kusiliba. Jokofu likarudia upya wake.
 
Ahsante.

Nime fanya zoezi la mlango ni nime kagua raba za mlango ziko sawa. Na mlango una nata hivi ku ufungua.

Nime angalia kile kidude cha Temp. Control mshale upo kwenye optimal (yaani kati ya Cold na Coldest). Version ni Samsung -Digital Inverter (mpya/siyo used).

Huenda hiyo sababu ya Mzunguko wa Gesi haupo Normal.
 
Baada ya kusoma
Nmeangalia angalia kidogo fridge yangu
Nmejifunza kitu
Pia mwenyewe nna ufundi kidogo hivyo n sawa nakusema nmeongeza kitu
IMG_7659.jpg
 
Ahsante kwa maelezo murua.

Binafsi Friji yangu ina partition 2. Juu na chini. Ila takribani miezi 2 nime baini, partition 1, ya chini haipoozi vitu (matunda, nk). Ila partition ya juu ina fanya kazi kama kawaida.

Bado sija tafuta fundi. Naomba mwanga ktk tatzo hili ndg.
Zima yawezekana kuna barafu inazuia airflow kwenye compartment ya fridge yako (kama una non frost fridge) fanya experiment ifuatayo jioni moja zima fridge yako toa kwenye umeme, iache mpaka asubuhu ili kama kuna barafu zote zitoke, then asubuh au machana irudishe kwenye umeme uone je itafanya kazi vizuri? Ikiwa sawa basi ujie shida ni barafu iliziba air flow kwenye compartment.but why barafu? Ni kwasababu ya kuacha milango wasi muda mrefu for no reason then moisture inakua introduced ndani ya fridge na kwenda kwenye evaporator kutengeneza Frost (barafu), then barafu ina restrict airflow.
 
Ahsante

Nitafanya hiyo test mkuu.

Mm nipo Mwanza. Mafundi wa Mwanza, mlete contacts zenu.
 
Inategemea na aina za kazi unazofanya, non frost ni nzuri na very efficient ila linataka kuwe na umeme wa uhakika ,
Yale ya frost ni ya kizamani na hayapo effiecient ila unaweza ukainjoi barafu hata kama umeme umekatika kwa muda
Kwa matumizi ya nyumbani non frost ipo poa ila kibiashara chukua tu yale ya kuweka barafu
Duuh basi mie nilikuwa najua yale mabarafu huwa watu wanaweka vitu vikiwa na maji maji kama ni container hufuti n.k. Basi hata nilivyonunua navyoona haina mabarafu nikajua kwa kuwa vitu tunaviweka vikiwa havina majimaji kwa nje mpaka zile container zilizohifadhia vitu. Nakumbuka long time ilikuwa umeme ukikatika unakuta maji yanachuruzuka sakafuni, nadhani hizo frost sidhani kama zipo madukani sasa hivi maana nyingi tunazonunua dukani ni non frost kwa elimu uliyotoa hapa, unless ununue kwa special request kutoka kwa muuzaji
 
Fridge nyingi za mtumba wanachomea compressor... So unaweza kuta wanaweka compressor ndogo inayoshindwa kujaza ubaridi unaotakiwa ndani ya muda unaotakiwa (though this subject to heat load na level of insulation ya fridge na mahali utapoiweka panajoto kiasi gan kuruhusu condenser ifanye kazi vuzuri. Na kuweza kusave umeme as much as possible.

Sasa kuhusu unachokitaka maana yake unabidi upat fridge ambayo ni non frost, ambayo heater, timer,frost sensor pamoja na thermostat zote zinafanya kazi vile inavotakiwa..

Kuhusu kumwaga maji ni kwamba refrigeration system yoyote huwa ina mwaga maji pale panapokua na humidity kubwa kwenye cool surface lakini pia pale cool surface (evaporator) inapokua na barafu inayotokana moisture (angalia ac za majumbani utakuta inadondosha maji nje ikiwa unafanya kazi, ac za magari, au hata ukiweka maji ya baridi kwenye glass utakuta kwa nje ile glass kwa nje tayari inatengeneza maji, why because of temperature deference kati ya source ya baridi na surroundings palipo na high humidity)

Sasa namna ya kuepuka maji kwenye fridge yanayotokana na moisture ni kuhakikisha mlango wa fridge haubaki wazi kwa muda mrefu... Mlango wa fridge ukibaki wazi huruhusu moisture kuingia na moisture kwakua inakua na elements za maji huenda kutengeneza barafu kwenye evaporator...

Lakini pia kwa fridge zilizo vizuri zinakuja na mechanisms ya ku handle situations kama hizi ili kuhifadhi maji yanayotengenezwa na fridge.. ndo issues ya heater, frost sensor na timer zinapokuja kufanya kazi yake sasa.. ina maana utakuta fridge nyuma ya compressor kuna container ya kupokea maji pale fridge inapo washa Heater kuondoa barafu kwenye evaporator, so barafu itayeyuka yale maji yatashuka kwenye container iloyo nyuma ya fridge.. hivo occasionally mtu unaweza kua unaangalia kama kile ki container kina maji au lah.. but hii hali ni mara chache kutokea kam hauna tabia ya kuacha mlango wa fridge wazi kwa muda mrefu.

Ukinunua fridge ya mtumba ambayo ni frost basi hii changamoto utakua nayo hasa ukiwa unaweka vitu vikiwa vinachuruzika maji ndani ya fridge.. na hasa umeme ukikatika.

Wauzaji wakupe warranty, kawashe fridge, weke thermostat kwenye setting ndongo hata number 1 ili fridge ifanye kazi muda mfupi kutest kwanza thermostat inafanya kazi au lah...

Mbili hakikisha fridge ina timer na timer inafanya kazi(kama timer ni ya manual unaweza test kirahisi.. wawashe fridge then azungushe timer manually mpaka fridge izimike then awashe kwa kuzungusha timer, hapa itakusaidia kujua uzima wa timer na wiring ya hiyo fridge used.

Issue ya heater kama inafanya kazi kwa pale si rahisi kuingundua unless uwefundi afungue na a test resistance ya heater kama ipo sawa na sensor yake.. unless uende utumie smbapo fungua mlango wa frigde uku ikiwa on kama dakika tano ili ijaze moisture ndani (upande wa freezer) then funga acha ifanye kazi mpaka evaporator itapo jaa barafu, alafu angalia je vitu ndani ya freezer vimeanza kuganduka/ubaridi umeanza pungua huku compressor inafanya kazi/huku fridge inaunguruma? kama ni hivo maana yake barafu imejaa na fen ndani ya freezer inashindwa kusukuma upepo wa kutosha kwakua evaporator imejaa barafu.. so maana yakr hapa either heater au sensor ya heater au vyote kwa pamoja havifanyi kazi. (So ukiwa na warranty kwa case kama hii ni kwamba unaweza rudisha fridge au ukawambia wakutengenezee)
mkuu friji langu ni la mtumba,.lina fridge juu na freezer chini, linagandisha fresh, changamoto yake halizimi na kuwaka, yaani ukiliwasha, kitawaka 24 bila hata kuzima, lina mfumo wa frost, na consuption ya umeme wameandika 90w, niliwasha siku nzima nione je lina kula umeme kiasi gani for 24hrs, nikaona ni kama 1.7 unit, je kwa utumiaji huo wa umeme liko sawa?
 
Mi niko na swali moja hivi nataka kujua.

Natakiwa niliche friji kwa muda gan bila kuliwasha ikiwa limetoka kwenye mtikisiko wa usafiri. Labda nikiwa limetoka mtaa mmoja kwenda mtaa mwingine kwa usafiri wa kirikuu.
 
Langu lilikua jipya lg niliambiwa masaa 7
 
Pia kama una AC, hapa panakuhusu.

Twende moja kwa moja kwenye mada. Watu wengi tunamiliki majokofu au friji lakini tunauelewa mdogo juu ya utendaji wa hichi kifaa. Kimsingi, kama mtumiaji hautakiwi kuwa na uelewa sana juu ya utendaji wa jokofu lako. Wataalamu au mafundi wanaohudumia jokofu lako wakati wa matatizo ndio wanatakiwa wawe na uelewa na wakupe miongozo mbalimbali juu ya kifaa chako. Kwa bahati mbaya sana, mafundi wengi wa majokofu hawana uelewa huo. Hapa ndipo tatizo linapoanzia na kukulazimu mmiliki wa jokofu uwe na ABC fulani juu ya kifaa chako, kitu ambacho si cha lazima sana. Na hapo ndipo nilipoona kuna haja ya kuleta kwenu uzi huu.

Kiini cha uzi huu ni kuhusu tatizo la ujazaji wa gesi kwenye majokofu yetu Pamoja na AC za majumbani kwetu.

Ili tuweze kuelewana vizuri, naomba nielezee jinsi mfumo wa upoozaji ndani ya jokofu unavyofanya kazi.

Kimsingi mfumo wa upoozaji kwenye jokofu lako una sehemu kuu kama tatu hivi. Yaani COMPRESSOR, CONDENSER, NA EVAPORATOR.

Compressor kazi yake ni kuisukuma gesi iweze kuzunguka kwenye mfumo wa upoozaji. Inaisukuma gesi kwenda kwenye EVAPORATOR, ikitoka kwenye EVAPORATOR inaenda kwenye CONDENSER na kurudi tena kwenye COMPRESSOR, mzunguko unaanza tena na kuendelea. CONDENSER na EVAPORATOR ni mirija au tube katika muundo wa zigizaga zilizotengenezwa kwa shaba au malighafi nyingine yoyote inayoweza kubadilishana jotoridi kwa wepesi kama kielelezo cha mchoro kinavyoonyesha hapo chini.

View attachment 2278705
Wakati gesi inafanya mzunguko au inazungushwa kati ya CONDENSER na EVAPORATOR ndipo inapofanya upoozaji. EVAPORATOR huwa iko ndani ya jokofu, yaani mule kwenye kabati ya baridi. CONDENSOR huwa nje ya jokofu upande wa nyuma. Gesi wakati inazunguka, ikipita kwenye EVAPORATOR inachukua lile joto na kwenda nalo nje kwenye CONDENSOR. Ikifika kwenye CONDENSOR inaliachia lile joto na gesi kuwa imepoa, inarudi tena kwenda kukusanya joto ndani ya jokofu na kulileta nje na kuliachia. Kwa gesi kufanya mzunguko huo na kazi ya kutoa joto ndani ya jokofu, ndani ya jokofu hubaki na ubaridi. Hapo chini kuna kielelezo cha picha
kikionyesha jinsi mpangilio wa COMPRESSOR, EVAPORATOR, na CONDENSER unavyokuwa kwenye jokofu.

View attachment 2278707

GESI

Tumeona kwamba, gesi kwenye jokofu kazi yake ni kuzunguka, kuchukua joto ndani ya jokofu na kulileta nje na kuliachia. Inasukumwa kurudi ndani kuchukua tena joto kupitia EVAPORATOR, inakujanalo nje na kuliachia kupitia CONDENSER.

TAMBUA

Katika hali ya kawaida, gesi katika jokofu lako haitakiwi kuisha. Tumeona hapo juu jinsi gesi inavyofanya kazi ndani ya jokofu lako. Haiungui kama mafuta ya gari tuseme kwamba inaisha. Gesi ipo kwenye mzunguko wa mduara ambao umefungwa na hufanya kazi kupitia mirija kama tulivyoelezana hapo juu. Yaani unaweza ukazaliwa mpaka unazeeka, jokofu lako likawa linapoza kama kawaida. Na bahati mbaya sana mafundi wengi wa mifumo ya kupooza hawajui kwamba gesi haitakiwi kuisha katika hali ya kawaida.

Sababu moja kubwa ya kuisha gesi kwenye jokofu ni kuvuja kwa gesi. Pale ambapo kunakuwa na tundu kwenye mfumo wa mzunguko wa gesi na gesi kuanza kuvuja.

Kwanza fundi anatakiwa atatue tatizo la kuvuja kwa gesi ndipo ajaze gesi kwenye kifaa chako. Tofauti na hapo anakupa suluhu ya muda mfupi tu kwa kujaza gesi bila kuzuia kuvuja. Baada ya muda mfupi utamtafuta akujazie tena gesi. Kisheria huu ni wizi. Yawezekana wanafanya makusudi, inawezekana pia hawajui kwamba lazima kutakuwa na tatizo la gesi kuvuja sababu katika hali ya kawaida gesi haitakiwi kuisha. Pia inawezekana fundi anajua ila hataki kujisumbu. Au anajua ila anauhakika hutamlipa gharama za kutafuta leakage au panapovuja.

Kama una jokofu lako ambalo unajaza gesi kila baada ya muda Fulani, sasa ni wakati wa kulitengeneza na kuzuia kuvuja ili kuepuka gharama zisizo za lazima. Fundi anatakiwa atafute gesi inapovujia, adhibiti hiyo sehemu. Baada ya hapo atafanya majaribio ya kuhakiki kama mfumo hauna sehemu inayovujisha gesi. Jaribio hilo atalifanya kabla ya kujaza gesi. Na jaribio hilo la kuhakiki afya ya mfumo linaitwa ‘pressure test’. Baada ya kufanya pressure test na kujiridhisha afya ya mfumo wa upoozaji, atafanya ‘vacuum’. Hapa ataondoa hewa iliyoingia kwenye mfumo wa upoozaji. Sababu baada ya gesi kuvuja na kuisha, hewa ya kawaida huchukua nafasi na kuingia kwenye mfumo. Hii hewa haitakiwi. Endapo gesi itajazwa bila kutoa hewa iliyoingia, ufanisi wa gesi kupooza utapungua na utashangaa kwamba jokofu langu sikuhizi halipoozi vizuri. Ni kama mafuta ya gari uchanganye na kimiminika kingine. Lazima ufanisi wa mafuta utapungua. Ndani ya mfumo wa kupooza inatakiwa iingie gesi peke yake ili ifanye kazi kwa ufanisi wa juu.

Katika pitapita yangu na kukutana na mafundi wa mifumo ya kupooza, sikumbuki kumuona fundi ana ‘vacuum pump’. Yaani pump au kifaa cha kuondolea hewa kwenye mfumo wa kupooza wa jokofu au AC.

Nawatakia upambanaji mwema.

Wakatabahu

Infopaedia
Asante mkuu kwa elimu hii muruwa kuhusu friji kiukweli tunapigwa sana na hawa wanaojiita "mafundi " unaweza kumwita fundi aje kutengeneza kumbe ndo anaharibu mazima unakuta fridge huwezi kutumia tena.
 
Shukrani kwa somo zuri..nina deep freezer nilinunua mwezi wa tatu ni (jipya kutoka dukani )..toka mwezi wa tatu mwaka huu 22 toka nimelinunua mpaka mwezi wa 11 mwanzoni lilikuwa linafanya kazi vizuri kabisa maana nalitumia kwenye biashara ya barafu na ice cream shida imeanza toka wiki iliyopita ..kiufupi haligandishi tena ila kupoza linapoza na matumizi ya umeme yameongezeka toka tatizo hilo lianze msaada tafadhari
 
Mafundi wanakuja liharibu zaidi
 
Naomba kujua, nataka kuanza kuuza Gesi za friji;
1. Maduka ya kuuza Gesi za friji kwa jumla yanapatikana maeneo gani jijini Dar es Salaam
2. Gesi za aina gani zinazotumika kwenye Friji, AC, na AC za magari na zipi zilizopitwa na wakati (yani R22 au R420 n.k.)
 
Back
Top Bottom