Dejane
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 50,587
- 71,492
Mim mwenyewe sizimi aiseeLimetengenezwa kuwaka maisha yake yote.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mim mwenyewe sizimi aiseeLimetengenezwa kuwaka maisha yake yote.
Hata mimi huwa sizimi... Umeme ukatike, urudi lipo tu.Mim mwenyewe sizimi aisee
Na we pia unachanganya, kazi ya expansion valve ni kupunguza ukubwa wa pipe ambayo gesi inapita ili kuiongezea pressure na sio kwamba expansion valve ndio inatia ubaridi....Hongera mtoa mada
Ila kuna vitu umechanganya kidogo
Uhalisia ni kwamba
Gesi ikitoka kwenye compresor huwa inashika joto so direct inapitishwa kwenye condensor ili ipoozwe na hata ikipoozwa haiwi na ule ubaridi kabisa, ubarid unatokea kwenye expansion valve
Expansion valve inaletaje ubaridi?
Natolea mfano wa perfume, ukijipulizia perfume kuna kaubaridi fulan huwa unakapata na kale kaubaridi kanazalishwa na ile valve unavyoibonyeza pale ili kujispray, same same to refrigeration system expansion valve ndiyo inazalisha ubarid kwa kuspray freon gas kabla haijaingia kwenye evaporator.
Mengine upo sawa ila hapo tu ndo ulichanganya mtoa mada
Sio kweli... Expansion valve haizalishi ubaridiSawa mtoa mada, ila lengo langu nilitaka ujue kitu unachokichanganya, i hope hii kitu umeitoa darasani ila haya mambo kila siku huwa nadili nayo.
Ubard unazalishwa kwenye expansion valve hapa inabd ukubali tu mtoa mada hata kama huelewi ww meza kama lilivyo.
Kuna mengi kwenye hizi system
Sio kweli..... We fuatilia utagundua..Ndio sababu tunazisitiza elimu isiwe ya kukariri ili tupate wataalam wazuri , nimemsoma mtoa mada vizuri sana , anajua na kujitahidi , ila kuna vitu unaona kabisa kavimeza kama vilivyo , na hawezi tena kutoka nje ya hiyo knowledge cycle ,
Ubaridi kwenye freezer na fridge unaaznia kutoka kwenye expansion valve ,
Nina fridge hicense dogo mlango mmoja juu linagandisha chini ndio ile kawaida...Unless iwe ni hizi za mtumba ambazo zime njungwq jungwa na thermostat au timer haifanyi kazi...
Ipo hizi any refrigeration system ina kitu kinaitwa thermostat... Thermostat ina monitor temperature ya evaporator ambapo ndipo baridi utokea.. sasa kwenye fridge kuna knob ya kuchagua temperature unayotaka compartment yako iwe nayo.. mfano unataka compartment ya freezer iwe na temperature ya 3°c.. maana yake uta set ile thermostat to that temperature.. so compressor itafanya kazi mpaka ile temperature ifikiwe.. then ikifikiwa compressor itazima yenyewe.. then joto likipanda mfano to 4°c compressor itawaka tena ku maintain ile temperature..
Sasa hapa kwenye fridge kuna frost na non frost...
Sasa kwa fridge za non frost huwa zinakua na evaporator ambayo inakua ndani then kunakua na feni inayopuliza ule ubaridi wa evaporator kuja vitu vilivomo ndani ya fridge kuvigandisha.. sasa changamoto ya hapa ni kwamba kuna muda hii fridge hujaa barafu so kutoa hii changamoto fridge huwa zinakua na heater na timer, na sensors ya kuzuia ku trigger heater iwake. So timer inakua na circle ya kuwasha Heater ili kuyeyusha barafu inayokua imejaa kwenye evaporator ili evaporator isi restrict airflow, lakini pia mfano kipindi cha baridi kama hivi sasa kwakua joto si kubwa fridge huwai kutengeneza barafu kwenye evaporator kabla ya circle ya timer kuanza kazi, so hapa ile sensor ya ku ditect frost kwenye evaporator coil huzimisha compressor na kuwasha Heater ili kuyesha ile barafu... So hivo ndivo fridge hufanya kazi (but hizi ni kwa non frost fridges) kwa frost fridges (nyingi ni za kizamani) kidogo working principals zinautofauti kidogo hasa upande wa evaporator.. yenyewe evaporator yake unakuta ni part kitako mahala vitu vinakaa, na zingine unakuta kuna pipe zimepita ndani .
So to conclude ni kwamba hakuna shida fridge kuiacha kwenye umeme na by the way ndivo inavotakiwa iwe.. kwakua ukizima fridge ukaiwasha baadae fridge itakula umeme mwingi kwakua it will work harder kufikia temperature ile ulii set kwenye knob yake.. but ukiacha kwenye umeme, fridge itakua inafanya kazi ya ku-mantain temperature tu. So itawaka kidogo na kuzima yenyewe.. na circle itaendelea.
Ila ikitokea thermostat imekufa basi fridge itafanya kazi muda mwingi bila kuzima na haitakua na mechanisms ya ku control temperature.. na ikitokea na sensor ya Frost direction imekufa au timer imekufa situation ndo itakua worse kwakua after sometime fridge itajaza barafu na ita perform vibaya hasa kama fridge ni non frost... Lakini pia kumbuka refrigeration kwakua inafanya kazi on principles of pressure difference between low side and high pressure ... So evaporator ikiwa na barafu sana itafanya low pressure ipungue sana nakufanya gas inayotakiwa irudi kwenye compressor ili iwe compressed isiwepo au iwe ndogo sana so compressor inaweza ku overheat na kufa kwakua hakuna enough cold refrigerant inayo rudi kupoza compressor... Na ndo maana ukiangalia AC system ya gari inakua na sensors/switch inayo monitor pressure ya low na high side kwamba pressure zikiwa out of range (both sides yaan low au high) basi the system shuts off to protect itself.
So ndo hivo.. sorry nimejibu kirefu kidogo japo system ina mambo kidogo..
Hata mim paleeHata mimi huwa sizimi... Umeme ukatike, urudi lipo tu.
Ni hiyo Fridge guard nimeweka hapo linaji'control lenyewe[emoji2]
Mkuu ile inaitwa expansion valve!! Anzia hapo kwanza ndo tuendelee !Sio kweli..... We fuatilia utagundua..
Gas inafika kwenye valve ikiwa ya baridi... Valve inafinya tu kuiongezea pressure.
Ila sio inaipa ubaridi... Bali wewe ndio unaanza kuuona ubaridi pale
Sent using Jamii Forums mobile app
Haya ndio madhara ya kikariri , muwe mnasoma na kuelewa wazee sio kukariri. mwishowe tutaonekana tuna madharau !!!Na we pia unachanganya, kazi ya expansion valve ni kupunguza ukubwa wa pipe ambayo gesi inapita ili kuiongezea pressure na sio kwamba expansion valve ndio inatia ubaridi....
Valve ile inafinya tu pipe ili gesi itoke ikiwa na pressure.
Sent using Jamii Forums mobile app
nilizan ww ni fund boss maana nilitaka musaada wakoPia kama una AC, hapa panakuhusu.
Twende moja kwa moja kwenye mada. Watu wengi tunamiliki majokofu au friji lakini tunauelewa mdogo juu ya utendaji wa hichi kifaa. Kimsingi, kama mtumiaji hautakiwi kuwa na uelewa sana juu ya utendaji wa jokofu lako. Wataalamu au mafundi wanaohudumia jokofu lako wakati wa matatizo ndio wanatakiwa wawe na uelewa na wakupe miongozo mbalimbali juu ya kifaa chako. Kwa bahati mbaya sana, mafundi wengi wa majokofu hawana uelewa huo. Hapa ndipo tatizo linapoanzia na kukulazimu mmiliki wa jokofu uwe na ABC fulani juu ya kifaa chako, kitu ambacho si cha lazima sana. Na hapo ndipo nilipoona kuna haja ya kuleta kwenu uzi huu.
Kiini cha uzi huu ni kuhusu tatizo la ujazaji wa gesi kwenye majokofu yetu Pamoja na AC za majumbani kwetu.
Ili tuweze kuelewana vizuri, naomba nielezee jinsi mfumo wa upoozaji ndani ya jokofu unavyofanya kazi.
Kimsingi mfumo wa upoozaji kwenye jokofu lako una sehemu kuu kama tatu hivi. Yaani COMPRESSOR, CONDENSER, NA EVAPORATOR.
Compressor kazi yake ni kuisukuma gesi iweze kuzunguka kwenye mfumo wa upoozaji. Inaisukuma gesi kwenda kwenye EVAPORATOR, ikitoka kwenye EVAPORATOR inaenda kwenye CONDENSER na kurudi tena kwenye COMPRESSOR, mzunguko unaanza tena na kuendelea. CONDENSER na EVAPORATOR ni mirija au tube katika muundo wa zigizaga zilizotengenezwa kwa shaba au malighafi nyingine yoyote inayoweza kubadilishana jotoridi kwa wepesi kama kielelezo cha mchoro kinavyoonyesha hapo chini.
View attachment 2278705
Wakati gesi inafanya mzunguko au inazungushwa kati ya CONDENSER na EVAPORATOR ndipo inapofanya upoozaji. EVAPORATOR huwa iko ndani ya jokofu, yaani mule kwenye kabati ya baridi. CONDENSOR huwa nje ya jokofu upande wa nyuma. Gesi wakati inazunguka, ikipita kwenye EVAPORATOR inachukua lile joto na kwenda nalo nje kwenye CONDENSOR. Ikifika kwenye CONDENSOR inaliachia lile joto na gesi kuwa imepoa, inarudi tena kwenda kukusanya joto ndani ya jokofu na kulileta nje na kuliachia. Kwa gesi kufanya mzunguko huo na kazi ya kutoa joto ndani ya jokofu, ndani ya jokofu hubaki na ubaridi. Hapo chini kuna kielelezo cha picha
kikionyesha jinsi mpangilio wa COMPRESSOR, EVAPORATOR, na CONDENSER unavyokuwa kwenye jokofu.
View attachment 2278707
GESI
Tumeona kwamba, gesi kwenye jokofu kazi yake ni kuzunguka, kuchukua joto ndani ya jokofu na kulileta nje na kuliachia. Inasukumwa kurudi ndani kuchukua tena joto kupitia EVAPORATOR, inakujanalo nje na kuliachia kupitia CONDENSER.
TAMBUA
Katika hali ya kawaida, gesi katika jokofu lako haitakiwi kuisha. Tumeona hapo juu jinsi gesi inavyofanya kazi ndani ya jokofu lako. Haiungui kama mafuta ya gari tuseme kwamba inaisha. Gesi ipo kwenye mzunguko wa mduara ambao umefungwa na hufanya kazi kupitia mirija kama tulivyoelezana hapo juu. Yaani unaweza ukazaliwa mpaka unazeeka, jokofu lako likawa linapoza kama kawaida. Na bahati mbaya sana mafundi wengi wa mifumo ya kupooza hawajui kwamba gesi haitakiwi kuisha katika hali ya kawaida.
Sababu moja kubwa ya kuisha gesi kwenye jokofu ni kuvuja kwa gesi. Pale ambapo kunakuwa na tundu kwenye mfumo wa mzunguko wa gesi na gesi kuanza kuvuja.
Kwanza fundi anatakiwa atatue tatizo la kuvuja kwa gesi ndipo ajaze gesi kwenye kifaa chako. Tofauti na hapo anakupa suluhu ya muda mfupi tu kwa kujaza gesi bila kuzuia kuvuja. Baada ya muda mfupi utamtafuta akujazie tena gesi. Kisheria huu ni wizi. Yawezekana wanafanya makusudi, inawezekana pia hawajui kwamba lazima kutakuwa na tatizo la gesi kuvuja sababu katika hali ya kawaida gesi haitakiwi kuisha. Pia inawezekana fundi anajua ila hataki kujisumbu. Au anajua ila anauhakika hutamlipa gharama za kutafuta leakage au panapovuja.
Kama una jokofu lako ambalo unajaza gesi kila baada ya muda Fulani, sasa ni wakati wa kulitengeneza na kuzuia kuvuja ili kuepuka gharama zisizo za lazima. Fundi anatakiwa atafute gesi inapovujia, adhibiti hiyo sehemu. Baada ya hapo atafanya majaribio ya kuhakiki kama mfumo hauna sehemu inayovujisha gesi. Jaribio hilo atalifanya kabla ya kujaza gesi. Na jaribio hilo la kuhakiki afya ya mfumo linaitwa ‘pressure test’. Baada ya kufanya pressure test na kujiridhisha afya ya mfumo wa upoozaji, atafanya ‘vacuum’. Hapa ataondoa hewa iliyoingia kwenye mfumo wa upoozaji. Sababu baada ya gesi kuvuja na kuisha, hewa ya kawaida huchukua nafasi na kuingia kwenye mfumo. Hii hewa haitakiwi. Endapo gesi itajazwa bila kutoa hewa iliyoingia, ufanisi wa gesi kupooza utapungua na utashangaa kwamba jokofu langu sikuhizi halipoozi vizuri. Ni kama mafuta ya gari uchanganye na kimiminika kingine. Lazima ufanisi wa mafuta utapungua. Ndani ya mfumo wa kupooza inatakiwa iingie gesi peke yake ili ifanye kazi kwa ufanisi wa juu.
Katika pitapita yangu na kukutana na mafundi wa mifumo ya kupooza, sikumbuki kumuona fundi ana ‘vacuum pump’. Yaani pump au kifaa cha kuondolea hewa kwenye mfumo wa kupooza wa jokofu au AC.
Nawatakia upambanaji mwema.
Wakatabahu
Infopaedia
Suluhisho iltakiwa upate fridge za lg au samsung zenye linear compressors na digital inverter, hizi hazihitaji fride guard maana zinatembea hata imeme ukiwa 100 volts , ni ghali sana though ila ni bora .Nina fridge hicense dogo mlango mmoja juu linagandisha chini ndio ile kawaida...
Ninapoishi kuna tatizo la umeme mdogo nikawa nalitumia bila fridge guard.
Baadae nikanunua guard shida ni hii sasa
Nyakati za mchana umeme unakuwa vizuuur lakini fridge inaweza ikawaka sometime inazima lakini guard inaonesha umeme upo stable na ikizima inapoooza kabisa ukifungua vitu vyoote vimeyeyuka...
Yaani naweza nikaliacha on siku nzima umeme upo safi ila unakuta maji tu ndani ambayo imegandisha na ikayeyusha.. lakini kitambo ilikuwa ukiacha masaa 12 vitu unakuta jiwe na usiku unazima unaiwasha teena asubuh ipo safi.
Usiku huwa naizima kutokana na umeme unakuwa mdogo inashindwa kusukuma mzigo.
Sollution yake ni nin hii mkuu?
Sent using Jamii Forums mobile app
mi nisaidie mkuu!,, jokof langu linapiza kwa halaka sana upande wa frizer ni kuanzia 15min na kuendelea ila upande wa chin ina chukua mda mrefu kuanzia 1:30hr mpk 2 hr na hapa inakuwa imepoza kawaida tu yani ubarid kawaida sana,, unanisaidiaje hapa boss,, nina aina ya( HOME BASE)nipo chatoPole sana kiongozi, bahati mbaya sipo huko kwa sasa halafu pia sifanyagi kazi za individual. Ila naweza kukusaidia kutambua leakage
Fanya hiv
Chukua maji weka kwenye ndoo kisha changanya na sabuni (napendekeza ya unga kwasabab ya povu).
Ukishachanganya hakikisha unapata povu jingi.
Pia tafuta sponji au kipande cha godoro.
Washa friji lako na hakikisha compresor inafanya kazi.
Baada ya kuwasha sasa unaweza kuanza kazi ya kuitafuta hiyo leakage
Unachukua lile povu kwa sponji halafu unalikamulia kwenye viungio vyote bila kusahau ile sehem unayoingizia gesi.
Ukishakamulia lile povu kama kuna leakage lazima itaonekana.
Kwa msaada zaid ingekua vema uniambie huwa unaona dalili zipi mpaka unamuita fundi akujazie gesi (mafundi wetu muda mwingne sio waaminifu).
Ref na chiller huwa zina matatizo mengi na mengine yanataka kufanana dalili hivyo ni venga ungefunguka kodogo nikuambie wapi ukaguse kwenye friji lako
Samahani kama nitakosea mimi sio fundi. Ila kimsingi hakuna gesi inayotoa ubaridi duniani. Joto linakawaida kusafiri kutoka ambako lipo kubwa kwenda kwenye joto dogo kutengeneza "thermal equilibrium ". Kitendo hiko kikiendelea itafika hali ambayo joto la gesi ni sawa na joto la kwenye friji..Haya ndio madhara ya kikariri , muwe mnasoma na kuelewa wazee sio kukariri. mwishowe tutaonekana tuna madharau !!!
Kinachoongeza freon pressure kwenye system ya jokofu au kiyoyozi ni compressor peke yake , baada ya kutoka kwenye compressor gas hiyo hupelekwa kwenye condenser ili ipoteze joto bila kupungua pressure then itaingia kwenye expansion valve kwa ajili ya kutoa ubaridi, baada ya hapo kunaanza cycle nyingine ya compreasion.
Mwanafunzi mtoro , hebu rejea kwenye somo la kemia kidato cha pili, sijui kama mtaala wa sasa wanasoma hivyo ili sisi tulisomaSamahani kama nitakosea mimi sio fundi. Ila kimsingi hakuna gesi inayotoa ubaridi duniani. Joto linakawaida kusafiri kutoka ambako lipo kubwa kwenda kwenye joto dogo kutengeneza "thermal equilibrium ". Kitendo hiko kikiendelea itafika hali ambayo joto la gesi ni sawa na joto la kwenye friji..
Ndio maana kuna mdau aliuliza kama anaweza kutumia friji kama AC? Akajibiwa inawezekana ila umeme utahitajika mwingi. Sababu ni hiyohiyo hewa ya chumba kizima inahitaji kugusa sehemu yenye ubaridi .
Tunaomba address ama mawasiliano yako binafsi nina hitaji huduma makini kama hiiPia kama una AC, hapa panakuhusu.
Twende moja kwa moja kwenye mada. Watu wengi tunamiliki majokofu au friji lakini tunauelewa mdogo juu ya utendaji wa hichi kifaa. Kimsingi, kama mtumiaji hautakiwi kuwa na uelewa sana juu ya utendaji wa jokofu lako. Wataalamu au mafundi wanaohudumia jokofu lako wakati wa matatizo ndio wanatakiwa wawe na uelewa na wakupe miongozo mbalimbali juu ya kifaa chako. Kwa bahati mbaya sana, mafundi wengi wa majokofu hawana uelewa huo. Hapa ndipo tatizo linapoanzia na kukulazimu mmiliki wa jokofu uwe na ABC fulani juu ya kifaa chako, kitu ambacho si cha lazima sana. Na hapo ndipo nilipoona kuna haja ya kuleta kwenu uzi huu.
Kiini cha uzi huu ni kuhusu tatizo la ujazaji wa gesi kwenye majokofu yetu Pamoja na AC za majumbani kwetu.
Ili tuweze kuelewana vizuri, naomba nielezee jinsi mfumo wa upoozaji ndani ya jokofu unavyofanya kazi.
Kimsingi mfumo wa upoozaji kwenye jokofu lako una sehemu kuu kama tatu hivi. Yaani COMPRESSOR, CONDENSER, NA EVAPORATOR.
Compressor kazi yake ni kuisukuma gesi iweze kuzunguka kwenye mfumo wa upoozaji. Inaisukuma gesi kwenda kwenye EVAPORATOR, ikitoka kwenye EVAPORATOR inaenda kwenye CONDENSER na kurudi tena kwenye COMPRESSOR, mzunguko unaanza tena na kuendelea. CONDENSER na EVAPORATOR ni mirija au tube katika muundo wa zigizaga zilizotengenezwa kwa shaba au malighafi nyingine yoyote inayoweza kubadilishana jotoridi kwa wepesi kama kielelezo cha mchoro kinavyoonyesha hapo chini.
View attachment 2278705
Wakati gesi inafanya mzunguko au inazungushwa kati ya CONDENSER na EVAPORATOR ndipo inapofanya upoozaji. EVAPORATOR huwa iko ndani ya jokofu, yaani mule kwenye kabati ya baridi. CONDENSOR huwa nje ya jokofu upande wa nyuma. Gesi wakati inazunguka, ikipita kwenye EVAPORATOR inachukua lile joto na kwenda nalo nje kwenye CONDENSOR. Ikifika kwenye CONDENSOR inaliachia lile joto na gesi kuwa imepoa, inarudi tena kwenda kukusanya joto ndani ya jokofu na kulileta nje na kuliachia. Kwa gesi kufanya mzunguko huo na kazi ya kutoa joto ndani ya jokofu, ndani ya jokofu hubaki na ubaridi. Hapo chini kuna kielelezo cha picha
kikionyesha jinsi mpangilio wa COMPRESSOR, EVAPORATOR, na CONDENSER unavyokuwa kwenye jokofu.
View attachment 2278707
GESI
Tumeona kwamba, gesi kwenye jokofu kazi yake ni kuzunguka, kuchukua joto ndani ya jokofu na kulileta nje na kuliachia. Inasukumwa kurudi ndani kuchukua tena joto kupitia EVAPORATOR, inakujanalo nje na kuliachia kupitia CONDENSER.
TAMBUA
Katika hali ya kawaida, gesi katika jokofu lako haitakiwi kuisha. Tumeona hapo juu jinsi gesi inavyofanya kazi ndani ya jokofu lako. Haiungui kama mafuta ya gari tuseme kwamba inaisha. Gesi ipo kwenye mzunguko wa mduara ambao umefungwa na hufanya kazi kupitia mirija kama tulivyoelezana hapo juu. Yaani unaweza ukazaliwa mpaka unazeeka, jokofu lako likawa linapoza kama kawaida. Na bahati mbaya sana mafundi wengi wa mifumo ya kupooza hawajui kwamba gesi haitakiwi kuisha katika hali ya kawaida.
Sababu moja kubwa ya kuisha gesi kwenye jokofu ni kuvuja kwa gesi. Pale ambapo kunakuwa na tundu kwenye mfumo wa mzunguko wa gesi na gesi kuanza kuvuja.
Kwanza fundi anatakiwa atatue tatizo la kuvuja kwa gesi ndipo ajaze gesi kwenye kifaa chako. Tofauti na hapo anakupa suluhu ya muda mfupi tu kwa kujaza gesi bila kuzuia kuvuja. Baada ya muda mfupi utamtafuta akujazie tena gesi. Kisheria huu ni wizi. Yawezekana wanafanya makusudi, inawezekana pia hawajui kwamba lazima kutakuwa na tatizo la gesi kuvuja sababu katika hali ya kawaida gesi haitakiwi kuisha. Pia inawezekana fundi anajua ila hataki kujisumbu. Au anajua ila anauhakika hutamlipa gharama za kutafuta leakage au panapovuja.
Kama una jokofu lako ambalo unajaza gesi kila baada ya muda Fulani, sasa ni wakati wa kulitengeneza na kuzuia kuvuja ili kuepuka gharama zisizo za lazima. Fundi anatakiwa atafute gesi inapovujia, adhibiti hiyo sehemu. Baada ya hapo atafanya majaribio ya kuhakiki kama mfumo hauna sehemu inayovujisha gesi. Jaribio hilo atalifanya kabla ya kujaza gesi. Na jaribio hilo la kuhakiki afya ya mfumo linaitwa ‘pressure test’. Baada ya kufanya pressure test na kujiridhisha afya ya mfumo wa upoozaji, atafanya ‘vacuum’. Hapa ataondoa hewa iliyoingia kwenye mfumo wa upoozaji. Sababu baada ya gesi kuvuja na kuisha, hewa ya kawaida huchukua nafasi na kuingia kwenye mfumo. Hii hewa haitakiwi. Endapo gesi itajazwa bila kutoa hewa iliyoingia, ufanisi wa gesi kupooza utapungua na utashangaa kwamba jokofu langu sikuhizi halipoozi vizuri. Ni kama mafuta ya gari uchanganye na kimiminika kingine. Lazima ufanisi wa mafuta utapungua. Ndani ya mfumo wa kupooza inatakiwa iingie gesi peke yake ili ifanye kazi kwa ufanisi wa juu.
Katika pitapita yangu na kukutana na mafundi wa mifumo ya kupooza, sikumbuki kumuona fundi ana ‘vacuum pump’. Yaani pump au kifaa cha kuondolea hewa kwenye mfumo wa kupooza wa jokofu au AC.
Nawatakia upambanaji mwema.
Wakatabahu
Infopaedia
Mkuu samahani kama nakukwaza . Lakini tangu nausoma uzi ni wewe na buzitata ndio nimewaona mmelielezea friji kwa 100% kuliko mleta mada. Shida yangu nami nilitaka mtumie maelezo sahihi katika kila hatua kama mlivyomtaka meta mada.Mwanafunzi mtoro , hebu rejea kwenye somo la kemia kidato cha pili, sijui kama mtaala wa sasa wanasoma hivyo ili sisi tulisoma
Freon inayowekewa kwenye ac na fridge ina tendency ya kutoa baridi inaporudi kwenye ground au natural state.
Compressor inachodanya ni kuzibana gas molecules na kuzifanya kuwa katika exiced states ndo maana gas hii hupata joto kali , expansion valve sasa hufanya kinyume , kuzitoa freon katika excited state na kuirudisha katika natural state , hapa ndo freon hutoa baridi
Cooling system kiufupi ni kwamba scientist walichunguza tabia za freon wakachukua faida zake kutengeneza baridi
Nilitaka nikujibu ila najikuta roho inakataa sijui kwann . Ila jaribu hata kugoogle mkuuNa we pia unachanganya, kazi ya expansion valve ni kupunguza ukubwa wa pipe ambayo gesi inapita ili kuiongezea pressure na sio kwamba expansion valve ndio inatia ubaridi....
Valve ile inafinya tu pipe ili gesi itoke ikiwa na pressure.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hapa kuna issue kidogo... Kuna expansion valve, kuna capillary tube, kuna Orifice tube hizi zote zinafanya kazi moja but expansion valve kidogo yenyewe ina advance kwakua inakua ina regulate passage ya refrigerant kutegemeana na temperature.. na ndo maana inakua na kichwa flan hivi na kimkia hivi pamoja na pin hii inavofanya kazi ni kwamba siku joto linapokua kubwa maana yake ni kwamba more refrigerant inahitajika kuingia kwenye evaporator ili kutengeneza baridi kubwa na kwa haraka ili ku overcome heat load.. na panapo kua hakuna joto kabwa, basi expansion ita expand kidogo (itafunguka kidogo) kuruhu gas kiasi ya baridi kuingia ndani ya evaporator ili kupoza compartment ya fridge yako..Na we pia unachanganya, kazi ya expansion valve ni kupunguza ukubwa wa pipe ambayo gesi inapita ili kuiongezea pressure na sio kwamba expansion valve ndio inatia ubaridi....
Valve ile inafinya tu pipe ili gesi itoke ikiwa na pressure.
Sent using Jamii Forums mobile app